
23/7/2025
Kushi News: Taarifa kwa Vyombo vya Habari Serikali ya "Matumaini" Yageuka kuwa Jinamizi kwa Maisha ya Watu kwa Kuporomoka kwa Thamani ya Pauni!
Katika hotuba yake baada ya kuapishwa kama Waziri Mkuu, Kamel Idris alisema: "Kauli mbiu yetu ni matumaini na ujumbe ni kufikia usalama, ustawi, na maisha mazuri kwa kila raia wa Sudan!" Katika taarifa yake ya kwanza kwa vyombo vya habari, alisema atajitolea muda wake na juhudi zake ili kufikia maisha yenye heshima kwa kila Msudan.
Na tunaingia mwezi wa tatu, na baraza lake la mawaziri halijakamilika hadi sasa, na matumaini ambayo aliahidi watu yamegeuka kuwa jinamizi la kutisha, lilianza na kuporomoka kwa pauni ya Sudan dhidi ya sarafu zingine, haswa dola, ambapo soko sambamba (nyeusi) lilishuhudia ongezeko kubwa, ambapo dola moja ilizidi kizingiti cha pauni elfu 3 za Sudan, na kuzorota huku kwa kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya ndani, kulichochea bei ya mafuta na bidhaa za msingi, na kufanya maisha ya watu kuwa magumu zaidi kuliko ilivyo kutokana na vita na athari zake.
Katika hali hii mbaya, Waziri wa Fedha anatosheka na ahadi na uhakikisho ambao haushibishi wala kuondoa njaa!
Sisi katika Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan, mbele ya uminywaji huu kwa watu, tunaeleza ukweli ufuatao:
Kwanza: Miongoni mwa sababu za msingi ambazo zilisababisha na zinaendelea kusababisha hali hizi mbaya za kiuchumi ni:
a- Kuchapisha karatasi za noti bila kifuniko chini ya bendera ya kubadilisha sarafu, kisha kukamilisha mchakato wa ubadilishaji katika majimbo ya Al-Jazeera, Khartoum na mengineyo.
b- Imethibitika kuwa baadhi ya sarafu za zamani ambazo zilibadilishwa zimeweza kuingia sokoni na kurudishwa, jambo ambalo huongeza kushuka kwa thamani ya ununuzi wa sarafu.
c- Kuendelea kwa vita, na kuongezeka kwa gharama zake, pamoja na uhalifu wa vikosi vya msaada wa haraka, kwa kuharibu viwanda vya uchapishaji wa sarafu, kuiba viwanda, na kufanya mchakato mkubwa wa kughushi sarafu ya ndani.
Pili: Sheria imebainisha dhahabu na fedha kwa ajili ya shughuli za kifedha, kwa kuzingatia kwamba zina thamani ya asili, ambayo hufanya thamani ya ubadilishaji kuwa imara, lakini serikali, kwa kufuata sera za Magharibi kafiri mkoloni, zinazowakilishwa na uchapishaji wa pesa za karatasi bila kifuniko cha dhahabu, na kisha kuwasilisha kwa maagizo ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia, katika kuzingatia sera ya kuelea; ambayo imefanya sarafu yetu kushuka kila siku hadi kuzimu dhidi ya dola ambayo haifai chochote ila thamani ya karatasi na uchapishaji, kufuata kwa serikali sera hizi ndiko kulikotufikisha katika kushuka huku mbaya, licha ya utajiri wa nchi katika rasilimali dhahiri na fiche.
Tatu: Tumewafanya makafiri wakoloni kuwa na njia na mamlaka juu yetu, licha ya katazo la wazi kutoka kwa sheria, Mungu Mwenyezi anasema: ﴿Na Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini﴾, ambapo wanaingilia mambo yetu, kupitia kile kinachoitwa mikutano ya amani ya uwongo, ambayo kupitia hiyo Sudan Kusini ilitenganishwa, na sasa wanapiga ngoma za kufanya mkutano huko Washington mwishoni mwa mwezi huu, na tunachoogopa zaidi, ni kwamba uminywaji huu ni kwa tendo la mtendaji ili kukubali kile kitakachotokana na mkutano huu wa uovu unaohusiana na utenganishaji wa jimbo la Darfur.
Mwisho, tunawaambia watu wetu nchini Sudan, uminywaji huu hautasimama, na kuingilia kati kwa makafiri wakoloni waziwazi katika maisha yetu, kupitia mawakala wao wa ndani, isipokuwa Khilafah Rashidah kwa misingi ya unabii, basi fanyeni kazi na Hizb ut-Tahrir, painia ambaye watu wake hawadanganyi, ili kuiweka.
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye lile litakalo kuuhisha.﴾
Jumatano 28 Muharram 1447 AH
2025/07/23 AD
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika jimbo la Sudan
Vyanzo: Kushi News / Abu Wadaha News

