Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Shirika la Kiyahudi ndilo tatizo kubwa katika nchi za Waislamu
Na wanaoliunga mkono ndio tatizo kubwa zaidi duniani; Ewe Trump!
Vyombo vya habari vimeeneza kauli ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Gaza, ambayo anasema: "Gaza ni tatizo kubwa kwa "Israel" na Mashariki ya Kati." Hatujasikia yeyote kati ya watawala wa Ruwaibidha katika nchi za Waislamu akijibu maneno yake, na kumwambia: Kwamba shirika la Kiyahudi linalonyakua ardhi ndilo tatizo kubwa zaidi katika nchi za Waislamu, na kwamba ninyi ndio mnaoipa mashine ya kivita na msaada wa kisiasa na kiuchumi; basi ninyi ndio tatizo kubwa zaidi katika ulimwengu mzima, kwani msimamo wenu wa kibepari ndio sababu ya umaskini wa ulimwengu, na ninyi ndio sababu ya kuzigawanya nchi za Waislamu katika dola ndogo dhaifu na mashirika bandia yanayowategemea.
Rais huyu mjeuri asingeweza kutoa kauli kama hii kama angepata mtu mmoja kati ya watawala wa Waislamu anayejibu kauli yake, na kuhamasisha majeshi kuondoa shirika la Kiyahudi lililopotoka, na kumrudisha huyu anayefumbia macho ukweli katika akili yake timamu, na kwamba shirika la Kiyahudi ndilo lililonajisi ardhi iliyobarikiwa, na ndilo linalowaadhibu watu wake vibaya, bali limezidi mipaka yake kwa ujeuri wake kwa nchi jirani na za mbali pia.
Tatizo la nchi za Kiislamu lilianza tangu ilipoangushwa dola ya Khilafah mwaka 1924 BK, na kugawanywa katika dola ndogo ndogo na dhaifu, zinazodhibitiwa na makafiri wakoloni, kisha ikafuata kunyakuliwa kwa Palestina na kuanzishwa shirika la Kiyahudi lililopotoka ndani yake, kwa msaada wa Uingereza, kisha uangalizi wa Amerika, na usaliti wa watawala wa Waislamu, ambao walithibitisha shirika la Kiyahudi, kisha wakalilinda na kuwazuia Waislamu kuikomboa Palestina, huu ndio hali ya watawala wa Ruwaibidha katika nchi zetu; baadhi yao wanalinda shirika la Kiyahudi, na baadhi yao wamefanya nalo makubaliano na kubadilishana uhusiano wa kidiplomasia hadharani, na baadhi yao wameanzisha nalo uhusiano kwa kificho, na baadhi yao wanalishtaki kwa Baraza la Usalama linaposhambulia ardhi yake na mamlaka yake kwa ndege zake, na baadhi yao wanalaani mapambano ya Waislamu dhidi yake huko Palestina, na baadhi yao wanashiriki katika kuzingira watu wa Gaza, na baadhi yao wameingia katika makubaliano ya Abraham, na wote wanayazuia majeshi katika kambi zao na kuyazuia kuikomboa Palestina, na wanawazuia watu wao hata kutoa maoni yao ya kukataa mauaji katika Ukanda wa Gaza, hakika ni ubaya ulioje wanayoyafanya!
Na sisi katika Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir tunampongeza Trump na viongozi wa shirika la Kiyahudi lililopotoka, kwamba hali hii haitadumu, na mmeona mabadiliko katika maoni ya umma wa kimataifa kuelekea uhalifu wa shirika la Kiyahudi huko Gaza, na Umma wa Kiislamu umetambua kadhia yake, na unaenda kwa hatua za haraka kuelekea kuanzisha dola yake, dola ya Khilafah ambayo inajaza mioyo yenu hofu na kitisho, na wakati huo hamtasikia jibu kutoka kwa Khalifa wa Waislamu; bali mtaona majeshi makubwa ambayo ya kwanza yako kwenu na ya mwisho yako kwake, na Hizb ut Tahrir unaongoza Umma kwa hatua za haraka ili kufikia lengo hili, basi furahini kwa yale yanayowasumbua, na hakika kesho iko karibu kwa anayeingojea.
Ofisi Kuu ya Habari
Hizb ut Tahrir