Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hakuna kitakacho zuia kuenea kwa wanamgambo na majeshi sambamba isipokuwa Ukhalifa ulioongoka kwa njia ya Utume
Kongamano la Tamantai lilitangaza muungano wa kijeshi unaoitwa Vikosi vya Pamoja vya harakati za mashariki mwa Sudan, ambao unajumuisha vikosi vya Kongamano la Beja Unified Leadership linaloongozwa na Muhammad Tahir, vikosi vya Orta Mashariki vinavyoongozwa na Kamanda Al-Amin Daoud, upinzani wa wananchi, na uhamasishaji unaoongozwa na Nadir Turk. Tangazo hili linakuja huku kukiwa na vita ambavyo visingekuwepo bila kuwepo kwa jeshi sambamba na jeshi la dola; Vikosi vya Msaada wa Haraka, vita hivi ambavyo vimeangamiza kila kitu, kuharibu miundombinu, kuwahamisha watu, kukiuka heshima, na kuua maelfu ya raia wasio na hatia kwa damu baridi, baada ya yote yaliyotokea, na bado yanatokea, serikali bado inafumbia macho kuibuka kwa majeshi mapya, bali inatumia baadhi yao, ambayo inahimiza kila mtu kuunda wanamgambo na jeshi sambamba na jeshi la dola, na kibaya zaidi ni kwamba majeshi haya yote yanayokinzana yanaendeshwa chini ya itikadi potofu, ama kikanda au kikabila, na ingawa kuwepo kwake kunamaanisha uharibifu wa nchi, kupoteza nguvu zake, na kuiandaa kwa mgawanyiko na utengano ambao unataka Magharibi kafiri mkoloni ambaye alianza kwa kutenganisha kusini mwa Sudan, na sasa anajitahidi kwa hatua za haraka kutenganisha Darfur.
Mazungumzo juu ya vikosi vya pamoja mashariki mwa Sudan, ambavyo ni vikosi vya kikanda, inamaanisha kuweka mashariki mwa Sudan kwenye mashine ya kupasua. Ama kutoka kwa mtazamo wa kisheria, haifai kwa dola kuwa na majeshi mawili, achilia mbali kuwa na majeshi yanayotegemea ushabiki wa kikabila au kikanda, Mtume ﷺ anasema: «Na yeyote anayepigana chini ya bendera ya upofu, akikasirika kwa ajili ya ushabiki, au anatoa wito kwa ushabiki, au anasaidia ushabiki, kisha akauliwa, basi kifo chake ni cha kijahiliya». Na Hizb ut-Tahrir ilieleza katika rasimu ya katiba ya dola ya Khilafah umoja wa jeshi, kwani ilikuja katika kifungu cha 66 cha rasimu ya katiba ya dola ya Khilafah: (Jeshi lote litafanywa jeshi moja na kuwekwa katika kambi maalum, isipokuwa kwamba baadhi ya kambi hizi lazima ziwekwe katika majimbo mbalimbali na zingine katika maeneo ya kimkakati, na zingine zitafanywa kambi za simu ambazo ni vikosi vya kudumu, na kambi hizi zitapangwa katika vikundi vingi, kila moja ikiitwa jeshi, na kupewa nambari na kusemwa jeshi la kwanza, jeshi la tatu, kwa mfano, au kuitwa kwa jina la jimbo kutoka kwa majimbo au wilaya kutoka kwa wilaya).
Sisi katika Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan, tunathibitisha kuwa kuanzisha harakati za silaha na wanamgambo wa kikabila au kikanda hakitumikii chochote isipokuwa mpango wa kafiri mkoloni anayetaka kuipasua Sudan na kuigawanya.
Tunatoa wito kwa wenye akili timamu miongoni mwa watu wa Sudan kufanya kazi ya kukata njia kwa mipango ya kafiri mkoloni na vibaraka wake ndani, kwa kufanya kazi kwa bidii na Hizb ut-Tahrir; kiongozi ambaye hasemi uongo kwa watu wake, kuanzisha Ukhalifa ulioongoka kwa njia ya Utume, ambao unaunganisha nchi na kuondoa machafuko haya yote, bali anajitahidi kuiunganisha na nchi zingine za Waislamu.
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye yale yanayo kufufueni﴾
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan