Organization Logo

الباكستان مكتب

ولاية باكستان

Twitter: http://twitter.com/HTmediaPAK

Tel:

HTmediaPAK@gmail.com

http://www.hizb-pakistan.com/

Hali Baada ya Mvua Kubwa na Mafuriko Imedhihirisha Tena Kwamba Waislamu Wanahitaji Khalifa wa Kusimamia Mambo Yao
Press Release

Hali Baada ya Mvua Kubwa na Mafuriko Imedhihirisha Tena Kwamba Waislamu Wanahitaji Khalifa wa Kusimamia Mambo Yao

September 09, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hali Baada ya Mvua Kubwa na Mafuriko Imedhihirisha Tena

Kwamba Waislamu Wanahitaji Khalifa wa Kusimamia Mambo Yao

Tangu Juni 26, mafuriko katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, Punjab na Karachi yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 650 na kuwajeruhi zaidi ya elfu. Pia yamesomba maelfu ya nyumba pamoja na akiba, mali, na magari ya watu. Dada zetu na binti zetu - alama ya usafi na heshima - wamenyimwa nyumba zao na faragha zao, na wamelazimika kuishi nje.

Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Pakistan inashiriki Waislamu wote huzuni na masikitiko kwa msiba huu. Tunasubiri kwa uvumilivu janga hili na tunawaomba Waislamu pia kuwa na subira, kama Mtume ﷺ alivyosema: «Hakuna msiba unaompata Muislamu, uchovu wala ugonjwa, wala wasiwasi wala huzuni, wala madhara wala dhiki, hata kama ni mwiba unaomchoma, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamfutia makosa yake kwa ajili yake» Imepokewa na Bukhari na Muslim, hata hivyo, wakati huu umefichua uwezo mdogo wa watawala wetu, uzembe wao na kutojali kwao. Hii sio mara ya kwanza kwa Pakistan kuzama katika janga la mafuriko. Mafuriko ya uharibifu ya 2010 na 2022 bado yapo kwenye kumbukumbu. Katika mafuriko ya 2022 pekee, theluthi ya nchi iliathirika, na watu milioni 33 waliathirika. Pakistan ni miongoni mwa nchi kumi zilizoathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi, kwani ina zaidi ya mito ya barafu 9,000, idadi kubwa zaidi nje ya ncha za kaskazini na kusini. Kuyeyuka kwake kwa kasi kumeongeza hatari ya mafuriko.

Hata hivyo, kama ilivyo kawaida, watawala wetu huonekana tu kwa siku chache za habari, kisha kila kitu husahaulika! Kwa mfano, serikali ya mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa imetenga rupia milioni 800 tu kwa mkoa mzima, na rupia milioni 500 kwa mkoa wa Bonir, ambayo ni kiasi kisichotosha kujenga upya miundombinu au kutoa msaada wa kimsingi kwa waathirika. Sera ya watawala hawa wa kidemokrasia imejikita katika kusimamia vyombo vya habari, sio kuwahudumia watu kwa uaminifu.

Ama chini ya Khilafah, Khalifa anawajibika kusimamia mambo ya umma wote, na anawajibika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na yuko chini ya usimamizi na uwajibikaji wa umma kwake, kama Mtume ﷺ alivyosema: «...basi imamu ni mchungaji na anawajibika kwa kundi lake» Imepokewa na Bukhari na Muslim, lau Khilafah ingekuwepo leo, isingejificha nyuma ya maneno kama "wingu la ghafla," lakini ingejenga miundombinu ya taasisi na mfumo jumuishi, na ingejihusisha na upangaji wa muda mrefu, na ingechukua hatua madhubuti za kupunguza hasara. Lakini serikali zilizofuata nchini Pakistan zimepuuza jambo hili kwa zaidi ya miongo saba, kwani vipaumbele vyao daima vimekuwa kulinda maslahi ya nguvu za kikoloni. Shida za watu hazichukuliwi kwa uzito isipokuwa kwa kiwango ambacho zinaathiri kuishi kwa serikali hizo.

Na chini ya Khilafah, maisha ya Muislamu ni matakatifu, na diya hulipwa kwa kupoteza maisha ikiwa sababu yake ni sababu za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na uzembe na upungufu. Ama katika mfumo wa kidemokrasia, thamani ya mtu hupunguzwa kuwa ushawishi wa kisiasa na uwezo wa kuathiri mapambano ya madaraka. Mfumo huu wa kidemokrasia wa kibepari haujawapa Waislamu ila unyonge, kunyimwa na ulemavu. Umefika wakati wa kuuzika mfumo huu na kuanzisha Khilafah. Na Waislamu wa Pakistan, kwa kushirikiana na majeshi yetu, wanapaswa kukomesha mfumo huu uliopitwa na wakati na kuanzisha Khilafah Rashidah ya pili kwa msingi wa manhaj ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Pakistan

Official Statement

الباكستان مكتب

ولاية باكستان

الباكستان مكتب

Media Contact

الباكستان مكتب

Phone:

Email: HTmediaPAK@gmail.com

الباكستان مكتب

Twitter: http://twitter.com/HTmediaPAK

Tel: | HTmediaPAK@gmail.com

http://www.hizb-pakistan.com/

Reference: PR-0198cc96-ce20-7b9f-80d9-6d9f60a14ac0