Organization Logo

بنغلادش مكتب

ولاية بنغلادش

Tel: 8801798367640

Fax: Skype: htmedia.bd

contact@ht-bangladesh.info

Mkasa wa Milestone: Watoto Wasio na Hatia na Rubani Wetu Jasiri Touqeer, Wahanga wa Kukosekana kwa Dola Mlezi
Press Release

Mkasa wa Milestone: Watoto Wasio na Hatia na Rubani Wetu Jasiri Touqeer, Wahanga wa Kukosekana kwa Dola Mlezi

July 27, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mkasa wa Milestone: Watoto Wasio na Hatia na Rubani Wetu Jasiri Touqeer, Wahanga wa Kukosekana kwa Dola Mlezi

Mnamo siku ya Jumatatu iliyopita, Julai 21, 2025, ndege ya kivita ya aina ya (F-7 BGI) ya Jeshi la Anga la Bangladesh ilianguka katika jengo la sehemu ya msingi ya shule na chuo cha Milestone katika eneo la Uttara katika mji mkuu, kutokana na hitilafu ya kiufundi. Hii ilisababisha ajali mbaya ya kusikitisha, iliyoonyeshwa katika matukio ya kutisha ya watoto na wavulana walioungua na kukatwa viungo kati ya waliokufa na waliojeruhiwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Subhaanahu wa Ta'ala, awahurumie marehemu, na awape uponyaji wa haraka majeruhi, na tunamuomba, Jalalihi wa'alaa, awaandike wahanga miongoni mwa mashahidi Peponi, kwa kuzingatia kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: «...Na mwenye kuungua moto ni shahidi» Imesimuliwa na Ahmad, Abu Daud na An-Nasa'i.

Enyi watu: Kama tukio hili la kusikitisha lilivyoonyesha ukweli na kujitolea kwa watu, pia limefichua unafiki na kutojali kwa watawala wa kilimwengu wenye ubinafsi na vyama vya siasa. Tumeshuhudia ushiriki wa kushangaza wa watu katika shughuli za uokoaji na uchangiaji damu kwa majeruhi, na kujitolea kwa ushujaa kwa mwalimu ambaye alitoa uhai wake kuokoa angalau wanafunzi 20. Kwa upande mwingine, serikali imeshindwa kutoa misaada na matibabu ya haraka kwa watoto walioungua, pamoja na kutoa magari ya wagonjwa kuwapeleka hospitalini, wakati watu wanajua vizuri kwamba watawala hawa na wasomi wa kisiasa wanapougua, husafirishwa kwa ndege maalum za wagonjwa kwenda Singapore kwa matibabu!

Wakati watu wote walikuwa katika hali ya maombolezo kutokana na janga hili, uamuzi wa kuahirisha mtihani wa cheti cha sekondari ulicheleweshwa hadi saa sita za usiku kwa kisingizio cha "sheria", ambayo ilizua hasira kubwa kati ya wanafunzi na wazazi wao. Ama wasomi wa kisiasa wa kilimwengu wenye pupa, walikuwa wanajishughulisha na hotuba, matamko na kupiga picha ili kupata faida za kisiasa, na kuchochea vimbunga vya nadharia za njama kupitia vyombo vya habari, badala ya kuiwajibisha serikali. Wakati huo huo, mikutano ya kugawana ushawishi katika kamati ya maridhiano ya kitaifa wala ziara za uchaguzi hazikusimamishwa. Na ukweli ambao ulimwengu wote unaujua ni kwamba mfumo wa kilimwengu wa kibepari kafiri ni kiwanda cha kuzalisha watawala wenye ubinafsi, wafisadi na wasiojali.

Enyi watu: Suala la kutisha ambalo limejitokeza tena kupitia tukio hili ni kupuuzwa na uzembe wa wasomi watawala wa kilimwengu kwa miongo kadhaa katika kujenga jeshi lenye nguvu na lililoandaliwa na silaha za ubora. Matokeo yake, tunapoteza askari wetu mashujaa mmoja baada ya mwingine katika ndege za kujitoa mhanga kutokana na hitilafu, si kukabiliana na maadui! Na hii si mara ya kwanza kwa ajali ya kuanguka kwa ndege hizi za kivita kutokea Bangladesh; kwani aina hii (F-7) imekumbwa na ajali kadhaa katika miaka kumi na moja iliyopita. Na ndege hii iliyotengenezwa China, iliyonukuliwa kutoka kwa Mig-21 ya Urusi, inajulikana kwa jina la utani "Ndege ya Zamani", na uzalishaji wake ulianza katika miaka ya sitini na uzalishaji wake ulisimamishwa mwaka 2013.

Enyi watu: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Imamu ni mchunga na yeye anawajibika kwa kundi lake...» Imekubaliwa. Na Ukhalifa mtukufu wa Umma wa Kiislamu umethibitisha hilo kwa karne nyingi kupitia misimamo ya Makhalifa Waongofu, kama vile Abu Bakr na Umar, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na watawala wengine wachamungu. Na Umar, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisisitiza uwajibikaji wake kwa watu akisema: "Lau nyumbu angejikwaa kwenye ufuo wa Furati, ningeogopa kwamba Mwenyezi Mungu ataniuliza kuhusu hilo Siku ya Kiyama."

Ama mfumo huu wa sasa wa kilimwengu kafiri, ambao hauwezi hata kuhesabu maiti za watu wake kwa miongo kadhaa, unatukumbusha leo kutokuwepo kwa dola ya Khilafah mlezi ambayo tumekosa kwa zaidi ya miaka mia moja, na uhitaji mkubwa wa Umma kwake. Kutokuboresha jeshi chini ya mfumo huu kafiri kunaonyesha udhaifu wa uhuru wetu, na ni ukweli unaotukumbusha kutokuwepo kwa nguvu kubwa ya kijeshi ya Khilafah ambayo tumekosa kwa zaidi ya karne moja. Mwenyezi Mungu, Subhaanahu wa Ta'ala, ameulazimisha dola ya Khilafah kujitahidi kwa bidii kuboresha jeshi lake na kulitia nguvu. Amesema Ta'ala:

﴿Na waandalieni nguvu kama mnavyoweza, na farasi waliofungwa tayari, ili kuwatisha maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo wasiokuwa hao msiowajua. Mwenyezi Mungu anawajua.﴾.

Chama cha Ukombozi kinawaalika wana wa nchi hii wenye ufahamu, wanasiasa waaminifu, wasomi, na maafisa wa jeshi, kuharakisha kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah mlezi na yenye nguvu bila kuchelewa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Bangladesh

Official Statement

بنغلادش مكتب

ولاية بنغلادش

بنغلادش مكتب

Media Contact

بنغلادش مكتب

Phone: 8801798367640

Fax: Skype: htmedia.bd

Email: contact@ht-bangladesh.info

بنغلادش مكتب

Tel: 8801798367640 | contact@ht-bangladesh.info

Fax: Skype: htmedia.bd

Reference: PR-019839bc-a0c0-7e03-b1f1-75ab2fa3fd3b