Maombolezo ya Mwanachama wa Ofisi ya Amir, Mwalimu Ahmed Bakr (Abu Osama) ﴿Miongoni mwa Waumini wapo watu walioitimiza ahadi waliyoagana na Mwenyezi Mungu, basi wapo miongoni mwao waliokwisha timiza nadhiri yao, na wapo wanaoingojea, wala hawakubadilisha (ahadi yao) kabisa﴾
September 14, 2025

Maombolezo ya Mwanachama wa Ofisi ya Amir, Mwalimu Ahmed Bakr (Abu Osama) ﴿Miongoni mwa Waumini wapo watu walioitimiza ahadi waliyoagana na Mwenyezi Mungu, basi wapo miongoni mwao waliokwisha timiza nadhiri yao, na wapo wanaoingojea, wala hawakubadilisha (ahadi yao) kabisa﴾

Maombolezo ya Mwanachama wa Ofisi ya Amir, Mwalimu Ahmed Bakr (Abu Osama)

﴿Miongoni mwa Waumini wapo watu walioitimiza ahadi waliyoagana na Mwenyezi Mungu, basi wapo miongoni mwao waliokwisha timiza nadhiri yao

na wapo wanaoingojea, wala hawakubadilisha (ahadi yao) kabisa

Amir wa Hizb ut Tahrir, na wanachama wa ofisi ya Amir, na Diwan Al-Madhalim, na Ofisi Kuu ya Habari, na Hizb ut Tahrir kwa ujumla... wanawapa pole Umma wa Kiislamu kwa kifo cha mwanachama wa ofisi ya Amir, Mwalimu Ahmed Bakr (Abu Osama), ambaye amefariki asubuhi ya leo, tarehe ishirini na mbili ya Rabi' al-Awal 1447 Hijria, sawa na tarehe kumi na nne ya Septemba 2025 Miladia, akiwa na umri wa miaka themanini na saba.

Hakika Abu Osama alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Hizb ut Tahrir, akiwa amebeba da'wa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili kuanzisha upya maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha dola ya Khilafah Rashidah... Hakika alisimama imara juu ya haki na akaibeba da'wa hadi umauti wake, hakutishwa na tawala na ujeuri wao, wala magereza ya madhalimu ya kutisha kama magereza ya Hafez na Bashar al-Assad ambayo alikaa kwa miaka mingi! Alipotoka humo, hakukaa wala hakutulia, bali aliendeleza safari yake katika kuibeba da'wa katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nguvu na ushupavu wa wanaume haswa, na jicho lake lilitazama kuchomoza kwa alfajiri ya Khilafah na kutekelezwa kwa Uislamu kwa itikadi na mfumo wake... lakini Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, alimchagulia yale yaliyo makuu na matukufu zaidi kwa idhini yake Subhana wa Ta'ala ﴿katika makao ya ukweli mbele ya Mfalme Mwenye uweza﴾.

Mwenyezi Mungu akurehemu ewe Abu Osama, na hakika sisi tunahuzunika kwa kuachana nawe, na hatusemi ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu Subhana ﴿Ambao yanapowasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika Kwake Yeye ndio tutarejea, Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye ndio tutarejea.

Tarehe ishirini na mbili ya Rabi' al-Awal 1447 Hijria                                                                                 Ndugu yako Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah haswa

Tarehe kumi na nne ya Septemba 2025 Miladia                                                                         Na vijana wa Hizb ut Tahrir kwa ujumla

shared image 8