Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maombolezo ya Anas Al-Sharif na Wenzake
(Imetafsiriwa)
Katika jioni ya Jumapili, Agosti 10, 2025, hema ndogo ya habari mbele ya Jengo la Matibabu la Al-Shifa katika mji wa Gaza liliharibiwa kabisa na shambulio la moja kwa moja kutoka kwa chombo cha Kiyahudi, na kusababisha kuuawa shahidi kwa waandishi wa habari watano waliokuwa wakiandika mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza. Miongoni mwa mashahidi hao walikuwa waandishi wa habari Anas Al-Sharif, na Mohammed Qurayqa, na wapiga picha Ibrahim Zaher, na Moamen Aliwa, na Mohammed Nofal, Mwenyezi Mungu awarehemu na awakubali miongoni mwa manabii, wasadikifu, mashahidi, na watu wema, na hao ni rafiki wema.
Watu wa Palestina, na watu wa Gaza haswa, bado wanakabiliwa na uchokozi usio na huruma kutoka kwa chombo cha Kiyahudi na nguvu za kimataifa zinazokiunga mkono, haswa Amerika. Maisha yao, nyumba zao, heshima yao, na mahali pao patakatifu vimekiukwa bila kizuizi. Waandishi wa habari, ambao kazi yao ni kushuhudia na kupeleka ukatili huu kwa ulimwengu, wanalengwa kimfumo. Kulingana na Al Jazeera, chombo cha Kiyahudi kimeua takriban waandishi wa habari na wanahabari 270, katika ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, maadili ya kimsingi, na hata kanuni rahisi zaidi za ubinadamu.
Mfumo wa kimataifa unachukua jukumu la moja kwa moja kwa uhalifu huu. Matamko matupu ya kulaani na maonyesho ya mfano ya huzuni hayaondoi serikali uwezo wa kuchukua hatua. Wakati mamia ya maelfu wameandamana katika miji kutoka Sydney hadi Tokyo hadi London, serikali zao zimekataa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya chombo cha Kiyahudi. Wakati huo huo, nchi jirani ambazo zina majeshi yenye uwezo wa kukomesha mauaji haya zinakaa kimya.
Mauaji ya Gaza ni ishara ya kuachwa, neno ambalo halitoshi kuelezea ukubwa wa usaliti. Hukumu za mara kwa mara zinazotolewa na Umoja wa Mataifa na miji mikuu ya ulimwengu ni kwa kweli vitendo vya ushirikiano. Nchi hizi zinaendelea kutoa msaada wa moja kwa moja wa kijeshi, kisiasa na kiuchumi kwa chombo cha Kiyahudi. Hakuna kitakachokomesha uhalifu wa chombo hiki au kukishitaki isipokuwa Ukhalifa ulioongoka kwa njia ya Utume, kama alivyobashiri Mtume ﷺ: «Kisha itakuwa ufalme wa kidhalimu, na itakuwa chochote ambacho Mwenyezi Mungu anataka iwe, kisha atakiinua atakapo, kisha itakuwa Ukhalifa kwa njia ya Utume» Ameipokea Ahmad.
Ukhalifa ulioongoka ndio mfumo pekee wa kisiasa na kijeshi wenye uwezo wa kuilinda Gaza na nchi zote zilizodhulumiwa za Waislamu. Umma lazima udai kuondolewa kwa watawala wao ambao wanazuia majeshi yao kutekeleza wajibu wao. Na majeshi haya yanapaswa kujitenga nao, na kuhamasisha kuinusuru Gaza, na kuwapa nusra wale wanaofanya kazi kwa ikhlasi ili kusimamisha Ukhalifa, yaani, Hizb ut-Tahrir.
Wajibu huu unaondoa wasiwasi kutoka moyoni mwa kila Muislamu anayetaka kuwasaidia Waislamu na kutetea mahali pao patakatifu. Hii ndiyo njia madhubuti.
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye jambo linalo kufufueni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu huingilia baina ya mtu na moyo wake, na kwamba kwake Yeye mtakusanywa.﴾
Haitham bin Thabit
Mwakilishi wa Habari wa Hizb ut-Tahrir
Amerika