Organization Logo

أفغانستان المكتب

ولاية أفغانستان

Tel:

hizbuttahrir.af@gmail.com

Mwisho wa uvamizi wa kijeshi wa Marekani na Jumuiya ya kujihami ya NATO ni fursa ya kukabiliana na ukoloni mambo leo laini na kuelekea kwenye Ukhalifa kwa mfumo wa Utume!
Press Release

Mwisho wa uvamizi wa kijeshi wa Marekani na Jumuiya ya kujihami ya NATO ni fursa ya kukabiliana na ukoloni mambo leo laini na kuelekea kwenye Ukhalifa kwa mfumo wa Utume!

September 02, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mwisho wa uvamizi wa kijeshi wa Marekani na Jumuiya ya kujihami ya NATO

ni fursa ya kukabiliana na ukoloni mambo leo laini na kuelekea kwenye Ukhalifa kwa mfumo wa Utume!

(Imetafsiriwa)

Miaka minne iliyopita, tarehe 31 Agosti 2021, uvamizi wa kijeshi wa Marekani na vikosi vya Jumuiya ya kujihami ya NATO (NATO) nchini Afghanistan, ambao ulidumu kwa miongo miwili, uliisha kwa kuondoka kwa askari wa mwisho wa Marekani kutoka humo saa sita za usiku. Hii inatokana hasa na mabadiliko ya lengo la Marekani kuelekea eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki, ili kupunguza kasi ya maendeleo ya China. Nchi ya Kiislamu, hasa Afghanistan na watu wake wanamgambo, imekuwa chanzo cha usumbufu kwa Marekani, na chanzo cha kukengeusha fikira zake kutoka kwa mkakati huu mpya. Tunabariki na tunaendelea kubariki mafanikio haya ya kihistoria na siku hii kuu kwa Waislamu wote, hasa watu wa Afghanistan, kampeni ya Da'wah, na wanamgambo.

Miaka hii minne ingeweza kuwa fursa ya kihistoria ya kutekeleza Uislamu kikamilifu na mwanzo wa mabadiliko makubwa nchini Afghanistan. Kama vile Dola ya Kiislamu ya Madina, katika miaka yake minne ya kwanza, ilivyoanzisha misingi ya umma, na kuweka kanuni wazi za siasa za ndani na nje, na kuimarisha uwepo wa Uislamu katika uwanja wa kimataifa, mfumo tawala nchini Afghanistan pia ungeweza kutumia fursa hizi muhimu kuweka mfumo wazi na mahususi kwa sera zake za ndani na nje, ukitumia Uislamu sio tu kama kauli mbiu, bali kama mfumo kamili na mtindo wa maisha katika nyanja za utawala, uchumi, elimu, mahakama na mambo ya nje.

Lakini, kwa bahati mbaya, fursa hii kubwa haikutumiwa ipasavyo. Badala ya kutekeleza Uislamu kikamilifu, baadhi ya hukumu zake zilitumika kwa kuchagua na hatua kwa hatua kulingana na mapendeleo ya kibinafsi, na ndani ya mifumo iliyorithiwa kutoka kwa mfumo wa zamani wa jamhuri na muundo wa taifa la kisasa. Kama matokeo, vipengele wazi na tofauti vya Dola ya Kiislamu havikubainishwa; na sera za kigeni hazikuzingatia Da'wah na Jihad; na umma haukuona dalili za mabadiliko ya kweli ya Kiislamu nchini Afghanistan. Kinyume chake, lengo limehamia katika kufikia utulivu wa ndani ndani ya mipaka ya kitaifa, kutafuta kutambuliwa kwa mfumo wa kimataifa, na kufikia usawa kati ya nguvu za kimataifa; ambayo ni mbinu ambayo inadhoofisha uhalali wa mfumo kwa muda mrefu.

Licha ya mwisho wa uvamizi wa kijeshi, ukoloni mambo leo laini bado upo, ambao ni aina ya hila zaidi ya aina za utawala, unaopenya katika siasa, uchumi na fikra. Huwatiisha mataifa kutoka ndani, bila kelele za vita au uvamizi wa kijeshi. Aina hii ya ukoloni mambo leo hudanganya kwa uhuru, lakini hudhoofisha utashi wa umma, na huzuia utekelezaji kamili wa Uislamu. Uzoefu wa kihistoria unaonyesha kuwa mataifa mara nyingi hushindwa na nguvu laini kuliko nguvu za kijeshi. Kwa hiyo, kukabiliana na changamoto hii kunahitaji umakini na ufahamu wa kisiasa, na kufukuzwa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na balozi za kigeni, na kujitolea kikamilifu kwa Uislamu.

Hatimaye, tunawakumbusha ndugu zetu wanamgambo kwamba fursa haijapotea bado, lakini inapaswa kutumiwa kwa busara, na kwamba ushindi huu wa kihistoria ubadilishwe kuwa jiwe la msingi na daraja la kuanzisha Ukhalifa ulioongoka kwa mfumo wa Utume. Ukhalifa unaounganisha umma, unaondoa ukoloni mambo leo, na unapeleka ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu. Vinginevyo, kuna hofu ya kweli ya kupoteza faida za siku hii kuu. Na kama ilivyotokea huko nyuma, Afghanistan inaweza kuanguka tena katika dimbwi la ukoloni mambo leo na udhaifu, kama Mungu Mtukufu alivyoonya: ﴿Na mkigeuka, atawaleta watu wengine badala yenu, kisha hawatakuwa kama nyinyi﴾.

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Afghanistan

Official Statement

أفغانستان المكتب

ولاية أفغانستان

أفغانستان المكتب

Media Contact

أفغانستان المكتب

Phone:

Email: hizbuttahrir.af@gmail.com

أفغانستان المكتب

Tel: | hizbuttahrir.af@gmail.com

Reference: PR-0199001d-d860-7951-91b5-1d0f9c65abc9