Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wanawake wa Kashmir Wamekuwa Wakibakwa na Kuteswa na Ukaliaji wa Kihindi Tangu 1947
(Imetafsiriwa)
Katika kikao cha sitini cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka huu, jukwaa la kimataifa la mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni za wanawake lilifanyika, lililoandaliwa na Shirika la Kimataifa la OCAPROCE chini ya kauli mbiu "Wanawake kwa ajili ya kukuza na kulinda urithi wa kitamaduni na kujenga amani endelevu ifikapo 2030". Dkt. Shoughfta, mwakilishi wa Kashmir, aliangazia masaibu ya wanawake wa Kashmir mikononi mwa vikosi vya kigaidi vya kijeshi vya India vinavyokalia ardhi hiyo. Alisema: "Nimesimama mbele yenu leo kwa sauti inayoashiria maumivu ya wanawake wasiohesabika waliokimya katika bonde la Jammu na Kashmir linalokaliwa na India. Sauti za risasi zimezama mayowe yao, na heshima yao imeraruliwa na uvamizi ambao hautumii risasi tu, bali pia miili yao, kama silaha za vita." Alitoaa wito kwa mfumo wa kimataifa kuchukua hatua za kukomesha unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake wa Kashmir, na kuwawajibisha waliohusika.
Mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yameitembelea Kashmir ili kuandika matukio ya unyanyasaji na ubakaji dhidi ya raia, na yale waliyoripoti yalikuwa ya kutisha. Jeshi la India, vikosi vya polisi vya akiba ya kati, na vikosi vya usalama vya mpakani vyote vinahusika katika unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake wa Kiislamu huko Kashmir, kwa lengo la kuwadhalilisha na kuwaadhibu, pamoja na kuwa njia ya kuwalazimisha wanaume wa Kiislamu wanaoshukiwa kuwa na misimamo mikali kujisalimisha. Wanawake pia wanauawa bila kesi, hupofushwa kimakusudi, na nyumba zao, maduka, na vijiji vyote huchomwa moto kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Kwa kuongezea, mashine ya propaganda ya India inawaonyesha wanawake wa Kashmir wa Kiislamu kama viumbe wazuri wanaosubiri wanaume Wahindu kuwaoa na kuwafanya Wahindi. Hatua hizi zote ni mipango iliyopangwa kwa uangalifu na serikali ya India kama njia ya kupanua ajenda ya jimbo la kikoloni la Wahindutva huko Kashmir kwa kuwatenga na kuwatisha wakaazi wa asili wa Waislamu.
Kashmir ni ardhi nyingine ya Kiislamu inayokaliwa, iliyokuwa ikitawaliwa na sheria ya Mwenyezi Mungu, na ilielezewa kama "paradiso ya dunia." Lakini tangu Waingereza walipoingia India mwaka 1608, na utawala wao wa moja kwa moja wa bara Hindi baada ya karibu miaka 150, imekuwa nchi ya njaa, umaskini, ukosefu wa usalama na mgawanyiko. Utawala huu duni wa kikoloni ulibadilishwa na serikali ya Magharibi iliyoandaliwa chini ya kivuli cha uhuru mnamo 1947, na ilikaliwa na jimbo la Wahindutva, kama vile Wayahudi wanavyokalia Palestina iliyobarikiwa, na imekuwa haiwezekani kwa Waislamu.
Hata hivyo, mwaka wa 2025, baada ya kushuhudia matamshi matupu ya taasisi za kimataifa kuhusu mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wayahudi huko Gaza, wengi bado wanatazamia taasisi hizo hizo, kama vile Umoja wa Mataifa, ambao ulianzishwa ili kuhakikisha utawala wa Marekani, na ambayo iliruhusu wavamizi kuchukua udhibiti na kudumisha nchi yetu kwanza kabisa, kutatua tatizo la unyanyasaji na ubakaji huko Kashmir! Na baada ya miongo kadhaa ya kuona ulimwengu ukiwaona wanawake wa Kashmir wakidhihakiwa, kutengwa na kulazimishwa, tunaweza kuona hakika kwamba taasisi hizi za kimataifa na pia serikali za Magharibi hazitaweza kukomesha ukiukwaji wa heshima ya dada zetu. Badala yake, kuanzishwa kwa dola inayotawaliwa na Uislamu pekee, na hivyo kutambua umuhimu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu anaipa ulinzi wa heshima na ustawi wa mwanamke Muislamu, ndio pekee utakomesha unyanyasaji wa dada zetu huko Kashmir, Palestina, Turkestan Mashariki na kwingineko. Dola hii ni Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo itakusanya jeshi lake kutetea heshima ya dada zetu popote walipo, kama vile Khalifa Al-Walid bin Abdul-Malik alimtuma kamanda mkuu wa Kiislamu Muhammad bin al-Qasim akiwaongoza jeshi kubwa kuwaokoa baadhi ya wanawake Waislamu waliotekwa na mfalme dhalimu wa Kihindu, Raja Daher, na kumfunga gerezani, pamoja na kwamba mji mkuu wa Khilafah ulikuwa Damascus wakati huo. Kwa hivyo, tunapaswa kuelekeza juhudi na umakini wetu katika kuanzisha Khilafah haraka iwezekanavyo. Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Fuateni yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, wala msifuate walinzi badala Yake. Ni machache mnayoyakumbuka﴾.
Sehemu ya Wanawake
Katika Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir