Jarida la Habari la Jumatatu kutoka Redio ya Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Syria 2025/07/28
Jarida la Habari la Jumatatu kutoka Redio ya Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Syria 2025/07/28

Msafara wa misaada unaendelea kwenda As-Suwayda na vyama vyake vya wafanyakazi vinatangaza kukatisha uhusiano na Dameski.

0:00 0:00
Speed:
July 28, 2025

Jarida la Habari la Jumatatu kutoka Redio ya Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Syria 2025/07/28

Jarida la Habari la Jumatatu kutoka Redio ya Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Syria

2025/07/28M

Mada Kuu:

  • Msafara wa misaada unaendelea kwenda As-Suwayda na vyama vyake vya wafanyakazi vinatangaza kukatisha uhusiano na Dameski.
  • Usomaji wa kina wa kile kinachoendelea huko As-Suwayda na mpango wa Amerika nchini Syria unategemea msingi mkuu katikati ya matamko ya kupuuzia kutoka kwa Rais wa serikali.
  • Jordan inapanga kuisaidia Syria kwa kujaza mitungi elfu 40 ya gesi kila siku.

Maelezo:

Asubuhi ya leo Jumatatu, msafara mpya wa misaada ya kibinadamu umewasili katika kivuko cha Basra Al-Sham katika eneo la mashariki la Daraa, ukienda kuelekea jimbo la As-Suwayda, ukiwa umebeba chakula, misaada na vifaa vya matibabu. Msafara huo, ulioratibiwa na Hilali Nyekundu ya Kiarabu ya Syria kwa msaada wa serikali ya Syria na jamii ya wenyeji, ulijumuisha malori 27 yenye tani 200 za unga, vikapu 2,000 vya makazi, vikapu 1,000 vya chakula, pamoja na vifaa mbalimbali vya matibabu.

Vyama kadhaa vya kitaaluma na vya kiraia katika jimbo la As-Suwayda vimetangaza kukatisha uhusiano wao na vyama vya kati huko Dameski, kulalamikia kile walichoeleza kama kupuuza kwa serikali kuu matukio ya hivi karibuni ambayo yameshuhudiwa katika jimbo hilo, na ukimya wake kuhusu ukiukwaji dhidi ya raia. Mwanzo ulikuwa jioni ya Jumamosi, Julai 26, wakati chama cha wahandisi wa kilimo - tawi la As-Suwayda liliweka taarifa ya kuomboleza wanachama wake wanne, na kupitia hiyo walitangaza kusitisha mawasiliano na chama kikuu, hadi "kuondolewa kwa mamlaka ya sasa na kuanzishwa kwa mamlaka inayowakilisha watu wa Syria na kulinda utu wao", kulingana na usemi wao. Taarifa za kususia ziliendelea kutoka kwa vyama vingine vya wafanyakazi, haswa chama cha walimu huko As-Suwayda, ambacho kilitangaza "uhuru wake kutoka kwa mamlaka kuu", kikiizingatia Dameski "mshirika katika damu", na kilisema katika taarifa yake kwamba wanafunzi wa jimbo hilo hawakuweza kufanya mitihani ya shule ya upili, licha ya juhudi ambazo walimu walifanya.

Kituo cha Al Jazeera kilimnukuu chanzo cha serikali ya Syria, kikisema leo Jumatatu, kwamba hali katika jimbo la As-Suwayda inazidi kuwa hatari na ngumu, kwa sababu ya kuenea kwa vikundi vya watu wenye silaha visivyodhibitiwa vinavyozuia kuingia kwa taasisi za serikali, na vinazuia huduma za umma. Chanzo hicho kiliiambia Al Jazeera kwamba habari za kijasusi zinaonyesha matukio ya mauaji huko As-Suwayda, huku vikundi vya watu wenye silaha vikizuia Wizara ya Afya kurekodi matukio haya, ikisisitiza ugumu wa kubaini maeneo salama yanayoruhusu mashirika ya kimataifa kutoa msaada, kwa sababu ya udhibiti wa vikundi hivi katika maeneo makubwa.

Katika jibu la swali kuhusu ukweli wa matukio yanayoendelea huko As-Suwayda? Na kile ambacho chombo cha Kiyahudi kinapanga kwa eneo la As-Suwayda na kusini mwa Syria kwa ujumla, na je, Amerika inakisaidia katika upangaji wake? Na uhusiano wa yote haya na yale yanayotajwa kuhusu mazungumzo ya kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya serikali ya Syria na chombo cha Kiyahudi, haswa kile kilichotokea kutoka kwa mikutano ya Azerbaijan na Paris? Amir wa Hizb ut-Tahrir, msomi mkuu Ata Abu Al-Rashtah alisema: Kwa kuzingatia matukio nchini Syria, inaonekana kwamba Amerika inayaendesha kwa mpango ambao haukuanza leo, ingawa umeongezeka baada ya kuja kwa Rais wa Amerika Donald Trump, na aliongeza jibu: Ni wazi kwamba mpango wa Amerika nchini Syria unategemea msingi mkuu, ambao ni kuchukua nafasi ya kibaraka na kibaraka mwingine, na kwa sababu hiyo, ilipa Uturuki mwanga wa kijani kubomoa utawala wa Bashar na kujenga utawala mpya unaoifuata, katikati ya matamko ya kupuuzia kutoka kwa Rais mpya wa Syria ambayo yanaonyesha kukubalika kwake kwa ubadilishaji huu, na akaongeza jibu: Inasikitisha sana kwamba Syria ya Sham, ambayo Mtume ﷺ alisema kuihusu: «KITOVU CHA NYUMBA YA UISLAMU NI SHAMU», inakuwa chini ya utawala unaoongozwa mbali na Uislamu na kwamba mtawala wake anajikita katika utiifu kwa Amerika na unyenyekevu kwa chombo cha Kiyahudi bila kupigana nacho, lakini badala yake anatafuta kufanya makubaliano ya amani nacho, na kufanya kile kinachopendeza chombo hiki na msaidizi wake Amerika ... hata amewaweka vijana wa Hizb ut-Tahrir, walinganiaji wa Khilafah Rashidah, gerezani na hakuwatoa humo ili kuipendeza Amerika na Mayahudi maadui wa Khilafah na watu wake, akidhani kuwa kumpendeza adui wa Mungu kutahifadhi utawala wake! Alihitimisha jibu: Tuna hakika kwamba Khilafah itarudi baada ya ufalme huu wa kidhalimu tunaouishi: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: «Kisha kutakuwa na Khilafah juu ya njia ya Utume. Kisha akanyamaza». Na wakati huo Uislamu na Waislamu wataheshimiwa, na ukafiri na makafiri watadharauliwa ... na wabashirie Waumini.

Wizara ya Nishati nchini Syria na mwenzake nchini Saudi Arabia, jana Jumapili, zilitia saini hati ya makubaliano ya kimkakati yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali za nishati. Sherehe ya utiaji saini, iliyofanyika katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, ilihudhuriwa na idadi ya maafisa na wawakilishi wa sekta za umma na binafsi, na hati hiyo ilijumuisha vifungu vinavyohusiana na kuimarisha uhusiano wa nchi mbili katika nyanja za umeme, nishati mbadala, unganisho la umeme wa kikanda, mafuta na gesi, tasnia ya petrochemical, na teknolojia ya kisasa, pamoja na kuimarisha uwezo wa binadamu, kusaidia uvumbuzi, na kuhamisha na kuanzisha teknolojia katika nchi hizo mbili.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Kusafisha Mafuta ya Petroli ya Jordan, Mhandisi Hassan Al-Hayari, alitangaza kuwa kuna mazungumzo ya hali ya juu na upande wa Syria ya kuipatia Syria hadi mitungi elfu 40 ya gesi ya nyumbani kila siku wakati wa msimu wa joto, kupitia mitambo ya kusafisha na kujaza katika jiji la Zarqa. Al-Hayari alieleza, katika taarifa za wanahabari, kwamba mradi huo bado uko katika hatua za masomo ya kiufundi na vifaa, na unatarajiwa kuwasilishwa rasmi kwa upande wa Syria, huku akisisitiza kwamba utekelezaji utategemea idhini ya Wizara ya Nishati ya Jordan na mamlaka husika, ikiwa ni pamoja na kuratibu usafirishaji na usafiri kupitia mipaka. Al-Hayari alieleza kuwa mpango huo unategemea kupokea mitungi tupu kutoka Syria na kuijaza katika kituo cha Salah al-Din cha kujaza gesi kaskazini mwa ufalme, kisha kuirejesha katika ardhi ya Syria ili kukidhi mahitaji ya wakazi kusini. Alisisitiza kwamba kipaumbele kitapewa soko la ndani la Jordan, haswa wakati wa msimu wa baridi.

Mkuu wa Mamlaka Kuu ya Usafiri wa Anga wa Syria, Omar Al-Hosari, alitangaza kuwa Mamlaka inafanya kazi ya kutekeleza mpango mkakati wa kina unaolenga kurejesha miundombinu ya sekta ya usafiri wa anga, na kuimarisha nafasi ya Syria kama kitovu cha kikanda katika harakati za usafiri wa anga, ndani ya maono ambayo yanaenea hadi mwaka 2030. Katika taarifa maalum kwa shirika la habari la "Sana", Al-Hosari alieleza kuwa mpango huo unajumuisha ujenzi mpya na ukarabati wa viwanja vya ndege vilivyopo, kupanua unganisho la anga la kikanda na kimataifa, kuboresha meli za usafiri wa anga za kitaifa, pamoja na kuendeleza mifumo ya urambazaji wa anga na mawasiliano, na kufungua njia kwa ushirikiano na kampuni za ndege za kikanda na kimataifa. Alisisitiza kwamba upanuzi wa viwanja vya ndege vya Dameski na Aleppo ni kipaumbele cha kitaifa, pamoja na ukarabati wa viwanja vingine vya ndege, na kusoma uanzishwaji wa viwanja vipya vya ndege, na kuhimiza uanzishwaji wa kampuni binafsi za ndege ili kuchangia katika kuchochea harakati za anga. Al-Hosari alifichua kuhusu mradi wa kipekee ambao ni kubadilisha uwanja wa ndege wa Mazzeh, ambao kwa sasa unatumika kwa madhumuni ya kijeshi, kuwa uwanja wa ndege wa kiraia uliotengwa kwa ndege za kibinafsi na wafanyabiashara, kwa lengo la kupunguza shinikizo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dameski, na kuunda mahali pa kuvutia uwekezaji na biashara katikati ya mji mkuu.

More from null