Mtazamo wa Habari 30-10-2025
Taasisi ya Kiyahudi yavunja makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza na Amerika inaihalalisha
Idara ya ulinzi wa raia huko Gaza ilitangaza siku ya Jumatano 2025/10/29 kwamba zaidi ya watu 100, wakiwemo watoto 24, waliuawa na karibu 200 walijeruhiwa kutokana na makumi ya mashambulizi ya uchokozi kutoka kwa taasisi ya Kiyahudi iliyoyazindua siku ya Jumanne, katika ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Taasisi ya Kiyahudi inazua visingizio vya uchokozi wake, ikidai kwamba kucheleweshwa kwa kukabidhi maiti za Wayahudi huko Gaza au kuuawa kwa askari wake, ndio sababu ya mashambulizi hayo, kwani inataka kuishinikiza Hamas hadi ikabidhi maiti zote na hadi isalimu amri na iache silaha zake na vikundi vingine.
Ikiwa kukabidhi maiti zote kutakamilika, taasisi ya Kiyahudi itaendeleza uchokozi wake kwa kisingizio cha kuangamiza Hamas na kuondoa silaha kutoka Gaza. Na haitaacha uchokozi wake maadamu haipati kizuizi kutoka kwa majeshi ya Waislamu ambayo yanavuka kuelekea Palestina ili kuing'oa kutoka mizizi yake.
Maagano na makubaliano hayana thamani kwa Wayahudi kama ilivyothibitishwa katika historia yao ya zamani na ya sasa. Na wakimaliza na Gaza, wataendeleza uchokozi wao dhidi ya Ukingo wa Magharibi, Syria, Lebanon na zinginezo.
Amerika na rais wake Trump hawatafanya chochote cha maana kuelekea taasisi ya Kiyahudi isipokuwa kuwahalalishia kwamba hawajakiuka makubaliano; kwa sababu taasisi hii ni msingi wa Amerika na mkono wake wa kuwakandamiza watu wa eneo hilo na kudumisha ushawishi wake.
Watawala wa nchi za Kiislamu waliwafanya makafiri kuwa marafiki badala ya waumini na wakapendelea unyonge kuliko heshima, na kizuizi cha imani kimepotea ndani yao, kwa hivyo wamekuwa waovu na wadhalimu ambao hawahukumu kwa kile ambacho Mungu amekiteremsha. Hakuna tiba kwao isipokuwa kuwaondoa na kuondoa mifumo yao inayokiuka Uislamu kutoka mizizi yake.
----------
Njama ya Burhan na Hemeti ya kuigawanya Sudan kutekeleza mipango ya Amerika
Vikosi vya msaada wa haraka huko Sudan vilitangaza tarehe 2025/10/27 kwamba vimedhibiti mji wa Al-Fashir, mji mkuu wa mkoa wa Darfur, baada ya kudhibiti makao makuu ya Kitengo cha 6 cha watembea kwa miguu, makao makuu ya mwisho ya jeshi la Sudan katika mkoa huo.
Ikumbukwe kwamba vikosi vya msaada wa haraka vimeimarisha udhibiti wake wa magharibi, kati na kusini mwa Darfur, baada ya kujiondoa sawa kwa jeshi kutoka maeneo hayo. Hakuna kilichobaki isipokuwa kaskazini mwa Darfur, pamoja na mji wa Al-Fashir, kwa hivyo ilianza kuuzingira tangu tarehe 2024/5/10, hadi jeshi lilipojiondoa kutoka humo na kuwaangusha watu wake.
Mfuatano wa matukio nchini Sudan unaibua mashaka juu ya njama ya Burhan, kamanda wa jeshi, kujiondoa kutoka Darfur na kuikabidhi kwa vikosi vya msaada wa haraka, ambayo inatayarisha mgawanyiko wa Darfur kutoka Sudan na kutangaza uwepo wake tofauti kama ilivyotokea katika Sudan Kusini.
Kwani kamanda wa jeshi na rais wa Baraza la Utawala, Burhan, na kamanda wa vikosi vya msaada wa haraka, Hemeti, ni miongoni mwa vibaraka wa Amerika na walikubaliana kuwapiga vibaraka wa Uingereza na kisha walielewana juu ya mgawanyiko, ili mmoja wao awe madarakani na mwingine katika upinzani ili nguvu za kisiasa, pamoja na vibaraka wa Uingereza, kujiunga na upande mmoja. Kisha vikosi vya msaada vilitolewa kutoka Sudan Mashariki na kutoka mji mkuu, Khartoum, na kujiondoa kuelekea magharibi ili kuzingatia mkoa wa Darfur, na kuudhibiti. Hemeti ameunda huko baraza la utawala na serikali kama maandalizi ya kutenganisha mkoa huo.
Rais aliyeanguka, Omar al-Bashir, alikuwa ametangaza kwamba lengo la Amerika ni kuigawanya Sudan katika nchi tano, ikiwa ni pamoja na kuanzisha dola katika mkoa wa Darfur, baada ya kuikabidhi Sudan Kusini na kukiri kujitenga kwake, hata alibariki kujitenga kwake kwani alihudhuria sherehe za kutangaza uhuru wake mwaka 2011. Mungu amlaani huyo mtawala na alaaniwe mfano wake Burhan, Hemeti na wengineo ambao wanafanya njama dhidi ya nchi yao na kutekeleza mipango ya Amerika ya kukaa katika mamlaka pungufu ambayo inategemea hadi wakati, na kisha hatima yao ni kuanguka na kutoweka.
-----------
Ushindi wa kibaraka wa Amerika, Hassan Watara, nchini Ivory Coast
Jioni ya tarehe 2025/10/27, ushindi wa Hassan Watara kwa muhula wa nne nchini Ivory Coast ulitangazwa baada ya uchaguzi uliofanyika siku mbili zilizopita. Alifika madarakani kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa 2010 dhidi ya Rais wa zamani Laurent Gbagbo, kibaraka wa Ufaransa ambaye hakutaka kuachia madaraka na jeshi lililokuwa likiunga mkono Ufaransa lilikuwa likimuunga mkono. Walakini, shinikizo la Amerika lilimlazimisha Gbagbo kujiuzulu na kukubali matokeo ya uchaguzi.
Kisha Hassan Watara alishinda katika uchaguzi wa 2015 na 2020. Alipata uungwaji mkono wa Amerika baada ya kufanya kazi nayo katika Shirika la Fedha la Kimataifa ili kulazimisha sera zake zisizo za haki kwa nchi. Akawa Waziri Mkuu katika nchi yake mwaka 1990. Ufaransa, ambayo ina ushawishi katika nchi, ilimzuia Watara kuchukua urais wa nchi.
Inaonekana kwamba ushawishi wa Ufaransa umedhoofika sana nchini Ivory Coast, kwa hivyo haikuweza kuleta vibaraka wake tena. Kwani Ivory Coast, kama nchi zingine za Afrika, iko katika eneo la mzozo wa kimataifa kati ya ukoloni wa zamani unaowakilishwa na Ufaransa na Uingereza, na ukoloni mpya unaowakilishwa na Amerika. Ikumbukwe kwamba nchi nyingi kati ya hizi ni nchi za Kiislamu, kwani idadi kubwa ya watu inaundwa na Waislamu katika nyingi yao. Walakini, tatizo lao liko katika udhaifu wa ufahamu wa kiakili na kisiasa na kupanda kwa vibaraka juu ya mabega ya watu, ndio wanaowezesha ukoloni kueneza ushawishi katika nchi na kisha kuiba utajiri wake na kuwaacha watu wake maskini au wasiojiweza.

