Organization Logo

تركيا مكتب

ولاية تركيا

Tel:

bilgi@hizb-turkiye.org :

http://www.hizb-turkiye.com

Simameni na watu wa Gaza wenye msimamo, si pamoja na Trump mwenye kiburi!
Press Release

Simameni na watu wa Gaza wenye msimamo, si pamoja na Trump mwenye kiburi!

October 02, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Simameni na watu wa Gaza wenye msimamo, si pamoja na Trump mwenye kiburi!

(Imetafsiriwa)

Miaka miwili imepita tangu mauaji ya kimbari yanayofanywa na chombo cha Kiyahudi chenye kukalia ardhi kwa mabavu huko Gaza, ambacho kilifanya ili kuficha kushindwa kubwa kilikopata tarehe 7 Oktoba 2023. Miaka miwili ambayo kila siku ilishuhudia mauaji mapya, na ukatili usioelezeka, na ulimwengu mzima umeshuhudia ukatili wa Wayahudi wavamizi ambao haukubaliki akilini. Ambapo walilenga watoto, wachanga, nyumba, shule, misikiti na hospitali. Ama watawala wa nchi za Kiislamu walikutana mara kwa mara, wakazungumza na kulaani, kisha wakatengana. Na kila kulaani kulihimiza Wayahudi kufanya zaidi ya uchokozi na mauaji. Chombo cha Kiyahudi kilizidi kiasi cha kuzuia kuingia hata kipande cha mkate au tone la maji huko Gaza kwa miezi mingi.

Wauaji wavamizi hawakutosheka na Gaza, bali walishambulia Syria, Lebanon, Iran, Yemen na Qatar, kisha msafara wa msimamo uliokuwa ukitoka Tunisia. Na wakati matukio haya yote yanaendelea, Erdoğan na baadhi ya watawala wa Kiarabu walikutana New York kwenye meza ya rais wa Amerika mwenye kiburi Trump, kujadili mpango unaojumuisha kuwapokonya silaha wanamgambo, kuikalia Gaza kwa mabavu na kuihini Palestina, na walimzidi sifa.

Sisi katika Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Uturuki, katika kumbukumbu ya miaka miwili ya vita vya Wayahudi dhidi ya Gaza, tulifanya maandamano chini ya kauli mbiu "Hatutaki maneno, bali matendo", huko Istanbul, Ankara na Şanlıurfa, kwa ushiriki na msaada wa makundi ya Kiislamu, na mbele ya makumi elfu ya Waislamu. Tunasema Mwenyezi Mungu awalipe kheri makundi yote ya Kiislamu yaliyotembea nasi, na Waislamu wote walioshiriki, na wanazuoni na wahubiri waliosema ukweli bila hofu. Na wakati wa taarifa kwa vyombo vya habari zilizotolewa baada ya maandamano, tulielekeza hotuba yetu kwa watawala tukiwataka wachukue hatua za kivitendo tukisema: "Enyi mnaomiliki nguvu na mamlaka! Mmekemea, melaani vikali, na kufanya mikutano isiyo na matunda ya kidiplomasia, wakati mamia elfu ya wasio na hatia wanauawa. Na mnajua vizuri kuwa yote haya hayakuwa hatua za kweli au za kuzuia. Wayahudi wavamizi hawazuiwi na maneno, na mauaji ya kimbari ambayo yameingia mwaka wake wa tatu hayaishi kwa hotuba za shauku, na wanaodhulumiwa huko Gaza hawaokolewi kwa maneno tu. Basi huu si wakati wa maneno bali wakati wa matendo, na kinachotakiwa si taarifa za kulaani bali hatua za kivitendo za kuzuia".

Tumepaza sauti tukitaka mamlaka isimame na watu wa Gaza wenye msimamo, si pamoja na Trump mwenye kiburi, na kuhama kutoka maneno kwenda vitendo halisi. Na tulitaka kufungwa kwa kituo cha Incirlik na kituo cha rada cha Kürecik, na kunyang'anya uraia raia wenye uraia pacha wanaohudumu katika jeshi la işğal na kuwashtaki, na kukata uhusiano wa kibiashara, na uhusiano wa kidiplomasia kabisa na chombo chenye kukalia ardhi kwa mabavu, na kukataa maazimio tasa ya Umoja wa Mataifa, na kufungua njia ya kibinadamu kwenda Gaza, na kulinda msafara wa msimamo kwa wanamaji, na kulichukulia chombo cha Kiyahudi kama chombo cha kigaidi, na kusimamisha kurudiarudia mpango wa Marekani wa suluhisho la mataifa mawili.

Pia tumesisitiza juu ya umuhimu wa kusimama na wanamgambo mpaka hakuna mvamizi hata mmoja anayesalia kwenye ardhi ya Palestina. Lakini kwa bahati mbaya, siku moja tu baada ya wito huu, Erdoğan alitangaza uungaji mkono wake kwa mpango wa Trump mwenye kiburi, na akamsifu. Mpango huu, unaoungwa mkono na Uturuki na tawala za Kiarabu, unachukulia upinzani wa Gaza kama ugaidi, na unatoa uhalali kwa işğal katika Palestina yote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu mpango huu usione mwanga kamwe. Na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, wale wanaosubiri faraja kutoka kwa Trump watakatishwa tamaa sana.

Ama ujumbe wetu kwa muuaji Netanyahu na Wayahudi wavamizi ni: Enyi waoga wanyonge! Mama Waislamu wananyonyesha watoto wao chuki dhidi yenu, na baba wanawausia watoto wao kupigana nanyi, na vijana wanahesabu siku za kujiunga na jeshi litakalowashinda. Hilo ni jeshi la Khilafah Rashidah, na siku hiyo vifua vya waumini vitafurahi kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu, na nyuso za madhalimu zitatiwa giza.

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Uturuki

Official Statement

تركيا مكتب

ولاية تركيا

تركيا مكتب

Media Contact

تركيا مكتب

Phone:

Email: bilgi@hizb-turkiye.org :

تركيا مكتب

Tel: | bilgi@hizb-turkiye.org :

http://www.hizb-turkiye.com

Reference: PR-01999a43-e1a0-74c1-a8bc-5e0e1e0d7310