Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Majibu ya Serikali katika Nchi za Waislamu kwa Uchokozi wa Wayahudi dhidi ya Iran Yanaaibisha!
Mfuatiliaji wa majibu ya serikali zilizopo katika nchi za Waislamu kwa mashambulizi ya taasisi ya Kiyahudi dhidi ya Iran; moyo wake umejaa huzuni na masikitiko kwa hali iliyowafikia Waislamu, baadhi yao ni wenye kulaani na kukemea, na baadhi yao wanaogopa kutokea kwa machafuko katika eneo hilo kutokana na mashambulizi haya, na baadhi yao wanaiona kama hatua hatari, na baadhi yao wameonyesha hofu yao juu ya athari ya hatua hii kwa suala la Palestina, na baadhi yao wametangaza utayari wao wa upatanishi kati ya Iran na taasisi ya Kiyahudi, na njia yao bora zaidi ni yule aliyetangaza utayari wake wa kusimama na Iran na kuiunga mkono katika majukwaa ya kimataifa, ikijulikana kuwa baadhi yao wamefungua anga kwa ndege za taasisi ya Kiyahudi kupita juu yake na kushambulia Iran na kuua na kuharibu kisha kurudi bila kupigwa risasi hata moja! Na baadhi yao wamezuia makombora na ndege zisizo na rubani za Iran zilizokuwa zinaelekea kuishambulia taasisi ya Kiyahudi, na hivyo kuwatosheleza Wayahudi kuzizuia!
Je, hali imewafikia kiwango hiki enyi Waislamu?! Badala ya kuona ushindani kati ya nchi za Waislamu katika kutuma ndege, makombora, vifaru, mizinga na wapiganaji ili kuzuia uchokozi wa taasisi ya Kiyahudi iliyopotoka dhidi ya moja ya nchi za Waislamu; badala yake tunaona kulaani na kukemea kwa aibu! Na tunaona ujeuri katika kuonyesha upatanishi, kana kwamba anayeonyesha upatanishi ni upande usio na upendeleo usio na uhusiano wowote na Uislamu na Waislamu, na kana kwamba yeye si mtawala wa moja ya nchi kubwa za Waislamu ambayo ilikuwa mji mkuu wa Ukhalifa kwa karne tano! Na janga ni katika serikali zilizopo katika nchi zinazotenganisha Palestina na Iran, ambazo ndege za taasisi ya Kiyahudi zilipita katika anga zake, na serikali ambazo zilizuia makombora ya Iran, na janga kubwa zaidi ni katika serikali ambazo zilipokea katika viwanja vyao vya ndege raia wa taasisi ya Kiyahudi waliokuwa wanarudi Palestina baada ya kusimamishwa kwa kazi katika viwanja vya ndege vya taasisi ya Kiyahudi kutokana na makombora ya Iran dhidi ya taasisi ya Kiyahudi!
Tunajua ni kwa kiasi gani Waislamu wanatamani jihadi, na kupigana na Wayahudi, na tuliona furaha ya watu walioshuhudia makombora na ndege zisizo na rubani za Iran zikipita juu ya vichwa vyao kuishambulia taasisi ya Kiyahudi, na tuliona sherehe za watu katika nchi nyingi za Waislamu walipoona makombora na ndege zisizo na rubani hizo zikiua, kujeruhi na kuharibu katika taasisi ya Kiyahudi; kwani ziliwaonjesha Wayahudi yale waliyowaonjesha Waislamu katika Gaza, Palestina, Lebanon, Syria na Yemen, na ilikuja siku ambayo waliona taasisi ya Kiyahudi ikihesabu waliouawa, waliojeruhiwa na waliopotea kutokana na makombora na ndege zisizo na rubani hizo, kama tulivyokuwa tukifanya huko Gaza - na bado tunafanya - kutokana na uhalifu wa taasisi ya Kiyahudi na mauaji yake ya halaiki huko!
Enyi Waislamu: Hakika mnasoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: ﴿PIGANENI NAO, ALLAH ATAWAADHIBU KWA MIKONO YENU NA ATAWADHALILISHA NA ATAWASHINDENI, NA ATAZIPOA NYOYO ZA WATU WAUMINI, NA ATAONDOA GHADHABU KATIKA NYOYO ZAO﴾, na hakika mnatamani siku ambayo Mwenyezi Mungu atawashinda dhidi ya Wayahudi, na azipoe nyoyo zenu na aondoe ghadhabu katika nyoyo zenu; hakika kama mnavyosoma katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; itakuwa kwa kupigana nao kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hilo ni amri ya lazima, na ni sehemu ya itikadi ya ushindi kwenu, na amri na jibu lake katika aya tukufu ni kama sharti na jibu lake, basi maana ya aya ni: piganeni nao, kwani mkiwapiga Allah atawaadhibu kwa mikono yenu, na atawadhalilisha, na atawashindeni na atazipoa nyoyo zenu, na ataondoa ghadhabu katika nyoyo zenu.
Na huenda msemaji wenu atasema: Hakika watawala wetu wanatuzuia kupigana na Wayahudi, basi hili ni sahihi, na hili linahitaji juhudi ziunganishwe ili kuondokana na watawala hawa wajinga waliopo kuwahudumia Wayahudi na makafiri walioko nyuma yao, na sisi katika Hizb ut-Tahrir; kiongozi ambaye watu wake hawadanganyi, mwenye mradi wa Khilafah kwa njia ya Utume; tunawaalika kufanya kazi nasi na kutuunga mkono ili kuondokana na watawala hawa, na kusimamisha Khilafah Rashidah, ili Mwenyezi Mungu Mtukufu aone kutoka kwetu na kwenu anachokipenda katika kupigana na Wayahudi na makafiri wakoloni, na kuondoa taasisi ya Kiyahudi iliyopotoka kutoka katika uwepo, basi tusibakishe athari yake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu Mwenye Uweza, ﴿NA HAKIKA ALLAH ATAWASAIDIA WANAOMSAIDIA. HAKIKA ALLAH NI MWENYE NGUVU, MWENYE UWEZA﴾.
Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir