Habari kwa Vyombo vya Habari
Vijana wa Hizb ut-Tahrir huko Al Qadarif
Wawahamasisha Waislamu Kuinusuru Gaza
Vijana wa Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Sudan katika mji wa Al Qadarif, leo Jumatatu 2025/7/28, saa moja baada ya adhuhuri, karibu na Msikiti wa Kale katika soko la Al Qadarif, waliandaa msimamo wa kuwasaidia watu wa Gaza, walibeba mabango yaliyoandikwa:
- Shirika la Wayahudi ni kivuli cha tawala za Kiarabu, kitu kikiondoka, kivuli chake huondoka
- Khilafah pekee ndiyo itakayokomboa Palestina
- ﴿NA WAKIKUOMBENI MSAADA KATIKA DINI, BASI JUU YENU KUWASAIDIA﴾
- Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: «NA ANAYE AMKIA ASIWE NA HAMU YA MAMBO YA WAISLAMU, BASI YEYE SI KATIKA WAO»
- Enyi Waislamu: Je, mmeridhia watoto wa Gaza wanakufa polepole mbele ya macho ya baba zao na mama zao?
- Je, kuna uhalifu mkuu kuliko kubaki kwa majeshi katika kambi zao na ndege na maroketi katika maeneo yao, na maadui wa Mwenyezi Mungu "waliokasirikiwa" wanalichafua Msikiti wa Al-Aqsa?!
- Enyi Umma wa Kiislamu, Enyi Umma bora mliotolewa kwa watu, msemeni kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu katika imani yenu, msemeni kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwasaidia ndugu zenu.
- Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: «SI MUUMINI YULE ANAYE LALA AMESHIBA NA JIRANI YAKE ANA Njaa PEMBENI YAKE» Imepokewa na Al-Hakim.
Msimamo huo ulipata mapokezi makubwa kutoka kwa waliohudhuria wakiiombea Gaza ushindi, huku wakisifu msimamo wa Hizb ut-Tahrir. Vijana wengi wa Umma walishiriki katika kubeba mabango, jambo ambalo linathibitisha kiu ya Umma ya kuwasaidia ndugu zao huko Gaza.
Ibrahim Uthman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Jimbo la Sudan