Organization Logo

السودان - مكتب - ناطق

ولاية السودان

الخرطوم شرق- عمارة الوقف الطابق الأرضي -شارع 21 اكتوبر- غرب شارع المك نمر

Tel: 0912240143- 0912377707

spokman_sd@dbzmail.com

www.hizb-ut-tahrir.info

Tofauti Kubwa Kati ya Utukufu Chini ya Kivuli cha Uislamu na Udhilifu Chini ya Ukandamizaji wa Mifumo Teule
Press Release

Tofauti Kubwa Kati ya Utukufu Chini ya Kivuli cha Uislamu na Udhilifu Chini ya Ukandamizaji wa Mifumo Teule

June 27, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tofauti Kubwa Kati ya Utukufu Chini ya Kivuli cha Uislamu na Udhilifu Chini ya Ukandamizaji wa Mifumo Teule

Kamati Kuu ya Mitihani ya Shahada ya Sudan, ilisihi jumuiya ya kimataifa na mashirika husika kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu, na kuchangia katika kuwawezesha wanafunzi wote wa Sudan, kufanya mitihani, haswa maeneo yaliyoathiriwa na vita, na hali ngumu za kibinadamu. (SUNA, 2025/06/26 BK)

Kundi la watu wetu bado wana matumaini mema kwa Umoja wa Mataifa na mashirika yake, na wanatarajia msaada kutoka kwa wale wanaoitwa jumuiya ya kimataifa na mashirika ya kimataifa, licha ya historia yake ambayo inathibitisha kwamba haitoi kwa ajili ya Mungu, kwani sio mashirika ya hisani, lakini ina ajenda ambayo inafichuka kila wakati kuhusu uadui wake uliotangazwa kwa Uislamu na Waislamu.

Mnamo mwaka wa 2016 BK, UNESCO ilifanya mkutano wa kuzuia (misimamo mikali ya vurugu), na moja ya matokeo yake ilikuwa kwamba "suala la kubadilisha mitaala ya elimu katika Mashariki ya Kati na maeneo mengine ambayo yanashuhudia ustawi wa mawazo ya itikadi kali lazima lishughulikiwe".

Neno hili (mawazo ya itikadi kali) linatumiwa na linamaanisha Uislamu pekee, kwa sababu nchi za Magharibi zinazodhibiti ulimwengu leo ​​zinataka Uislamu wa kikuhani, usiohusika katika maisha, katika suala la mifumo ya utawala na siasa, mfumo wa kiuchumi, na mfumo wa kijamii, ili wasipate kikwazo katika kutekeleza mipango yao, lakini badala yake wanaendelea na matendo yao yote ya uhalifu dhidi ya Waislamu; kutoka mateso na mauaji ya halaiki, na kujitenga kwa Sudan Kusini, na vita inayoendelea sasa Sudan, ni matokeo tu ya kufuata ubepari wa Magharibi, na mashirika yake ya uhalifu.

Jukumu la mashirika haya yanayoitwa ya kibinadamu linazidi kile kilichotangazwa, hadi jaribio la kupotosha maoni ya umma, kwa kuchapisha habari za kupotosha juu ya ukweli wa hali katika maeneo wanayofanya kazi, ili kazi yao iendelee, pamoja na kutekeleza majukumu ya ujasusi yenye shaka kwa niaba ya nguvu za kimataifa, hadi idadi ya wachunguzi walipowafafanua kuwa ni zana za ukoloni mamboleo! Badala yake, ni moja ya zana hatari zaidi za mzozo wa kimataifa.

Na katika Sudan, mara ngapi mashirika haya ya kimataifa yamefichuliwa yakifanya kazi ya ujasusi, na upelelezi kwa maslahi ya nchi za Magharibi, na haishii tu kukusanya habari, lakini badala yake inaenea hadi kueneza sumu za mgawanyiko, na mizozo kati ya makundi ya watu, kama ilivyotokea Sudan Kusini, ambapo mashirika haya yalichangia kupitia upendeleo wao kwa upande mmoja wa mzozo, ili kuzidisha mizozo hii, wakitumia kinga walizopewa.

Utunzaji wa mambo unahitaji kushughulika na mashirika haya ya kimataifa kwa kutoaminiana, kwani matendo yao ambayo yamezua mashaka mengi, yana sifa ya utata mwingi kutokana na migongano ya maslahi ya nchi, na ukungu wa misimamo ya nchi zinazounga mkono.

Ukombozi wetu uko mikononi mwetu na sio mikononi mwa maadui zetu ambao wanatuandalia mazingira mabaya; iwe ni wale wanaotutangazia uadui wao, au wale wanaovaa unafiki kama vazi la marafiki, na vazi la "washirika" (wafadhili).

Kuhusisha masuala ya elimu; ambayo ni muhimu zaidi katika malezi na utengenezaji wa vizazi kupitia mashirika haya yenye shaka ni kujiua kisiasa, na maafa makubwa, ambayo madhara yake ya uharibifu kwa jamii yanaonekana mapema au baadaye.

Elimu inawakilisha nguzo muhimu katika uamsho wa Waislamu, na ili iwe hivyo, lazima kuwe na mfumo wa kisiasa unaotegemea itikadi ya Uislamu Mkuu, mfumo ambao unajumuisha maono ya kisiasa tofauti, ya hali ya juu, na huru kwa nchi yake, kuchukua wanadamu kutoka kwenye giza la ukafiri, upotovu na ujinga, hadi kwenye nuru ya Uislamu na uadilifu wake, ambayo huleta kwa wanadamu katika nyanja zote za maisha; kiroho, kiakili, kimaadili, kisiasa, kiuchumi, na zinginezo, na katika sayansi na teknolojia. Mfumo huu wa kisiasa bila shaka ni mfumo wa Khilafah Rashidah kwa misingi ya Utume, ambayo inatekeleza Uislamu na mifumo yake kikamilifu, ambayo iliongoza ulimwengu kwa karne kadhaa katika ubora wa taasisi zake za kitaaluma, ubunifu wake wa hali ya juu, na uvumbuzi, na pia mchango wake mkubwa katika maendeleo ya binadamu, hivyo tofauti kubwa kati ya heshima chini ya kivuli cha Uislamu, na udhalili chini ya kivuli cha mifumo tegemezi.

Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan

Official Statement

السودان - مكتب - ناطق

ولاية السودان

السودان - مكتب - ناطق

Media Contact

السودان - مكتب - ناطق

Phone: 0912240143- 0912377707

Email: spokman_sd@dbzmail.com

السودان - مكتب - ناطق

الخرطوم شرق- عمارة الوقف الطابق الأرضي -شارع 21 اكتوبر- غرب شارع المك نمر

Tel: 0912240143- 0912377707 | spokman_sd@dbzmail.com

www.hizb-ut-tahrir.info

Reference: PR-0197b149-f2d8-7239-a84b-3db271a0608e