
31/8/2025
Sudani News: Watu wa Al-Fashir Kati ya Nyundo ya Vita na Pasi ya Njaa, na Hakuna Wokovu kwao Ila Dola ya Khilafa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan
Mji wa Al-Fashir, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, unashuhudia janga halisi la kibinadamu, huku kukiwa na mapigano kati ya pande zinazopigana, ambapo makumi ya raia wameuawa katika siku chache zilizopita, wakati wakazi wanakabiliwa na mzingiro mkali, kwa zaidi ya mwaka mmoja, na njaa ya makusudi, huku kukiwa na ukimya wa kimataifa wa kutisha, huku Umoja wa Mataifa ukithibitisha kuuawa kwa watu wasiopungua 89 katika mapigano ya siku za hivi karibuni.
Kinachowapata watu wetu huko Al-Fashir; kutoka mauaji, ugaidi na njaa, ni jambo lisilokubalika katika sheria ya Kiislamu, na uhalifu usiosameheka, na ikiwa vikosi vya msaada wa haraka vinabeba dhambi yake, kwa kuwa wao ndio wanaozingira raia, na kuwashambulia kwa mizinga yao, na kuwanyima chakula na maji, basi jukumu la dola ni kubwa zaidi, kwa kuwa inawajibika kwa raia wake, kwa kauli yake ﷺ: «Na imamu aliye juu ya watu ni mchungaji na yeye ataulizwa juu ya kundi lake». Na pia inawajibika kutoa chakula, malazi na usalama, Amani na baraka zimshukie: «Miongoni mwenu akiamka akiwa salama katika nafsi yake, na mwenye afya katika mwili wake, na anacho chakula cha siku yake, ni kama vile amekusanyiwa dunia nzima», lakini yenyewe, yaani dola, imeitelekeza jukumu lake, na ikaanza kuomba Umoja wa Mataifa na mashirika yake, Waziri Mkuu Kamel Idris alisema kwamba aliliomba Baraza la Usalama litumie mamlaka yake ya kisheria, kukomesha mzingiro unaoendelea wa mji wa Al-Fashir, kwa zaidi ya siku 500, na anajua kuwa jukumu ni lake, kisha Umoja wa Mataifa huu ulikuwa umetoa, kupitia Baraza lake la Usalama, azimio namba 2736 mnamo Juni 13/2024 BK, na kwa uungaji mkono wa wanachama 14 na Urusi kujizuia kupiga kura, Baraza hili liliidhinisha azimio linalotaka vikosi vya msaada wa haraka kusitisha mzingiro wao wa Al-Fashir, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, na linatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano, kupunguzwa kwa mivutano huko Al-Fashir na maeneo yake ya jirani, na kuondolewa kwa wapiganaji wote wanaotishia usalama na usalama wa raia, na azimio hili halijatekelezwa licha ya kupita zaidi ya mwaka mmoja tangu litolewe! Jambo ambalo linathibitisha kwamba upande unaoendesha vita, hautaki mzingiro huu uishe isipokuwa kwa kuanguka kwa Al-Fashir, ili Darfur yote iwe mikononi mwa vikosi vya msaada wa haraka, na iwe tayari kujitenga, kama inavyotaka Amerika, ambayo inapanga kuigawa Sudan katika majimbo matano, na imeanza na Sudan Kusini.
Serikali inapaswa kulazimisha mara moja majeshi yake yote ili kuvunja mzingiro wa Al-Fashir, na ifuate kwa misafara ya chakula na dawa, kwani hili ndilo linalo wajibishwa kisheria na haki ya uangalizi, na ndilo pia linalo wajibishwa kushindwa njama ya Amerika ya kuitenga Darfur.
Enyi watu wetu nchini Sudan: Tiba ya msingi ya matatizo yetu yote katika kila sehemu ya nchi yetu, bali tiba ambayo inaondoa mizizi ya Magharibi kafiri kutoka nchi yetu, na inashindwa njama za Amerika na nchi za kikoloni, zinazotaka kuigawa Sudan, tiba ya hayo yote ni kanuni ya Uislamu, inatekelezwa na dola yake ya Khilafa kwa njia ya Utume.
Basi fanyeni kazi na Hizb ut-Tahrir ili kusimamisha Khilafa Rashidah ya pili kwa njia ya Utume; faradhi ya Mola wenu na chanzo cha utukufu wenu.
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye litakalo kufufueni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu huingilia baina ya mtu na moyo wake, na kwamba kwake Yeye mtakusanywa﴾
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Sudani News / Abu Wadaha News

