Organization Logo

بنغلادش مكتب

ولاية بنغلادش

Tel: 8801798367640

Fax: Skype: htmedia.bd

contact@ht-bangladesh.info

Uhamishaji wa Serikali ya Kihindu "Hindutva" Waislamu kwenda Bangladesh chini ya Tishio la Silaha ni Uadui wa Wazi kwa Waislamu kama Uadui wa Taasisi ya Kiyyahudi Inayokalia kwa Mabavu
Press Release

Uhamishaji wa Serikali ya Kihindu "Hindutva" Waislamu kwenda Bangladesh chini ya Tishio la Silaha ni Uadui wa Wazi kwa Waislamu kama Uadui wa Taasisi ya Kiyyahudi Inayokalia kwa Mabavu

July 04, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhamishaji wa Serikali ya Kihindu "Hindutva" Waislamu kwenda Bangladesh chini ya Tishio la Silaha

ni Uadui wa Wazi kwa Waislamu kama Uadui wa Taasisi ya Kiyyahudi Inayokalia kwa Mabavu

Serikali ya Kihindu ya Modi "Hindutva" inaendelea kuongeza kiwango cha ukandamizaji na mateso dhidi ya Waislamu wa India, kuanzia kubomoa nyumba zao, hadi kuwafukuza kwa nguvu na dhuluma kutoka nchi yao. Katika hilo, wanafuata nyayo za taasisi ya Kiyahudi inayokalia kwa mabavu huko Palestina. Hivi karibuni, utawala wa India umeanza kuwatendea Waislamu wa India kama wanyama, kwa kuwazungumzia kama "wahamiaji haramu", na kuwafukuza mamia yao kwenda Bangladesh chini ya tishio la silaha, bila kuzingatia taratibu zozote za kisheria "za kitaifa" au za kimataifa. Mwanamke anayeitwa Rahima Khatun alisema: "Walitutendea kama wanyama. Tuliwaambia sisi ni Wahindi, kwa nini tunaingia Bangladesh? Lakini walituelekezea bunduki na kututishia: (Msipochukua njia nyingine, tutawapiga risasi)". Aliongeza: "Baada ya kusikia milio minne ya risasi kutoka upande wa India, tulipatwa na hofu, tukavuka mpaka kwa miguu.

Baadhi walijaribu kuficha ukweli kwa kudai kwamba suala hilo linatokana na mivutano ya kisiasa ya sasa kati ya India na Bangladesh. Lakini ukweli ni kwamba kinachotokea ni sehemu ya kampeni endelevu inayolenga kuwanyima Waislamu wa India uraia wao, na kufuta utambulisho wao wa Kiislamu, kama vile taasisi ya Kiyahudi inavyofanya huko Palestina.

Na nchini India, ambako Waislamu zaidi ya milioni 200 wanaishi, tumeona mfululizo wa hatua zinazolenga kuondoa utambulisho wa Kiislamu, kuanzia kubomoa Msikiti wa kihistoria wa Babri na kujenga hekalu mahali pake, hadi kufuta urithi wa utawala wa Kiislamu wa miaka elfu moja, na kubomoa kaburi la Aurangzeb, na kupitisha sheria ya uraia, sheria ya usajili wa wakazi, na hatimaye kupitisha sheria ya marekebisho ya Waqf. Hiyo yote inaonyesha jitihada za serikali ya Kihindu kuwanyima Waislamu utambulisho wao, na kuwageuza kuwa raia wasio na uraia. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: ﴿Utawakuta walio wakali zaidi katika uadui kwa walio amini kuwa ni Mayahudi na wale walio shiriki﴾.

Swali linaloulizwa ni: Kwa nini serikali ya Kihindu inathubutu kufikia hatua hii? Na jibu ni:

Kwanza: Ingawa Waislamu katika eneo hili wameungana katika dini na damu, lakini ukoloni kafiri wa Uingereza uliwagawanya na kuwadhoofisha kwa misingi ya utaifa (Mhindi, Mbangali, Mpakistani...), na ukawawekea watawala vibaraka wa kilimwengu ambao hawawalindi Waislamu, wala hawajali hatima yao. Kwa sababu hii, mshauri wa usalama wa serikali ya mpito ya Kibangali alisema: "Ikiwa itathibitika kuwa wao ni raia wa Bangladesh, tutawakubali", na kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha kilimwengu nchini alisema: "Sio Delhi wala Rawalpindi, wala nchi nyingine yoyote, Bangladesh kwanza"! Ama wanasiasa na wasomi wa kilimwengu, wao ni wanafiki na wachukia Waislamu, kwani wananguruma kama simba dhidi ya dhuluma za Wahindu nchini Bangladesh, na wamenyamaza kama paka waoga mbele ya ukandamizaji wa Waislamu nchini India. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Si katika sisi anayelingania ubaguzi, wala si katika sisi anayepigana kwa ajili ya ubaguzi, wala si katika sisi anayefia ubaguzi» Imesimuliwa na Abu Daud.

Pili: Hakika India ni chombo cha Marekani kafiri mkoloni katika eneo hilo, na mwanachama wa muungano wa kijeshi wa "Quad" katika eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki. Kama vile Marekani inavyotumia taasisi ya Kiyahudi katika Mashariki ya Kati kukandamiza Umma wa Kiislamu, inatumia serikali ya Kihindu katika Asia ya Kusini kwa kusudi hilo hilo.

Enyi Waislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: ﴿Na wakiomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia﴾ Ikiwa Waislamu wanashambuliwa mahali popote, basi kuwasaidia ni lazima kwa Waislamu wote. Na mmeona jinsi gani watawala wa Kiislamu wa kitaifa na wa kilimwengu hawatumi majeshi kuwasaidia watu wa Palestina au Kashmir au Arakan, huku wakiwatuma chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa na kwa amri ya Marekani kuwaua Waislamu na kumwaga damu yao!

Watawala hawa si walinzi wa Umma, bali ni wasaliti wanaopanga njama dhidi yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Hakika Imamu ni ngao anayepiganwa nyuma yake na anayeogopwa» Sahih Muslim. Na kinachowapata Waislamu kila mahali kutokana na dhuluma ni matokeo ya kukosekana kwa mtawala wa kweli wa Umma; Khalifa. Kwa hivyo, hakuna njia mbele yetu ila kuungana ili kusimamisha dola ya Khilafah Rashidah, badala ya kutegemea watawala hawa vibaraka. Wito wetu lazima uwe kwa wana waaminifu wa Umma katika majeshi, ili wampe Nusra Hizb ut-Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Kumbukeni kwamba huu ni wajibu wenu kama Waislamu.

﴿Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, kwa yakini atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale walio kuwa kabla yao, na kwa yakini atawathibitishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia baada ya khofu yao amani. Waniabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotofu

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

Katika Wilaya ya Bangladesh

Official Statement

بنغلادش مكتب

ولاية بنغلادش

بنغلادش مكتب

Media Contact

بنغلادش مكتب

Phone: 8801798367640

Fax: Skype: htmedia.bd

Email: contact@ht-bangladesh.info

بنغلادش مكتب

Tel: 8801798367640 | contact@ht-bangladesh.info

Fax: Skype: htmedia.bd

Reference: PR-0197c661-60c0-760f-9ec3-319944ac83a5