Organization Logo

بنغلادش مكتب

ولاية بنغلادش

Tel: 8801798367640

Fax: Skype: htmedia.bd

contact@ht-bangladesh.info

Uhamishaji wa Serikali ya Kihindu "Hindutva" Waislamu kwenda Bangladesh chini ya tishio la Silaha ni uadui wa wazi kwa Waislamu kama vile uadui wa Taasisi haramu ya Kiyahudi
Press Release

Uhamishaji wa Serikali ya Kihindu "Hindutva" Waislamu kwenda Bangladesh chini ya tishio la Silaha ni uadui wa wazi kwa Waislamu kama vile uadui wa Taasisi haramu ya Kiyahudi

July 04, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhamishaji wa Serikali ya Kihindu "Hindutva" Waislamu kwenda Bangladesh chini ya tishio la Silaha

ni uadui wa wazi kwa Waislamu kama vile uadui wa Taasisi haramu ya Kiyahudi

Serikali ya Kihindu ya Modi "Hindutva" inaendelea kuongeza kiwango cha ukandamizaji na mateso dhidi ya Waislamu Wahindi, kuanzia na kubomoa nyumba zao, hadi kuwafukuza kwa nguvu na dhuluma kutoka nchini mwao. Katika hilo, inafuata nyayo za taasisi haramu ya Kiyahudi huko Palestina. Hivi karibuni, utawala wa India umeanza kuwatendea Waislamu Wahindi kama wanyama, kwa kuwaita "wahamiaji haramu", na kuwafukuza mamia yao kwenda Bangladesh chini ya tishio la silaha, bila kujali hatua zozote za kisheria "za kitaifa" au za kimataifa. Mwanamke anayeitwa Rahima Khatun alisema: "Wametutendea kama wanyama. Tuliwaambia sisi ni Wahindi, kwa nini tunaingia Bangladesh? Lakini walituelekezea bunduki na kututishia: (Msipofuata njia nyingine, tutawapiga risasi)". Aliongeza: "Baada ya kusikia milio minne ya risasi kutoka upande wa India, tuliogopa, tukavuka mpaka kwa miguu.

Wengine walijaribu kuficha ukweli kwa kudai kwamba jambo hilo linatokana na mivutano ya sasa ya kisiasa kati ya India na Bangladesh. Lakini ukweli ni kwamba kinachotokea ni sehemu ya kampeni endelevu inayolenga kuwanyima Waislamu Wahindi uraia wao, na kufuta utambulisho wao wa Kiislamu, kama vile taasisi ya Kiyahudi inavyofanya huko Palestina.

Nchini India, ambako Waislamu zaidi ya milioni 200 wanaishi, tumeona mfululizo wa hatua zinazolenga kuangamiza utambulisho wa Kiislamu, kuanzia na kubomoa msikiti wa kihistoria wa Babri na kujenga hekalu mahali pake, hadi kufuta urithi wa utawala wa Kiislamu uliodumu kwa miaka elfu moja, kubomoa kaburi la Aurangzeb, na kupitisha sheria ya uraia, sheria ya usajili wa watu, na hatimaye kupitisha sheria ya marekebisho ya Wakfu. Yote hayo yanaonyesha jitihada za serikali ya Kihindu za kuwanyima Waislamu utambulisho wao, na kuwageuza kuwa raia wasio na utaifa. Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Hakika utawakuta walio maadui zaidi kwa walio amini ni Mayahudi na wale walio shiriki﴾.

Swali linaloulizwa ni: Kwa nini serikali ya Kihindu inathubutu kiasi hiki? Na jibu ni:

Kwanza: Ingawa Waislamu katika eneo hili wameungana katika dini na damu, ukoloni kafiri wa Uingereza uliwagawanya na kuwadhoofisha kwa misingi ya utaifa (Mhindi, Mbengali, Mpakistani...), na kuwateua watawala vibaraka wa kidunia ambao hawawalindi Waislamu, wala hawajali hatima yao. Kwa sababu hii, mshauri wa usalama wa serikali ya mpito ya Kibengali alisema: "Ikiwa itathibitika kuwa wao ni raia wa Bangladesh, tutawakubali", na kiongozi wa chama kikubwa cha kidunia nchini alisema: "Sio Delhi wala Rawalpindi, wala nchi nyingine yoyote, Bangladesh kwanza"! Ama wanasiasa na wasomi wa kidunia, wao ni wanafiki na wachukia Waislamu, kwani wananguruma kama simba dhidi ya dhuluma za Wahindu nchini Bangladesh, na wananuna kama paka waoga mbele ya ukandamizaji wa Waislamu nchini India. Mtume ﷺ amesema: «Si katika sisi anayeita ubaguzi, wala si katika sisi anayepigana kwa ubaguzi, wala si katika sisi anayefia ubaguzi» Imepokewa na Abu Daud.

Pili: India ni chombo cha Marekani kafiri ya kikoloni katika eneo hili, na mwanachama wa muungano wa kijeshi wa "Quad" katika eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki. Kama vile Marekani inavyotumia taasisi ya Kiyahudi katika Mashariki ya Kati kuukandamiza Umma wa Kiislamu, ndivyo inavyotumia serikali ya Kihindu katika Asia ya Kusini kwa madhumuni hayo hayo.

Enyi Waislamu, Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Na wakiomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia﴾ Ikiwa Waislamu wanashambuliwa popote, basi kuwasaidia ni wajibu kwa Waislamu wote. Mmeona jinsi gani watawala wa kitaifa na wa kidunia wa Waislamu hawatumi majeshi kusaidia watu wa Palestina au Kashmir au Arakan, huku wakiyatuma chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa na kwa amri ya Marekani kuwaua Waislamu na kumwaga damu yao!

Watawala hawa si walinzi wa Umma, bali ni wasaliti wanaoufanyia njama. Mtume ﷺ amesema: «Hakika Imamu ni ngao, anapiganiwa nyuma yake na anahofiwa» Sahihi Muslim. Kinachowatokea Waislamu kila mahali kutokana na dhuluma ni matokeo ya kukosekana kwa mtawala wa kweli wa Umma; Khalifa. Kwa hivyo, hakuna njia nyingine mbele yetu ila kuungana ili kusimamisha dola ya Khilafah Rashidah, badala ya kutegemea watawala hawa vibaraka. Wito wetu lazima uelekezwe kwa wana waaminifu wa Umma katika majeshi, kutoa Nusra kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Kumbukeni kwamba huu ni wajibu wenu kama Waislamu.

﴿Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale walio kuwa kabla yao, na atawathibitishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Waniabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotofu

Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilaya ya Bangladesh

Official Statement

بنغلادش مكتب

ولاية بنغلادش

بنغلادش مكتب

Media Contact

بنغلادش مكتب

Phone: 8801798367640

Fax: Skype: htmedia.bd

Email: contact@ht-bangladesh.info

بنغلادش مكتب

Tel: 8801798367640 | contact@ht-bangladesh.info

Fax: Skype: htmedia.bd

Reference: PR-0197c662-dba8-7856-b6ad-819d32f8fbfc