Organization Logo

القسم النسائي في المكتب الإعلامي المركزي

المركزي

Tel: 0096171724043

Fax: 009611307594

ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

http://www.hizb-ut-tahrir.info/

Turkestan ya Mashariki: Giza la Kuangamiza Taifa Zima
Press Release

Turkestan ya Mashariki: Giza la Kuangamiza Taifa Zima

September 22, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Turkestan ya Mashariki: Giza la Kuangamiza Taifa Zima

Katika Turkestan ya Mashariki, mama wanatiwa mbaroni na watoto wanatenganishwa na familia zao na wasichana wadogo wanatunguliwa... Katika Turkestan ya Mashariki, taifa linachinjwa na kuangamizwa kimyakimya (Shirika la Habari la Turkestan ya Mashariki, 2025/09/12).

Haijafichika kwa mtu yeyote juhudi za serikali ya Kichina yenye uhalifu katika Turkestan ya Mashariki za kulifuta utambulisho wa watu wake Waislamu, kwa hivyo inawakandamiza wanawake, inawaonea na kuwazuia kuvaa nguo zao na kufanya sala zao, na inawatenganisha watoto na wazazi wao ili kuosha akili zao na kuwalisha utamaduni wake wa kikafiri na kuwatoa katika Uislamu, pamoja na kuwatungua wasichana wadogo ili kupunguza kuzaa kwao kizazi kipya kinachoamini Uislamu.

Kile ambacho Uchina inakifanya katika Turkestan ya Mashariki ni vita isiyo na hatari ndogo kuliko vita ya Wayahudi huko Gaza; vita vya kuangamiza vinafunua chuki kubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu, vita vinavyoongozwa na maadui wa Uislamu kila mahali.

Vita vya Uchina katika Turkestan ya Mashariki ni vita ya kimya ambayo inatafuta kuangamiza taifa, kufuta utambulisho wake, kuwatoa kutoka mizizi yao, na kuwatoa kutoka katika dini yao ili iwayeyushe katika utamaduni wake wa kikomunisti. Ama vita vya utawala wa Kiyahudi vinatangazwa kwa silaha na njaa vinavyofanywa na utawala huu ghasibu na washirika wake ili kukata kizazi cha watu wa Gaza na kukalia ardhi yao na kutimiza ndoto yao kuu wanayoipanga.

Hizi vita zinazoongozwa na madhalimu si chochote ila ni vita vya kuangamiza ambavyo lengo lake ni kuondoa kila kitu kinachohusiana na Uislamu na Waislamu na kushinda ustaarabu wa madhalimu makafiri wahalifu. Wanaunga mkono wengine na wanahalalisha heshima na damu, wanavunja utakatifu na kunyakua ardhi.

Na mbele ya dhulma na ukandamizaji huu wote, tunawapata watu wa Gaza wamesimama imara wakitoa ulimwenguni masomo katika kujitolea na kujitoa mhanga katika kulinda ardhi yao, na tunawapata Waislamu wa Uighur hawaanguki wakiwa wametukuka kama mizizi ya ardhi ambayo joka halikuweza kuing'oa.

Licha ya dhulma na ukandamizaji wanaokumbana nao watu wa Turkestan na ukiukwaji unaofichua uhalifu wa kinyama na vita vya kuangamiza, wanapinga kimyakimya ukandamizaji wa mamlaka za Kichina na kuwalazimisha kukana dini yao kwa vitisho.

Uchina imeanzisha kambi kadhaa ili kumtia mbaroni kila Muislamu na kumtesa na kumlazimisha kuachana na dini yake na kuasi. Kambi ambazo akili zao huoshwa na kujazwa na ustaarabu wake wa kikomunisti wa kikafiri, wakilenga kuficha mazoea yake haya ya ukandamizaji na sera zake za kikatili ambazo anatafuta kuangamiza taifa zima kupitia hizo. Licha ya hayo, harufu ya matendo yake hayo maovu ilianza kuvuma; Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilithibitisha tena katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu hali ya haki za binadamu kwa mwaka 2024, iliyotolewa Agosti 12, kwamba Uchina inaendelea kufanya uhalifu wa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Turkestan ya Mashariki. Na ili kuficha uchafu wa sera zake na uhalifu wake, Uchina inaandaa mabaraza ambayo inataka kukanusha yale yanayoenezwa kuyahusu kama vile jukwaa la "Maendeleo ya Haki za Binadamu huko Xinjiang", na mada zote zilizojadiliwa zilikuwa jaribio la kuhalalisha uhalifu wake dhidi ya haki za binadamu huko Turkestan ya Mashariki, na kupamba sura yake mbaya mbele ya ulimwengu kupitia shughuli za uwongo zinazolenga kuficha hali ya ukandamizaji, kuficha ukweli, na kuosha ukiukwaji unaofanywa dhidi ya Waislamu wa Uighur.

Pia, kwa miaka mingi, Uchina inaendelea kuandaa maonyesho ya urithi wa kitamaduni usioshikika kama sehemu ya sera yake ya kupamba ukaliaji wake wa Turkestan ya Mashariki na kuimarisha sera ya uanzishwaji wa kitaifa ambayo inawakilisha moja ya nguzo za uhalifu wa mauaji ya kikabila. Propaganda za Kichina kupitia maonyesho haya zinatafuta kukuza wazo kwamba urithi wa watu asilia huko Turkestan ya Mashariki, kama vile Uighur, Kazakh na Kyrgyz, ni sehemu ya utamaduni wa Kichina au uliundwa chini ya ushawishi wake.

Enyi umma wa Kiislamu: Mko wapi kutokana na kile kinachowatokea watoto wenu huko Turkestan ya Mashariki?! Kwa nini unyonge huu na ukimya huu?! Watoto wenu wanapinga licha ya kile wanachokipata kutokana na ukatili na ukandamizaji, wanapigana kwa imani thabiti, wakiwa watukufu licha ya udhalilishaji wa mamlaka za Kichina kwao. Kwa hivyo mnasubiri nini kuwasaidia?!

Hawa makafiri madhalimu wanapigana na Uislamu uliomo ndani ya Uighur, wanataka kuuangamiza na kuutoa kutoka ndani ya vifua vyao, lakini wao wamesimama imara na wanawaomba ndugu zao katika dini msaada, kwa hivyo nyinyi Waislamu mnafanya nini?

Enyi Maulamaa wa Kiislamu: Ndugu zenu huko Turkestan wanauawa ili Uislamu usichukuliwe kutoka kwao, kwani wao ndio wanazuoni ambao wanaeneza hukumu zake na kuzieleza. Lakini Uchina inatafuta kuwanyamazisha, kwa hivyo mko wapi katika kueneza ujumbe wenu? Je, mmezungumzia vita hivi ambavyo Uchina inavianzisha kimyakimya dhidi ya Waislamu huko na kuifichua kwenye majukwaa na kuwafahamisha watu wote kuhusu hayo? Je, mmeziita jeshi za Waislamu na kuwahimiza kuharakisha kumaliza mauaji haya na utakaso huu wa kikabila?

Uchina imedai kuwa inapambana na ugaidi na mkutano wa "amani" uliandaliwa chini ya kichwa "Kupambana na Ugaidi na Kuhifadhi Usalama wa Ulimwengu katika Hali Mpya: Majukumu ya Kikanda na Kimataifa", na ilitoataka mfumo wa kimataifa kushirikiana katika kupambana na ugaidi na kuweka usalama wa ulimwengu, na imekuwa wazi inamaanisha nini kwa "ugaidi", ni Uislamu na kila kitu kinachoashiria kuwa ustaarabu wa kale mkuu unaofanya kazi ya kurejesha nafasi yake na kurudi katika maisha ili kuwaongoza watu kwenye njia ya ukombozi na wokovu na kufuta kila athari ya ustaarabu huu wa Magharibi uliooza na mbaya.

Enyi Waislamu: Sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir tunashuhudia kwa Mwenyezi Mungu kwamba tumewaita watu wa nguvu na kinga na tumezindua vilio vya misaada mmoja baada ya mwingine, tukiwasihi maulamaa na jeshi na kila mtu anaye na maamuzi ya kisiasa; kumaliza mauaji haya, na tumethibitisha kwamba hili halitakuwa isipokuwa katika dola inayokusanya Waislamu waliotawanyika na kuwaondolea mikono ya makafiri wahalifu.

Enyi Waislamu: Maadui wanatuona kama taifa moja na wanashughulika nasi katika nchi zote za Kiislamu kama maadui zao, wanawadharau watoto wetu na kuwaua na wanatafuta kutuangamiza sote, kwa hivyo mtafanya haraka lini na damu itachemka lini katika mishipa yenu na mtaamini kwamba ni vita ya uwepo? Mtaelewa lini kwamba vita ni vita kati ya ustaarabu mbili: ustaarabu wetu wa Kiislamu au ustaarabu wao wa Magharibi?

Mtafahamu lini kwamba hawa hawatatosheka na kuwaangamiza watu wa Turkestan wala watu wa Gaza wala Afrika ya Kati wala Waislamu wengine kila mahali? Suala ni kubwa zaidi kuliko hilo; Ni vita kati ya ustaarabu kutoka kwa mwenye elimu mwenye hekima na ustaarabu kutoka kwa uvumbuzi wa akili ya mwanadamu tasa aliye thubutu kumkosea Muumba wake na akaweka hukumu na sheria, na ni tofauti kubwa kati ya ustaarabu uliowekwa na Muumba wa ulimwengu mwenye hekima mjuzi na ustaarabu uliowekwa na mja kafiri duni!

Kitengo cha Wanawake

Katika Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir

Official Statement

القسم النسائي في المكتب الإعلامي المركزي

المركزي

القسم النسائي في المكتب الإعلامي المركزي

Media Contact

القسم النسائي في المكتب الإعلامي المركزي

Phone: 0096171724043

Fax: 009611307594

Email: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

القسم النسائي في المكتب الإعلامي المركزي

Tel: 0096171724043 | ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Fax: 009611307594

http://www.hizb-ut-tahrir.info/

Reference: PR-019961b9-d628-790f-8733-841c827f9f34