Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuongezeka kwa Ukandamizaji wa Marekani Dhidi ya Mashirika ya Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Katika mahojiano ya hivi majuzi na mtangazaji wa redio Sid Rosenberg, Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio alieleza kuhusu mchakato unaoendelea wa kuyaorodhesha makundi ya Muslim Brotherhood na Baraza la Uhusiano wa Kiislamu la Marekani (CAIR) kama mashirika ya kigaidi. Waziri Rubio alisema kuwa uainishaji huu "unaendelea, na ni wazi kuwa kuna matawi tofauti ya Muslim Brotherhood, kwa hivyo kila moja itabidi iainishwe."
Ingawa Rubio alikiri kwamba uainishaji kama huo unahitaji hatua za kisheria ili kuhimili changamoto za kimahakama, maoni yake yanaakisi mwelekeo unaokua wa kuyaonyesha baadhi ya makundi ya Kiislamu - ya kigeni na ya ndani - kama vitisho kwa usalama wa taifa na wapinzani wa sera za kigeni za Marekani. Hii inaakisi matamshi ya awali ya msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, ambaye alisema kwamba Mahmoud Khalil alilengwa kwa sababu alikuwa "adui wa sera za kigeni na maslahi ya usalama wa taifa la Marekani."
Kwa miongo mingi, Waislamu nchini Marekani wamekuwa wakikabiliwa na ujasusi, ubaguzi, uhalifu na vitisho chini ya kivuli cha kupambana na ugaidi na usalama wa taifa. Hotuba za chuki dhidi ya Uislamu kutoka tawala zilizopita, za Kidemokrasia na za Republican, zimepelekea kuongezeka kwa uhalifu wa chuki dhidi ya jumuiya ya Waislamu.
Haiishii tu kwa Muslim Brotherhood au Baraza la Uhusiano wa Kiislamu la Marekani (CAIR), lakini inaathiri mashirika yote ya Kiislamu na jumuiya zetu kwa wakati mmoja. Kulenga mashirika ya Kiislamu kwa sababu za kisiasa - hasa yale yanayotetea masuala ya Waislamu au hukumu za Kiislamu - hakuwezi kuonekana nje ya muundo mpana wa uadui dhidi ya Uislamu.
Nabii ﷺ na Masahaba Radhi za Allah ziwe juu yao walikabiliwa na marufuku ya kisiasa, kufukuzwa na kampeni kama hizo za kumchafua mtu huko Makka, sio kwa sababu ya vurugu, lakini kwa sababu ya kutoa wito kwa Uislamu.
Uislamu unatuhimiza kutetea dini yetu, kusema ukweli, na kuandaa kwa pamoja kwa ajili ya manufaa ya Umma. Sisi Waislamu nchini Marekani lazima tusimame pamoja kwa uthabiti katika ukweli, tuunganishe sauti zetu, tutetee, na tukatae vitisho vilivyoundwa ili kutunyamazisha na kuondoa dini yetu.
Mwenyezi Mungu anatukumbusha kwa kusema: ﴿Hakika Waumini ni ndugu﴾, na kwa kauli yake: ﴿Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao, wanaamrisha mema na wanakataza maovu, wanashika Sala, wanatoa Zaka, na wanamtii Allah na Mtume wake. Hao ndio atawarehemu Allah. Hakika Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima﴾.
Sisi katika Hizb ut Tahrir tunahimiza mashirika yote ya Kiislamu kulinda. Jambo hili halihusu shirika moja, bali kulinda utambulisho wetu wa Kiislamu nchini Marekani.
Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika