Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ukumbusho kwa Waislamu Kuhusu Utukufu wa Muislamu: Damu Yake, Mali Yake na Heshima Yake
Vyombo vya habari vimeripoti habari za uhalifu wa kutisha uliofanyika katika mji wa Al-Fashir nchini Sudan, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na uhamishaji ambao umesababisha maelfu ya familia kuyahama makazi yao.
Swali linalojitokeza ni: Inawezekanaje kwa Muislamu anayeshuhudia kwamba hapana mungu ila Allah na kwamba Muhammad ni mjumbe wa Allah na anaamini siku ya Akhera; inawezekanaje kwake kudharau damu ya ndugu yake Muislamu, mali yake na heshima yake?! Inawezekanaje kwake kumtisha, wakati Mtume ﷺ anasema: «HAIRUHUSIWI KWA MUISLAMU KUMTISHA MUISLAMU»?!
Jambo kama hili limetokea hapo awali katika nchi kadhaa za Kiislamu kama vile Syria, Misri, Yemen, Libya, Iraq na zinginezo, je, Waislamu wamesahau utukufu wa damu yao wenyewe?
Hakika, ni jambo linalojulikana kwa dini kwa lazima kuwa ni haramu kumuua Muislamu kwa makusudi kwa mujibu wa maandiko ya wazi ya Qur'an, Allah Mtukufu anasema: ﴿NA YEYE AMUUA MUMIN KWA MAKUSUDI, BASI MALIPO YAKE NI JAHANNAM, ATADUMU HUMO, NA ALLAH AMEMKASIRIKIA, NA AMEMLAANI, NA AMEMWEKELEA ADHABU KUBWA﴾ Je, kuna adhabu kali zaidi ya hii kwa muuaji wa kukusudia? Na Mtume ﷺ anasema: «KILA KITU CHA MUISLAMU NI HARAMU KWA MUISLAMU MWENZAKE; DAMU YAKE, MALI YAKE NA HESHIMA YAKE», Na miongoni mwa mambo ya mwisho ambayo Mtume ﷺ aliusia katika hotuba ya kuaga ilikuwa ni kuharamisha Muislamu damu yake, mali yake na heshima yake kwa Muislamu, na maandiko ya kisheria yameenea kuhusu ulazima wa kuhifadhi heshima za Muislamu, na sheria imeimarisha vikali haki ya yule anayevunja chochote katika heshima hizi.
Nini tatizo lenu enyi Waislamu? Je, inawezekana Muislamu akavunja heshima za ndugu zake Waislamu kwa sababu tu anamiliki silaha? Je, ni kwa urahisi kiasi hiki ambacho makafiri wakoloni wanaweza kuwatawala baadhi ya Waislamu, kuwapa nguvu na silaha, na kuwafanya wavunje heshima za ndugu zao Waislamu? Vipi askari polisi au askari katika majeshi ya Waislamu anainua silaha dhidi ya raia wasio na hatia? Je, anadhani itamnufaisha mbele ya Allah Mtukufu kusema kwamba yeye ni mtumwa anayeamrishwa?
Enyi Waislamu:
Lazima mtambue hatari ya jambo hili na ukubwa wake mbele ya Allah Mtukufu, kwa kuwa muuaji wa Muislamu anastahili ghadhabu ya Allah na anastahili laana Yake na kufukuzwa kutoka kwa rehema Zake na anastahili kudumu milele katika Jahannamu, kama alivyosema Mtume ﷺ: «MTU HUENDELEA KUWA KATIKA UPANUZI WA DINI YAKE MAADAMU HAKUPATA DAMU ILIYO HARAMU», Hivyo, haijalishi amefanya madhambi gani yasiyo ya kuua kwa makusudi, yuko katika upanuzi wa dini yake, lakini kwa kuua kwa makusudi, anapoteza upanuzi huu, na ananyimwa mafanikio, na anakumbwa na ghadhabu ya Allah Mtukufu, na hakuna udhuru wowote utakaomnufaisha, hata kama ndugu yake Muislamu alimkabili kwa silaha, Mtume ﷺ anasema: «WAISLAMU WAWILI WANAPOKUTANA NA MAPANGA YAO, MUUAJI NA ALIYEUAWA WATAKUWA MOTONI. ILISEMWA: HUYU NI MUUAJI, LAKINI VIPI ALIYEUAWA? ALISEMA: ALIKUWA NA HAMU YA KUMUUA MWENZAKE». Na lau muulizaji angeuliza nini cha kufanya katika hali hii, basi Mtume ﷺ anajibu swali hili, wakati fitina zinapotokea, Abu Musa Al-Ash'ari amesimulia kwamba Mtume ﷺ alisema: «HAKIKA MBELE YA SAA KUNA FITINA KAMA VIPANDE VYA USIKU MWEUSI, AMBAZO MTU ATAAMKA ASUBUHI NAYE NI MUUMIN NA ATAINGIA JIONI NAYE NI KAFIRI, NA ATAINGIA JIONI NAYE NI MUUMIN NA ATAAMKA ASUBUHI NAYE NI KAFIRI, ANAYEKAA HUMO NI BORA KULIKO ALIYEYASIMAMIA, NA ANAYETEMBEA HUMO NI BORA KULIKO ANAYEKIMBIA, BASI VUNJENI MIENDE YENU, NA KATENI KORDU ZENU, NA PIGENI MAPANGA YENU KWENYE MAWE, NA AKIINGIWA - YAANI MMOJA WENU - BASI AWE KAMA MWANA BORA WA ADAMA».
Kwa kila Muislamu, kwa kila ofisa, askari na polisi, kwa kila anayemiliki silaha:
Hakika Allah Mtukufu ametupa akili ili tufikiri kwayo, na ametuwajibisha kuitumia kwa matumizi sahihi, hivyo mtu asitende wala kufanya jambo lolote wala kutamka neno lolote kabla ya kujua hukumu yake ya kisheria, na kujua hukumu ya kisheria kunahitaji kuelewa uhalisia unaokusudiwa kuwekewa hukumu ya kisheria, hivyo ni lazima Muislamu awe na ufahamu wa kisiasa, ili atambue mambo kwa uhakika wake, na asifuate mipango ya makafiri wakoloni ambao hawatutakii sisi wala Uislamu kheri, na wanafanya juhudi kwa kila wawezalo kwa nguvu, hila na ujanja kutugawanya vipande vipande na kutawala nchi zetu na kunyakua uwezo wetu na utajiri wetu, hivyo vipi Muislamu anakubali kuwa chombo mikononi mwa makafiri wakoloni hao, au mtekelezaji wa amri za vibaraka wao?! Je, anatamani kitu kidogo cha anasa za dunia zinazopita ili apoteze Akhera yake na awe miongoni mwa watu wa Motoni watakaodumu humo milele, waliolaaniwa na kufukuzwa kutoka kwa rehema za Allah? Je, Muislamu anakubali kumridhisha mtu yeyote kati ya wanadamu viumbe dhaifu huku akimkasirisha Allah Mtukufu ambaye mikononi mwake kuna dunia na Akhera?! Someni kauli ya Allah Mtukufu na mchukue msimamo wenu: ﴿NA KWA YAKINI TUMEKWISHA WAUMBA WENGI KATIKA MAJINI NA WATU WA KWENDA MOTONI. WANA NYOYO AMBAZO HAWAFAHAMU KWAZO, NA WANA MACHO AMBAYO HAWATAZAMI KWAZO, NA WANA MASIKIO AMBAYO HAWASIKII KWAZO. HAO NI KAMA WA NYAMA, BALI WAPOTOFU ZAIDI. HAO NDIO WENYE KUGHAFILIKA﴾ Je, mnaridhika kuwa kama wanyama, bali mme potea zaidi kuliko wao; hivyo hamnufaiki na macho yenu wala masikio yenu wala akili zenu, na mkuwe miongoni mwa watu wa Motoni?!
Enyi Waislamu:
Hakika Hizb ut Tahrir inamuonya kila Muislamu asimpate Muislamu mwenzake na chochote: katika damu yake au mali yake au heshima yake, na inawahadharisha na ghadhabu ya Allah Mtukufu na adhabu Yake kali, wallahi jambo hili ni la kweli na si la mzaha, hivyo msiwe miongoni mwa walioghafilika ambao hawaamki isipokuwa wakati wa kifo, wala si wakati wa majuto, na wakati ambapo imani yake haimnufaishi mtu ikiwa hakuamini hapo awali au hakupata kheri katika imani yake, wala anasa chache za dunia zisikuongopeni, kwani zinaondoka bila shaka, na hakika kifo kiko karibu na mmoja wenu kuliko kamba ya kiatu chake, hivyo asiruhusu mtu yeyote kumdhuru ndugu yake kwa chochote bila haki. Na hakika Hizb ut Tahrir inawaalika kuinua kiwango cha uelewa wa kisiasa, na kuzingatia hukumu za Allah Mtukufu, na kufanya kazi pamoja nayo ili kuhukumu kwa yale ambayo Allah ameyateremsha, ili iondolee mikono ya makafiri wakoloni na vibaraka wao juu yenu, na ifeli mipango yao katika nchi zetu.
﴿ENYI MLIO AMINI! MUITIKIENI ALLAH NA MTUME ANAPOKUITENI KWA LILE LINALOKUHUI SHENI. NA MJUE KWAMBA ALLAH HINGILIA BAINA YA MTU NA MOYO WAKE, NA KWAMBA KWAKE YEYE NDIO MTAKUSANYWA. NA ILINDENI FITNA ISIWAFIKIE PEKEE WALE WALIO DHULUMU MIONGONI MWENU. NA MJUE KWAMBA ALLAH NI MKALI WA KUADHIBU﴾
Ofisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir