Habari kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Sudan - Mji wa Kosti, Nile Nyeupe
Wakutana na Dkt. Muhammad Al-Haitham, Katibu Mkuu wa Chama cha National Unionist katika Jimbo la Nile Nyeupe
Siku ya Ijumaa, 2025/9/12, ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/Jimbo la Sudan ulifanya ziara kwa Dkt. Muhammad Al-Haitham, Katibu Mkuu wa Chama cha National Unionist, katika jengo la Azraq Taiba huko Kosti.
Ujumbe huo ulikuwa chini ya uongozi wa Dkt. Ahmed Fadl Al-Sayed, mwanachama wa Hizb ut-Tahrir, akifuatana na Profesa Abdul Majeed Othman (Abu Hajar) na Profesa Muhammad Babiker, wanachama wa Hizb ut-Tahrir.
Baada ya utambulisho, kiongozi wa ujumbe alieleza kuwa ziara hii inakuja kama sehemu ya kampeni iliyoanzishwa na Hizb ut-Tahrir/Jimbo la Sudan, kuzuia kujitenga kwa Darfur, akieleza hatari ya mpango huo kwa umoja wa nchi, kwa kuzingatia kwamba suala la umoja wa nchi na umoja wa umma ni suala la hatima ambalo hatua ya maisha au kifo inachukuliwa dhidi yake.
Pia alitaja kampeni ambayo chama kilifanya hapo awali ili kukwamisha mpango wa kutenganisha Sudan Kusini, akionya juu ya maafa na misiba ambayo Sudan ilipata kama matokeo ya kutenganishwa kwa Kusini, na jinsi Amerika ilivyofaulu katika hilo, na sasa inataka kutenganisha Darfur.
Kisha kiongozi wa ujumbe alimuelekeza Dkt. Muhammad Al-Haitham jukumu, na kumwambia kuwa kuna watu nyuma yako ambao lazima uwaelimishe juu ya mpango huu wa uhalifu ambao Amerika inafanya, hivyo Dkt. alikubaliana na mazungumzo ya ujumbe, na alisisitiza kuwa yuko pamoja na umoja wa umma na ni suala lake la hatima, na akasema tunakubaliana na mradi wa Hizb ut-Tahrir kukwamisha mpango wa Magharibi kafiri wa kutenganisha Darfur, na akasema ni lazima chama kiendelee na safari, na tuweke mikono yetu pamoja ili kukwamisha mpango huu mchafu wa kuikata Darfur kutoka Sudan.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Jimbo la Sudan

