Habari kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan
Wakutana na Idadi ya Viongozi wa Mji wa Al-Abyad
Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan, jana Jumatatu, Novemba 3, 2025, ulizuru idadi ya viongozi wa mji wa Al-Abyad, mji mkuu wa Kordofan Kaskazini. Ujumbe huo uliongozwa na Ustadhi Al-Nadhir Muhammad Hussein Abu Minhaj, mwanachama wa Baraza la Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan, akifuatana na Mhandisi Banqa Hamid, na Ustadhi Muhammad Saeed Boukeh, wanachama wa Hizb ut-Tahrir.
Ambapo ujumbe ulikutana na:
Ustadhi Khalid Hussein - Mkuu wa Chama cha Muungano wa Kidemokrasia, Tawi la Jalaa Al-Azhari.
Daktari Abdullah Yusuf Abu Seil - Wakili na Profesa wa Sheria katika Vyuo Vikuu.
Sheikh Abdul Rahim Jouda - kutoka kundi la Ansar al-Sunna.
Bwana Ahmed Muhammad - Mwandishi wa Shirika la Habari la Suna.
Mikutano hiyo iligusia mada ya sasa; kuanguka kwa Al-Fasher na uhalifu ulioambatana nao wa wanamgambo dhidi ya watu wa mji huo, na kuangusha kwa viongozi wa jeshi, ambao hawakutimiza wajibu wao kwa watu wa Al-Fasher na kuondoa mzingiro kutoka kwao, na wana uwezo wa kufanya hivyo katika kipindi chote cha mzingiro, na mashambulio ya mara kwa mara dhidi yao zaidi ya mashambulio 266.
Kisha ujumbe uliwakabidhi nakala ya chapisho la Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan lenye kichwa: "Kuanguka kwa Al-Fasher kunafungua njia kwa mpango wa Amerika wa kukata Mkoa wa Darfur na kuzingatia ushawishi wake nchini Sudan, hadi lini tutakuwa kuni za mzozo wa kimataifa?!".
Majibu yao yalikuwa ya kipekee na waliomba kuendelea kwa mikutano hii.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan