Habari kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Sudan
Wakutana na Mkurugenzi wa Idara ya Khalawi na Misikiti katika mji wa Port Sudan
Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Sudan, chini ya uongozi wa Ustadhi Nasser Reda, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut-Tahrir katika jimbo la Sudan, akiambatana na Ustadhi Abdullah Ismail, mwanachama wa Kamati ya Mawasiliano, walimtembelea Sheikh Onour Muhammad Ahmed, Mkurugenzi wa Idara ya Khalawi na Misikiti katika mji wa Port Sudan ofisini kwake, kama sehemu ya kampeni inayoandaliwa na chama, ili kukwamisha mpango wa kuigawa Sudan kwa kutenganisha Darfur.
Ustadhi Nasser alizungumzia yanayoendelea sasa Sudan mikononi mwa Magharibi makafiri, hasa Amerika; ambayo ilitenganisha kusini mwa Sudan, na sasa inajitahidi kutenganisha Darfur, kisha hatua inayofuata ni mashariki mwa Sudan. Jambo hili ni miongoni mwa mambo muhimu, na masuala ya hatima, hakuna uzembe ndani yake, na linahitaji kutoka kwa maimamu wa misikiti, na wanasiasa, na wasomi, na viongozi wa jeshi, na watu kwa ujumla, kufanya kazi kwa bidii ili kukwamisha mpango huu. Nasser alitoa ushahidi kadhaa unaothibitisha aliyoyasema.
Sheikh Onour alikubaliana na mazungumzo ya Nasser na akasema, jukumu letu ni lipi? Ustadhi Nasser alimueleza kinachotakiwa kutoka kwa maimamu na walinganiaji, hivyo Sheikh alimtaka amtumie programu ya chama ya kukwamisha mpango mzima.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Mkurugenzi wa ofisi, na Sheikh Labab, mwanachama wa Baraza la Maulamaa wa Jimbo, na Sheikh Al-Tayeb Al-Shambali, Mkurugenzi wa Masuala ya Wahifadhi katika jimbo la Bahari Nyekundu.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Jimbo la Sudan