Organization Logo

السودان - مكتب - ناطق

ولاية السودان

الخرطوم شرق- عمارة الوقف الطابق الأرضي -شارع 21 اكتوبر- غرب شارع المك نمر

Tel: 0912240143- 0912377707

spokman_sd@dbzmail.com

www.hizb-ut-tahrir.info

Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Sudan Wakutana na Mkuu wa Halmashauri ya Wanazuoni katika Jimbo la Nile Nyeupe
Press Release

Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Sudan Wakutana na Mkuu wa Halmashauri ya Wanazuoni katika Jimbo la Nile Nyeupe

September 09, 2025
Location

Habari kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Sudan

Wakutana na Mkuu wa Halmashauri ya Wanazuoni katika Jimbo la Nile Nyeupe

Siku ya Jumatatu iliyopita, 2025/9/8, katika mji mkuu wa Nile Nyeupe; mji wa Rabak, ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Jimbo la Sudan, ulikutana na Sheikh Allama Abdullah Al-Nour Toto, Imamu na Khatibu wa Msikiti Mkuu wa Asalaya, na Mkuu wa Tawi la Halmashauri ya Wanazuoni wa Sudan la Nile Nyeupe nyumbani kwake katika wilaya ya Asalaya. Ujumbe huo ulikuwa chini ya uongozi wa Dk. Ahmed Mohamed, mwanachama wa Hizb ut-Tahrir, akiambatana na maprofesa, Faisal Madani, Abdel-Magid Othman Abu Hajar, na Al-Zein Abdel-Rahman; wanachama wa Hizb ut-Tahrir, ambapo mkutano huo ulikuwa sehemu ya kampeni ya Hizb ut-Tahrir ya kuzuia kujitenga kwa Darfur.

Kiongozi wa ujumbe, Dk. Ahmed, alizungumza kuhusu ziara hiyo kuja kama sehemu ya kampeni iliyozinduliwa na chama kuzuia kujitenga kwa Darfur, akieleza mpango wa Marekani wa kutaka kuitenganisha Darfur, kupitia mpango wa mipaka ya damu, kwa kurarua lililoraruliwa, na jinsi mpango huo unavyoendelea katika njia ya kujitenga kama vile Kusini ilivyojitenga, na akieleza kwamba muumini haumwi kutoka tundu moja mara mbili, kwa hivyo hatutaruhusu Darfur kujitenga kama vile Kusini ilivyojitenga kwa haki ya kujitawala. Kiongozi wa ujumbe alisisitiza umuhimu wa umoja wa umma na kwamba ni mojawapo ya masuala muhimu, na kwamba umma hauwezi kusimamishwa kuzuia miradi ya kafiri isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah ambayo inaiunganisha.

Sheikh alifichua na kufafanua, baada ya kuishukuru chama, akisema: Ziara katika suala hili linalohusiana na umma wa Kiislamu na umoja wake, haitoshi masaa haya, na akasema: Magharibi inaufanyia umma hila na kupanga njama usiku na mchana, na akasema waziwazi: Ninatakiwa kufanya nini hasa? Tukamwambia: Kufanya kazi ya kuhamasisha watu ili kukwamisha mpango wa kutenganisha Darfur, na kwamba watu wanapaswa kujua kwamba hakuna njia isipokuwa umoja wa umma kwa kusimamisha Khilafah Rashidah.

Sheikh alihitimisha hotuba yake kwa kuwashukuru vijana wa chama, akisema: Ni mara yake ya kwanza kukutana na vijana kutoka Hizb ut-Tahrir katika ziara kwake, ingawa alikuwa amesoma kuwahusu, na alirekodi ziara yake katika maonyesho ya kitabu mwaka 2012. Akiahidi kwamba kilichobaki cha umri wake kitakuwa katika huduma ya mradi wa umoja wa umma, Mungu akipenda, na akasema: "Ahadi ni kwa Mungu".

Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir

Katika Jimbo la Sudan

Official Statement

السودان - مكتب - ناطق

ولاية السودان

السودان - مكتب - ناطق

Media Contact

السودان - مكتب - ناطق

Phone: 0912240143- 0912377707

Email: spokman_sd@dbzmail.com

السودان - مكتب - ناطق

الخرطوم شرق- عمارة الوقف الطابق الأرضي -شارع 21 اكتوبر- غرب شارع المك نمر

Tel: 0912240143- 0912377707 | spokman_sd@dbzmail.com

www.hizb-ut-tahrir.info

Reference: PR-01992e81-93e0-7c98-b17e-03334b00ee71