Habari kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan
watembelea idadi ya mawakili huko Al-Ubayyid
Katika mfumo wa kampeni ya Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan ya kufeli mpango wa Marekani wa kuitenganisha Darfur, ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir, ukiongozwa na Ustadhi Al-Nadhir Muhammad Hussein Abu Minhaj, mjumbe wa baraza la Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan, akifuatana na Ustadhi Muhiuddin Kajor, na Ustadhi Muhammad Saeed Boukeh, wajumbe wa chama, walifanya ziara siku ya Jumanne 2025/11/11, kwa idadi ya mawakili mashuhuri katika mji wa Al-Ubayyid, ambapo kiongozi wa ujumbe aliwaeleza lengo la kampeni ya chama, na jinsi tunavyoweza kufeli mpango huo mbaya.
Na Maustadhi waliotembelewa ni: Dkt. Khalfalla Hassan Ali Hamid Al-Muharami, na Ustadhi Mutasim Muhammad Ahmad, na Ustadhi Atif Baloul, na alikuwa pamoja naye Da'i Sheikh Hamid Balila, na Ustadhi Yusuf Ali Ahmad Saeed, na misimamo yao yote ilikuwa mizuri sana na inaunga mkono kampeni, na walishukuru chama kwa msimamo huu, na hatua hii inayohitajika.
Na mwishoni mwa ziara hizi, ujumbe uliwakabidhi ndugu mawakili nakala za machapisho ya chama, na waliwaahidi kuendeleza mikutano.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan