Msiba wa Mbeba Da'wa
Ustadh Yusuf Dhiab Al-Shalabi (Abu Dhiya)
﴿Miongoni mwa Waumini wapo watu walioshikamana na ahadi waliyoagana na Mwenyezi Mungu; basi wengine wao wamekwisha timiza nadhiri yao,
na wengine wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo.﴾
Imani yetu katika hukumu ya Mwenyezi Mungu na kwa kutarajia malipo, Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir/Jimbo la Jordan inamtangazia msiba wa mbeba da'wa katika safu zake: Ustadh Yusuf Dhiab Al-Shalabi (Abu Dhiya), ambaye amehamia katika rehema za Mwenyezi Mungu siku ya Alhamisi, Mosi Muharram 1447 Hijria, sawa na 2025/06/26 Miladia, akiwa na umri wa miaka themanini na tisa, baada ya ugonjwa mrefu ambao amehesabu thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu.
Abu Dhiya alitumia miaka ya umri wake akipambana, akisema ukweli, akishiriki kikamilifu katika matukio yote ambayo yanahitaji ujasiri katika kubeba da'wa kwa lugha yake fasaha ya Kiarabu ambayo alikuwa stadi na kuifundisha, akifuatilia kwa bidii hali ya Umma wa Kiislamu, hakuogopa lawama ya yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Azma yake haikupungua licha ya kufuatiliwa, kukamatwa na kunyanyaswa alikokumbana nako, na ugonjwa wake ambao haukumzuia isipokuwa katika miaka ya mwisho ya umri wake, Mwenyezi Mungu amrehemu marehemu wetu kwa rehema pana na amuweke katika bustani zake kubwa, na Mwenyezi Mungu akuzidisheni ujira ahli zake na jamaa zake na awape subira na faraja, na hatusemi isipokuwa kile kinachompendeza Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ndiye aliyetoa na ndiye aliyetwaa na kila kitu kwake kina kipimo.
﴿Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye ndio tutarejea﴾
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Katika Jimbo la Jordan