Jimbo la Bangladesh: Kongamano la Kisiasa "Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?"
September 16, 2025

Jimbo la Bangladesh: Kongamano la Kisiasa "Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?"

Jimbo la Bangladesh: Kongamano la Kisiasa "Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?"‎

Hizb ut-Tahrir / Jimbo la Bangladesh linaandaa kongamano la kisiasa lenye kichwa:

" Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?  "‎

Baada ya uasi wa wananchi mnamo Julai 2024 ambao ulimlazimisha dikteta Hasina kukimbia, watu wa Bangladesh walitarajia Bangladesh mpya (Bangladesh 2.0). Ili kutuliza uasi huo, muungano unaounga mkono Uingereza ulikabidhi mamlaka ya kisiasa kwa serikali ya mpito inayoongozwa na Yunus, mshirika wa Amerika.

Watu wamedai mabadiliko makubwa nchini Bangladesh, lakini Merika na Uingereza zimefanya njama dhidi ya matarajio ya watu kwa kudumisha mfumo wa kikoloni wa Magharibi -mfumo kandamizi wa kibepari wa kilimwengu- jinsi ulivyo. Chini ya bendera ya mageuzi, hawa wamelinda mfumo ulioshindwa kwa kubadilisha nyuso tu.

Serikali ya mpito imejiteua kuwa msimamizi wa uwongo wa uasi huo, kwani inawasaliti watu kwa upande mmoja kwa kuendeleza maslahi ya kijiografia na kiuchumi ya Amerika badala ya kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu, na kwa upande mwingine, vyama vya siasa vinavyounga mkono Amerika vinashiriki katika mapambano ya hisa zao za madaraka, ambayo yanaharibu utaratibu na sheria kupitia mizozo ya kisiasa, unyang'anyi, ukaidi, na vurugu.

Wakoloni wa Magharibi na polisi wao wa kikanda, India, bado wanaingilia mara kwa mara siasa zetu, haswa kwa kuendesha propaganda dhidi ya matarajio ya watu ya kurudi kwenye mfumo wa Kiislamu na kuanza tena maisha ya Kiislamu.

Kongamano hili la kisiasa litaweka wazi njama ya Merika, Uingereza na India dhidi ya matarajio ya watu katika uasi wa Julai 2024, na litatafuta kuelekeza uasi huo katika mwelekeo wake sahihi - ambayo ni mabadiliko kamili ya dola.

Kuweni nasi..

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Jimbo la Bangladesh

Ijumaa, 27 Rabi' al-Awwal 1447 Hijria, inayoambatana na 19 Septemba 2025 Miladia

Bangladish line

- Wakati na Mahali -

Kichwa: Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?
Tarehe: 19 Septemba 2025 Miladia
Muda: 04:00 alasiri (kwa saa za Madina) / 07:00 jioni (kwa saa za Bangladesh)
Muda: Saa moja na nusu

Bangladish line

- Matangazo ya Moja kwa Moja ya Kongamano -

bang 2025

Bangladish line

- Matangazo ya Moja kwa Moja ya Kongamano kutoka kwa Tovuti ya Odyssey -

1bang2025

Bangladish line

2025 09 19 BNG CONF EN 1

Bangladish line

Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea tovuti za Hizb ut-Tahrir / Jimbo la Bangladesh:

Tovuti rasmi ya Hizb ut-Tahrir / Jimbo la Bangladesh

Barua pepe ya Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir / Jimbo la Bangladesh

Bangladish line

More from null