Organization Logo

تونس - المكتب الإعلامي

ولاية تونس

Tel: 71345949

Fax: 71345950

http://www.ht-tunisia.info/ar/

Jimbo la Tunisia: Maombolezo ya Mbeba Da'wa, Ustadh Hassan Nower
Press Release

Jimbo la Tunisia: Maombolezo ya Mbeba Da'wa, Ustadh Hassan Nower

June 21, 2025
Location

Maombolezo ya Mbeba Da'wa

Ustadh Hassan Nower

﴿Miongoni mwa Waumini wapo watu waliosadiki yale waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Basi wengine wao wamekufa,

na wengine wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo

Hizb ut Tahrir katika jimbo la Tunisia inamuomboleza mmoja wa wanaume wake kutoka kwa wabebaji da'wa, Ustadh Hassan Nower, ambaye amefariki dunia leo Ijumaa, tarehe 24 Dhul-Hijjah 1446 Hijria, sawa na 2025/6/20 Miladia, baada ya kuugua kwa muda mrefu, ugonjwa uliomlemesha mwili wake lakini haukuzima mwenge wa ujumbe wake wala azma yake ya kufanya kazi katika safu za wafanyakazi wa kurejesha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume.

Mzee Hassan Nower, alishika wadhifa wa mhariri mkuu wa gazeti la At-Tahrir, alikuwa, Mwenyezi Mungu amrahamu, hakubali suluhu juu ya neno la haki, wala hakuwaogopa watu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, aliandika makala ambazo misimamo yake ilikuwa adimu, na alikabiliana na uonevu wa batili kwa haki, na alibaki mwaminifu kwa ahadi ya neno la kweli ambalo halikubali mkombo wala halinyamazi katika zama za ukimya katika ugonjwa wake wa mwisho.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amkubali katika watu wema, na ainue daraja yake katika daraja za juu, na awape familia yake, jamaa zake, wapenzi wake na masahaba zake wote subira, uthabiti na hesabu.

﴿Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye ndio marejeo yetu

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Jimbo la Tunisia

Official Statement

تونس - المكتب الإعلامي

ولاية تونس

تونس - المكتب الإعلامي

Media Contact

تونس - المكتب الإعلامي

Phone: 71345949

Fax: 71345950

Email:

تونس - المكتب الإعلامي

Tel: 71345949 |

Fax: 71345950

http://www.ht-tunisia.info/ar/

Reference: PR-01978897-cfe0-7e10-a3bd-5c347e69a5b6