Matangazo ya Kifo cha Mbebaji wa Da'wa
Mabrouk bin Nasser
﴿Na tutakujaribuni kwa hofu kidogo na njaa na upungufu wa mali na nafsi na matunda; na wabashirie wanaosubiri.﴾

Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Tunisia inatangaza kwa masikitiko na uchungu mwingi kifo cha ndugu Mabrouk bin Nasser ambaye amehamia kwa Bwana wake, Alhamisi tarehe 23 Dhul-Hijjah 1446 Hijria, sawa na 2025/6/19 Miladia, ambaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Hizb ut-Tahrir ambao walikuwa wakifanya kazi katika safu zake katika mazingira magumu zaidi ya ukandamizaji na udikteta, ambapo alikamatwa katika magereza ya Bourguiba na kisha katika magereza ya Ben Ali, alitumia akiwa mvumilivu na akitarajia malipo, na aliendelea kushikamana na da'wa yake na kujitolea kuibeba akiita Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, akiwa imara katika da'wa yake, akiamini ahadi ya Mola wake Mwenyezi na habari njema za Mtume wake mtukufu ﷺ, hadi umauti ulipomfika, hivyo ndivyo tunavyomhesabu na hatumsafishi mtu yeyote mbele ya Mungu.
Tunamuomba Mungu amuweke ndugu yetu Mabrouk bin Nasser katika Firdaus ya juu kabisa ya Pepo, na amjaalie kuwa pamoja na wale ambao Mungu amewaneemesha miongoni mwa Manabii na Masiddiq, Mashahidi na Watu wema na hao ni rafiki wema.
﴿Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea﴾
Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Tunisia