Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mayahudi Wanachimba Makaburi Yao Kwa Mikono Yao Wenyewe
Na Watawala Waislamu Wanazuia Umma Kuwazika
Wakati mabomu ya chombo cha Kiyahudi na mizinga yake yakimiminika juu ya vichwa vya watu wetu huko Gaza, ambapo wanapiga majengo ya makazi, vyuo vikuu, na misikiti, na hata kusawazisha mahema na ardhi, na mifupa ya watoto na nyama yao inachanganyika na vifusi, mkutano wa aibu na fedheha ulikutana na kumalizika, mkutano wa wanyonge kutoka Waarabu na wasio Waarabu. Mkutano huo, ambao uliitwa Mkutano wa Dharura wa Kiarabu na Kiislamu na ulifanyika Doha, haukutoa zaidi ya kile kilichotarajiwa kutoka kwa wanyonge hao; kukemea na kulaani tu. Na hata kulaani huku hakukuwa kwa mashahidi waliokufa huko Doha na Gaza, bali kwa shambulio linalodaiwa dhidi ya "uhuru wa ufalme wa Doha". Baada ya idadi ya mashahidi huko Gaza kuzidi makumi ya maelfu, hawakupata hata "chembe" ya kukemewa na kulaaniwa kwao. Kinyume chake, wanyonge hao walitoa taarifa ya kukemea "uchokozi wa usaliti na uovu wa Israel dhidi ya uhuru wa Doha", huku wakipitisha taarifa ya mwisho ambayo haitoki nje ya sera ya woga ambayo wamepitisha tangu walipoteuliwa juu ya shingo za umma bora uliotolewa kwa watu katika nchi za Kiislamu.
Haijapita akilini kwa vibaraka wa Amerika miongoni mwa washiriki katika jambo hili la upuuzi kukutana pembeni mwa mkutano huo ili kusisitiza kile kinachowashughulisha, ambacho ni kupambana na Uislamu na Waislamu. Abdel Fattah al-Sisi alikutana na Shehbaz Sharif, pembeni mwa ushiriki wake katika shughuli za mkutano huo. Balozi Mohamed El-Shennawy, msemaji rasmi wa urais wa Misri, alisema kuwa Sisi alianza mkutano huo kwa kutoa rambirambi za dhati kwa serikali na watu wa Pakistani kwa wahasiriwa wa mafuriko ya hivi karibuni, na kwa wahasiriwa wa shambulio la kigaidi lililotokea mnamo Septemba 13, akisisitiza msimamo thabiti wa serikali ya Misri katika kulaani aina zote za ugaidi na itikadi kali, na kukataa kwake kabisa matukio haya yanayotishia usalama na utulivu. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Pakistani alithamini jukumu zuri la Misri katika kutuliza hali ya mambo ya kikanda, akisifu juhudi za Cairo katika upatanishi wa kusitisha mapigano huko Gaza na juhudi zake za kupunguza mateso ya raia, pamoja na jukumu lake katika kuwezesha kufikiwa kwa makubaliano ya kuanza tena ushirikiano kati ya Iran na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki.
Wakati damu inachemka katika mishipa ya umma kwa kile kinachotokea katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, na mioyo yao inateketea kwa ajili ya ndugu zao dhaifu huko Gaza na Palestina kwa ujumla, na wakati umma unajiandaa kupigana na Wayahudi, na wakati wale waliokasirikiwa wanamkasirisha umma wa mabilioni mawili, kana kwamba hali yao inasema: "Kwa nini hamji kutuzika katika makaburi tuliyochimba kwa mikono yetu wenyewe?", katika nyakati hizi wanyonge hawa wanakutana wakati wanatawala umma ambao ungetaka kung'oa milima, ingeng'oa, vipi basi kuponda chombo cha uvamizi ambacho hakiwezi kusimama mbele ya nchi ndogo kabisa kutoka kwa nchi hizo zilizokusanyika?!
Ufafanuzi wa kitendawili hiki umekuwa ukijulikana kwa watu wote: hawa si watawala wa kweli wa umma, bali ni vibaraka wa nguvu za kikoloni za Magharibi na wafuasi wa uvamizi, na wengi wao ni Wayahudi, na kazi yao pekee ni kulinda maslahi ya Magharibi katika nchi za Waislamu, na kulinda chombo cha kansa na kambi ya kijeshi ya Magharibi iliyoendelea katikati ya nchi za Kiislamu. Pia wanafanya kazi ya kuzuia umoja wa umma wa Kiislamu na kuanzishwa kwa dola ya Kiislamu, Ukhalifa ulioongoka kwa njia ya unabii.
Kazi ya kuwafagilia na kufagilia ushawishi wa Magharibi kutoka nchi za Waislamu imekuwa ya haraka zaidi na ya lazima kuliko hapo awali, hasa kwa watu wa nguvu na ulinzi katika nchi za Waislamu, yaani majeshi na hasa jeshi la Pakistani la Mujahid Muislamu. Na imekuwa lazima kwa maafisa waaminifu ndani yake kutoa nusra kwa Hizb ut-Tahrir, kwa maana hii ndiyo kazi pekee ambayo inawaondolea lawama na kuhifadhi heshima yao ambayo imechafuliwa na viongozi wao wanyonge hawa. Ikiwa hawatofanya hivyo, watazama katika aibu na fedheha duniani kabla ya Akhera. Basi watainusuru lini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kuipa Hizb ut-Tahrir nusra ili isimamishe Ukhalifa ambao utahukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na kuandaa majeshi ya kukomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, na kulipiza kisasi kwa akina mama waliopoteza watoto wao, watoto na wazee, na kuzika uvamizi katika makaburi iliyochimba kwa mikono yake?
Hakika hii ni heshima ambayo haistahiliwi isipokuwa na yule anayestahili, basi nani anayestahili heshima ya kunusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake ﷺ miongoni mwa watu wa nusra ili aokoke adhabu ya Akhera na kupata neema ya Pepo?!
﴿Enyi mlio amini! Piganeni na wale walio karibu yenu miongoni mwa makafiri, na wajue kwenu ukali, na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu﴾
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Wilaya ya Pakistan