Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Lazima Vikundi Vyaaminifu nchini Bangladesh Viungane Dhidi ya Sera ya Kinyonge
Inayoendeshwa na Serikali ya Mpito Dhidi ya Amerika Mkafiri Mkoloni
Serikali ya mpito inaisaliti nchi kwa kuonyesha kusitasita kwake kulinda mipaka yetu dhidi ya Jeshi la Arakan linaloungwa mkono na Amerika, huku ikiwa na hamu ya kuwatuma wanajeshi wetu katika misheni ya kuwahudumia Amerika huko Ukraine. Kuanzia Disemba 2024 hadi Septemba 10, 2025, kundi la waasi lenye makao yake makuu nchini Myanmar liliwateka nyara wavuvi 325 kutoka maeneo mbalimbali kando ya Mto Naf na Ghuba ya Bengal, kama ilivyoripotiwa na bdnews24.com mnamo Septemba 12, 2025. Cha kushangaza ni kwamba serikali ya Yunus ililipuuza Jeshi la Arakan (ambalo ni mshirika wa Amerika) ambalo linafanya kazi katika nchi yetu na linatishia watu wetu na uhuru wetu. Wakati huo huo, iliharakisha kuunga mkono Ukraine ili kumfurahisha bwana wake mpya mkoloni, Amerika. Amerika inafikiria kupeleka vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika eneo la buffer kati ya Urusi na Ukraine ikiwa makubaliano ya amani ya mwisho yatafikiwa, na vikosi kutoka nchi zisizo wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Atlantiki ya Kaskazini (NATO), kama vile Bangladesh, vinaweza kupelekwa, kama ilivyoripotiwa na NBC News. Mshauri wa masuala ya kigeni katika serikali ya mpito, Touhid Hussein, aliliambia vyombo vya habari kwamba Bangladesh ingependa kushiriki katika operesheni yoyote kama hiyo. Zaidi ya hayo, vikosi vya usalama vya mpakani vya India vinaendelea kuwaua wana wetu katika maeneo ya mpakani, na watu zaidi wameuawa katika miezi ya hivi karibuni, huku serikali yetu haifanyi chochote au inafanya kidogo sana kuwalinda. Kwa hivyo, ni unafiki uliokithiri kwamba serikali yetu inataka kuwakodisha wanajeshi ambao tunawahitaji ndani kufanya kazi kama mamluki kwa niaba ya nchi za Magharibi.
Enyi Maafisa Waaminifu katika Jeshi la Kibangali: Tunawahakikishia na kuwakumbusha daima kwamba misheni za Umoja wa Mataifa za kulinda amani ni zana tu za ukoloni mamboleo unaoongozwa na Amerika kupitia serikali ya mpito, ambapo misheni hizi zinatumiwa kudhoofisha utulivu wa maeneo na kupata rasilimali na mali za kimkakati kwa ajili ya mfumo wa kimataifa wa Magharibi unaoongozwa na Amerika. Kwa kushiriki katika miradi hii, mnakuwa washirika katika miradi ya kikoloni ya makafiri wavamizi.
Enyi Maafisa: Watawala wetu wasaliti wamewafanya kuwa mchezo usio na thamani katika mfumo wa kimataifa wa kibepari wa Magharibi. Katika uroho wao wa kupata sarafu za kigeni za bei nafuu na kwa matumaini ya kupata uaminifu wa nchi za Magharibi, wanataka msisahau yaliyopita yenu tukufu. Ni jeshi la Waislamu pekee ndilo lililokomboa ubinadamu kutoka katika giza la makafiri tangu enzi ya Mtume ﷺ, ambapo halikujifungia ndani ya mipaka fulani, bali lilianza kuutendea haki ulimwengu kupitia jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu ﷻ. Lakini leo, watawala hawa wamewashusha hadi kiwango ambacho mnashindwa hata kulinda mipaka yenu, achilia mbali ulimwengu mzima. Jeshi la Khilafa halijawahi kutafuta maisha ya anasa kama wanajeshi mamluki wa himaya za Kirumi na Kiajemi kwa kubadilishana dhahabu na fedha. Lakini kwa bahati mbaya, watawala wetu wadanganyifu wamewafanya mpate dola katika misheni za Umoja wa Mataifa, na wamechukulia hilo kuwa sababu ya fahari yenu. Angalieni ni kwa kiwango gani mataifa ya kitaifa yamewafikisha leo!
Tunawaita mtoe nusra kwa Hizb ut-Tahrir ili kusimamisha Khilafa Rashidah kwa njia ya Utume. Lengo lenu pekee katika maisha lazima liwe kucheza nafasi muhimu katika kusimamisha Khilafa na kuondoa nguvu za kikafiri za Magharibi na mfumo wake wa kimataifa. Kumbukeni, hakuna umma wowote ambao umepata fursa hii kubwa ya kuhuisha Uislamu kikamilifu katika kipindi cha miaka 1400 iliyopita tangu enzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ﷻ anasema: ﴿Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili aishindishe dini yote, japo wachukie washirikina﴾.
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Bangladesh