Organization Logo

أفغانستان المكتب

ولاية أفغانستان

Tel:

hizbuttahrir.af@gmail.com

Lazima Majibu ya Kiburi cha Trump Yawe ni Kusimamisha tena Khilafah ya Pili iliyoongoka!
Press Release

Lazima Majibu ya Kiburi cha Trump Yawe ni Kusimamisha tena Khilafah ya Pili iliyoongoka!

September 22, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Lazima Majibu ya Kiburi cha Trump Yawe ni Kusimamisha tena Khilafah ya Pili iliyoongoka!

(Imetafsiriwa)

Mara nyingine tena, Donald Trump amechukua msimamo wa kiburi na wa kutishia dhidi ya serikali ya Afghanistan na Waislamu, akitangaza: "Ikiwa Taliban haitaikabidhi Marekani kambi ya Bagram iliyoijenga, mambo mabaya yatatokea."

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Afghanistan inalaani matamshi ya Trump kwa maneno makali zaidi, na inachukulia makubaliano yoyote katika suala hili kuwa ni usaliti kwa Uislamu, Jihadi, na damu ya mashahidi, na inaonya kwamba uwepo wowote mpya wa Amerika - haijalishi unaitwaje - utageuza Afghanistan kuwa uwanja wa mapambano kwa nguvu kuu za kikoloni zinazoshindana.

Matamshi ya Trump yanaweza kusomwa kama jaribio la kuishinikiza mamlaka ya Afghanistan kupata makubaliano ya kisiasa, kiuchumi au kiusalama, au kama tishio kwa nchi za eneo hilo. Lakini kilicho wazi ni mawazo yake ya kikoloni kuelekea Afghanistan. Kambi ya anga ya Bagram, ambayo ilikuwa kituo cha makumi ya maelfu ya wanajeshi wa Marekani na ishara ya nguvu ya Marekani katika eneo hilo, iliondolewa baada ya Marekani kushindwa katika vita vya Afghanistan. Kuondoka kwa Marekani kutoka Bagram haikuwa tu mwisho wa uwepo wa kijeshi; lakini pia ilikuwa ishara ya kupungua kwa nguvu na ushawishi wa Marekani kikanda na kimataifa, kushindwa ambayo sasa kunateketeza moyo wa Trump. Wakati huo huo, baadhi ya pande za ndani na nje, kupitia mawasiliano au shinikizo la kisiasa, zinajaribu kubadilisha baadhi ya viwango vya Kiislamu vya watawala na kuwahimiza kukubali, kurudi nyuma, au kufanya mikataba katika suala hili. Yeyote anayefikiria kwamba kuimarisha ushirikiano na Marekani, au hata kurudi kijeshi, kutaifaidisha Afghanistan amekosea sana. Hii ndiyo udanganyifu ule ule uliowaongoza watawala wasaliti wa Kiarabu kupatana na Marekani, na ni mantiki ile ile iliyotolewa na watawala wa Republican, mantiki ambayo haijaleta ila dharau, kukimbia, kuanguka na kujitenga na Uislamu.

Ardhi za Kiislamu ni mali ya Waislamu, na sheria ya Kiislamu pekee ndiyo marejeo ya kuamua hatima yao. Marekani, taifa linalopigana, halisimami tu katika upinzani wa kimsingi na wa kisiasa, bali pia katika uadui wa kijeshi dhidi ya Umma wa Kiislamu, bali dhidi ya ubinadamu wote. Marekani imeauni hadharani mauaji ya kimbari huko Gaza yanayofanywa na chombo cha Kiyahudi, na sasa inaandaa mkataba wa kuwauzia silaha za thamani ya dola bilioni 6.4, kwa lengo la kuua, kuwafukuza na kuwanyima Waislamu zaidi. Jibu la Uislamu kwa madhalimu hawa wenye kiburi ni lipi ila Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?

Watawala wa Afghanistan wanapaswa kutambua kwamba hili ni jaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mtukufu, ili kuwatofautisha wenye kushukuru na wenye kukufuru. Lazima wafanye kazi ya kufufua roho ya Uislamu, ustahimilivu na Jihadi katika jamii kwa njia ya kimfumo. Lazima wawe waangalifu dhidi ya unyonge na kupenda dunia kwao wenyewe na kwa jamii. Mtume ﷺ alipoulizwa, "Ni udhaifu gani?" alisema: «Ni kupenda dunia na kuchukia mauti», sifa hizi huondoa hofu ya adui kutoka mioyoni mwa Waislamu. Na ingawa Trump anatishia na kujaribu kuwatisha watawala na matokeo, lazima tukumbuke kwamba Shetani pia hunong'oneza na kueneza hofu ya matokeo ya matendo fulani; hatupaswi kuruhusu maneno hayo ya kishetani na ya kiburi kujaza mioyo yetu na hofu au kutusukuma kukata tamaa. Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Huyo si mwingine ila ni Shetani anawatisha marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni mimi, ikiwa nyinyi ni Waumini﴾.

Kumbukeni: Maadamu tumezuiwa katika mfumo wa taifa la kisasa na viwango vyake vya sasa vya kisiasa, roho yetu ya Jihadi itadhoofika, na jitihada zetu za kukaribia mfumo wa kimataifa zitaweka hatari ya kurudia historia ya ukoloni huko Afghanistan. Maadui wanasisitiza kutumia udanganyifu, hila na mipango ya kuwadhoofisha Waislamu. Kwa hiyo, mpaka tuanzishe nguzo ya kisiasa ambayo kitovu chake ni Uislamu na Umma wa Kiislamu, na mpaka tuisimamishe tena Khilafah iliyoongoka, adui ataendelea kututisha kwa ujeuri na kutangaza uvamizi wa ardhi zetu.

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Afghanistan

Official Statement

أفغانستان المكتب

ولاية أفغانستان

أفغانستان المكتب

Media Contact

أفغانستان المكتب

Phone:

Email: hizbuttahrir.af@gmail.com

أفغانستان المكتب

Tel: | hizbuttahrir.af@gmail.com

Reference: PR-01996cda-7440-7980-a4f0-86559b9dd178