Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Siku ya Katiba: Miaka Sitini ya Kushindwa kwa Katiba ya Kisekula
(Imetafsiriwa)
Agosti 27, 2025 inaashiria kumbukumbu ya miaka kumi na tano ya kutungwa kwa Sheria Kuu ya 2010. Katiba ya Kenya ya 2010 ilisifiwa kama ya mageuzi, ikianzisha mageuzi muhimu ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yaliyolenga kukomesha miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu chini ya katiba iliyopita.
Katika suala hili, Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya, tungependa kufafanua yafuatayo:
Tangu ilipotungwa, mizozo ya kikatiba nchini Kenya imejikita zaidi katika mianya ya utekelezaji, mizozo ya uchaguzi, utengano wa mamlaka, kanuni ya jinsia, na mchakato wa marekebisho. Kama Dkt. Willy Mutunga, Jaji Mkuu wa kwanza nchini Kenya, alivyosema mara kwa mara, Katiba ya Kenya ya 2010 ni hati ya maendeleo ambayo itachukua angalau miaka 20-30 kutekelezwa kikamilifu. Dhana kwamba katiba mpya itaweza kushughulikia matatizo ambayo katiba ya kikoloni ilishindwa kushughulikia, basi miaka 15 ni ushahidi tosha wa kushindwa vibaya kwa katiba ya kisekula, na kisa pekee cha mafanikio ni kuongeza muda wa maisha duni, kuzidisha rushwa, hali mbaya ya kiuchumi, mauaji ya kiholela, na mengine mengi.
Ni rahisi kwa vyombo vya kisiasa kuendesha katiba za kilimwengu, ambapo maslahi ya kisiasa hupewa kipaumbele hata kuliko sheria na katiba. Msingi wa katiba mpya iliyopigiwa kura na Wakenya baada ya kura ya maoni ya 2010 kimsingi ni sawa na katiba ya zamani ya kikoloni katika kumpa mwanadamu uhuru kamili na kuunyima Muumba wa mwanadamu, uhai na ulimwengu kama chanzo pekee cha mwongozo na sheria. Ukweli wa katiba za kilimwengu unaonyesha udhaifu wa asili ya binadamu katika kuamua mwongozo wa wanadamu ambapo mara nyingi hukabiliwa na ujanja na marekebisho au hata uundaji kamili wa hati mpya. Hatimaye, historia imethibitisha mara kwa mara kwamba mwanadamu hawezi kuwa chanzo cha mwongozo wa kufikia ukombozi wa kweli kutoka kwa dosari za katiba za kidemokrasia ambazo kanuni mbaya ya kibepari hustawi. Hakika, tunatoa wito kwa watu kutoka matabaka yote ya jamii, ikiwa ni pamoja na wasomi, wanazuoni na wanasiasa, kufanya kazi ya kuimarisha mwongozo wa kimungu ambao hauelekei kurekebishwa na si mawindo ya uongozi unaozingatia ubinafsi. Hakika, mwanadamu anahitaji mwongozo unaotoka kwa Mwenyezi Mungu. Ukombozi huu ulidhihirika wazi katika hotuba ya Rib'i bin Amir kwa Rustum, kamanda wa Milki ya Uajemi: "Mwenyezi Mungu ametutuma ili tuwaokoe watu kutoka katika ibada ya watu kwenda katika ibada ya Mola wa watu, na kutoka katika dhuluma ya dini kwenda katika uadilifu wa Uislamu, na kutoka katika dhiki ya dunia kwenda katika upana wa dunia na Akhera."
Katiba ni hati muhimu inayoamua mfumo wa utawala, inaanzisha mkataba kati ya watawala na raia, na pia ni usemi wa itikadi na maadili ya taifa ambayo huongoza nyanja zote za maisha. Uislamu, kama itikadi kamili, unahitaji katiba inayotokana na sheria za Mwenyezi Mungu. Katiba hii inaweza kutekelezwa tu kupitia Dola ya Khilafah, itakayoundwa hivi karibuni, kwa idhini ya Mungu, katika mojawapo ya nchi za Kiislamu.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi wa Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya