null
null
null
null
null
null
null
null
null
null
Wabashirie wanafiki kwamba watakuwa na adhabu chungu. (138) Ambao wanawafanya makafiri kuwa marafiki badala ya waumini. Je, wanataka utukufu kwao? Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. (139) Naye amekwisha kuteremshia juu yenu katika Kitabu kwamba mnaposikia aya za Mwenyezi Mungu zikikanushwa na kufanyiwa mzaha, basi msikae nao mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hakika nyinyi hapo mtakuwa kama wao. Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanafiki na makafiri pamoja katika Jahannamu. (140)
null