Khilafa Inanyakua Wanayoyazua
Habari:
Ameeleza kufungamana kwake na "Dira ya Israeli Kuu"... Netanyahu katika mahojiano na kituo cha I24: Nina ujumbe wa kihistoria wa kiroho unaorithiwa na vizazi. (Kituo cha Al Jazeera (jukwaa la X), Agosti 13, 2025)
Maoni:
Lengo la "Israeli Kuu" linahitaji kunyakua ardhi kutoka Misri, Jordan, Syria, Lebanon, Iraq na Rasi ya Arabia, ambayo ni matamanio yasiyowezekana na maono yasiyo ya kisiasa. Hiyo ni kwa sababu matendo makuu kama haya na mabadiliko katika ramani za kijiografia na kisiasa za eneo hilo kwa hakika ni makubwa kuliko Netanyahu, serikali yake na chombo chake, kwani Amerika, bibi wa eneo hilo - kwa bahati mbaya - haijaonyesha dalili zozote za hamu ya mabadiliko kama anavyoota Netanyahu, jambo linalofanya wazo hilo kufanana na propaganda za kibinafsi kwa Netanyahu, kwa kuzingatia harakati za mwili na sauti alizoonekana nazo katika mkutano uliotajwa, kwa njia ambayo anataka kuonekana kama kiongozi wa kihistoria!
Na chochote kusudi la taarifa hiyo, ukweli mchungu ni kwamba eneo hilo linaweza kubadilishwa katika ramani kwa namna yoyote na wakati wowote nguvu kuu zinapotaka. Ilikuwa hivyo mwanzoni mwa karne iliyopita mikononi mwa Ufaransa na Uingereza, na ikaendelea kwa kasi ndogo mikononi mwa Amerika; mistari bandia ya kijiografia na vyombo vya kitaifa ambavyo ni geni kwa utamaduni wa watu wa eneo hilo, kupanda chombo cha Kiyahudi, kuunganisha Syria na Misri kisha kuzitenganisha, kutenganisha Sudan Kusini na Kaskazini, kugawanya Iraq kwa mistari ya kimadhehebu iliyojaa damu, na inaonekana kuwa ni mazingira ya Syria mpya...
Na hivyo kukata, kubandika na kushona kutaendelea kulingana na ukubwa na maslahi ya nchi kubwa, hadi Waislamu, watu wa eneo hilo, watakaposema, imetosha! Na msemo huu utatafsiriwa kuwa nguvu ya kiakili ya kisiasa yenye ufahamu ambayo inarejesha mambo katika asili yake; dola ya Khilafa kwa njia ya unabii inarejesha heshima, utukufu, nchi na mali zao na utakatifu wao kwa Waislamu.
Hapo ndipo patakuwa na makabiliano makubwa na Amerika na nchi kubwa, ama chombo cha Kiyahudi hakitakuwa chochote ila nzi, ambaye Khilafa itamfukuza kutoka puani mwake.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya ofisi ya habari kuu ya Hizb ut-Tahrir
Mh. Osama Al-Thuaini