Hakuna Ndogo Wala Kubwa Na Kuangamia Kwenu Ni Ahadi Ya Kimungu
Habari:
Kukataa kwa Kiarabu matamshi ya Netanyahu kuhusu (Israel Kuu)... (Raai Al-Youm)
Maoni:
Netanyahu alitangaza waziwazi na bila kificho kwa taarifa fupi kwamba hili ni matakwa ya Mola na ahadi yake kwa watu wake wateule na yeye ndiye aliyechaguliwa kutekeleza mradi huu mkuu unaoitwa (Dira ya Israel Kuu).
Je, haujafikiwa na hamasa ya makabila katika Sham, Jordan, Iraq na Peninsula ya Arabia, Ewe Natani? Je, hujui kuwa ardhi ina watu wake, ikiinuka kutoka makao yake haikae tena isipokuwa juu ya uharibifu wa ufalme wako ambao unatarajia kivuli chake.
Amezungumza kile kinachoendelea katika duru zilizofungwa na kile kinachojulikana na wanadamu wote isipokuwa watawala wanaotamani kuanzisha uhusiano wa kawaida na wanaotembea katika njia ya upofu mkuu! Na cheo kikubwa ambacho hakipatikani ila kwa kipofu mkuu katika mkusanyiko wa Mashariki wa Freemason, haoni wala hasikii wala hajisikii, na akipigwa shavu la kulia, anatoa shavu la kushoto, anakubali uovu katika watu wake na anachukulia hilo kuwa ni maendeleo, ustaarabu na ujanja wa kisiasa!
Ama msimamo dhaifu na hafifu na sauti tulivu kwa haya iliyotoka kwa nchi za Kiarabu na ambayo matamshi ya Netanyahu yamezielekeza, ni kukemea, kulaani na kuchukizwa na matamshi haya kana kwamba lugha yao inasema usitufedheheshe ewe Bibi na usitufungulie milango ya Jahannamu kwa matamshi yako haya, unalipua bomu ambalo hakuna ajuaye upeo wa athari zake na matokeo yake isipokuwa Mungu, linaweza kugeuza meza juu yako na juu yetu na mradi wako ambao tunakubaliana nawe juu yake utakuwa vumbi lililotawanyika.
Kwa hivyo majibu ya hawa hayakuwa ila jibu la aibu kwa mtu mwenye kiburi na jasiri ambaye anatambua anazungumza na nani na anazungumza naye vipi, na anajua maadui ni nani na marafiki ni nani, na lau kama hawa wenye aibu na wanaochukizwa wangekuwa na majibu ya kiume, jibu lingekuwa kile unachoona si kile unachosikia, lakini hilo halipo, mmiliki wake Harun al-Rashid amekufa, na laiti Omar angekuwa kati yetu, huyu mjinga mwenye aibu hangethubutu kusema neno, bali hangalikuwa na athari yoyote yeye wala taasisi yake.
﴿NA M/MUNGU NI MWENYE KUSHINDA KATIKA MAMBO YAKE, LAKINI WATU WENGI HAWAJUI﴾
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Salim Abu Subaitan