July 25, 2025 295 views

Ofisi Kuu: Sehemu ya Wanawake "Kampeni ya Ulimwengu - Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Kukata Tamaa"

Ofisi Kuu: Sehemu ya Wanawake "Kampeni ya Ulimwengu - Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Kukata Tamaa"

 Sudan Profile Pic AR copy 

 Mzozo wa kikatili nchini Sudan kati ya Jeshi la Wanajeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, mtawala wa Sudan, na kikundi cha wanamgambo, Kikosi cha Msaada wa Haraka kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), naibu wa zamani wa Burhan katika Baraza la Utawala, umeingia mwaka wake wa tatu sasa. Baadhi ya makadirio yanaonyesha kuwa idadi ya vifo imefikia 150,000 huku ukatili mbaya ukifanywa na pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya umati, mateso na ubakaji wa kimbari. Pia kumekuwa na ripoti za utakaso wa kikabila na mauaji yaliyofanyika katika miji, vijiji na kambi mbalimbali za wakimbizi. Vita vimesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu, mzozo mkubwa wa wakimbizi na mzozo mkubwa wa njaa duniani, huku nusu ya watu milioni 50 wakikabiliwa na njaa.

Hata hivyo, mzozo huu umeelezwa kuwa "vita vilivyosahaulika" na "mgogoro uliofichwa na usioonekana" kwa sababu haujapata umakini wa kimataifa na habari za kimataifa unazostahili. Kwa hivyo, Sehemu ya Wanawake katika Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni ya ulimwengu ili kuangazia janga linalozidi kuwa mbaya la kibinadamu linalowakumba Waislamu wa Sudan. Kampeni pia itashughulikia: sera na ajenda zilizofichwa nyuma ya mzozo, nchi za kikanda na kimataifa zinazodhamini vita na sababu zake, historia ya Sudan na mambo ambayo yamesababisha migogoro yake ya hivi karibuni na kushindwa kwake kiuchumi, na kwa nini mfumo wa demokrasia utashindwa kutatua matatizo mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kikabila na kijamii ya Sudan, na jinsi uongozi wa Kiislamu wa Dola ya Khilafah Rashidah unaweza kujenga mustakabali mzuri, salama na wenye mafanikio kwa Sudan na nchi nyingine za Kiislamu.


﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye lile linalo kuishieni﴾

 [Surah Al-Anfal: 24]

Sehemu ya Wanawake katika Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir

Jumamosi, 01 Safar Al-Khair 1447 Hijria sawa na 26 Julai 2025 Miladia

N CMO

- Kufuatilia kampeni katika lugha zingine -

English

Türkçe

Deutsch

Urdu

Kiswahili

Français

 N CMO

Kusoma taarifa kwa vyombo vya habari ya Sehemu ya Wanawake

ambayo ilitangaza uzinduzi wa kampeni yake ya ulimwengu yenye kichwa:

"Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Kukata Tamaa"

Jumamosi, 01 Safar Al-Khair 1447 Hijria sawa na 26 Julai 2025 Miladia

Bonyeza hapa

N CMO

Rekodi ya utangazaji ya uzinduzi wa kampeni ya ulimwengu

"Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Kukata Tamaa"

N CMO

فلاير السودان2 

N CMO

- Hashtag za Kampeni -

#MgogoroWaSudan

#SudanCrisis

#SudanKrizi

#SoudanCrise

 N CMO

- Kufuatilia kampeni ya ulimwengu katika vyombo vya mawasiliano vya kielektroniki -

Facebook: QANITATHT1

Twitter: @ALQANITAT

Instagram: @WOMEN_SHARIA

N CMO

غلاف السودان

N CMO

More from null