Sudan: Janga la Karne Lililofichwa Machoni pa Ulimwengu
Dola ya Kiislamu, mlinzi wa raia wake, haipo, na Waislamu wanaishi katika dhiki, mateso na majanga katika sehemu mbalimbali za dunia, ikiwa ni pamoja na Sudan, ambayo kwa sasa inakabiliwa na mojawapo ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu katika historia ya kisasa kutokana na mapigano ya umwagaji damu yanayoendelea kwa miaka miwili kati ya jeshi na vikosi vya msaada wa haraka, ambayo yamesababisha majanga ya kutisha ambayo hakuna mtu anayezungumzia au kujaribu kuyazuia. Vita vilivyosahaulika ambavyo vyombo vya habari havitoi mwanga wowote, na hakuna nchi au taasisi zinazofichua mambo yake ya ndani.
Wakazi wanateseka kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki, uhamaji, ukimbizi wa kulazimishwa, njaa, magonjwa, unyanyasaji wa kijinsia na majanga mengine, na hakuna mwangalizi au msimamizi!
Pamoja na ukatili unaofanywa na pande zote zinazopigana, makadirio yanaonyesha idadi kubwa ya vifo na majeruhi, hasa miongoni mwa wanawake, watoto na wazee. Idadi ya vifo imekadiriwa kuwa si chini ya watu 150,000, ambapo zaidi ya 60,000 wako katika jimbo la Khartoum pekee katika miezi 14 ya kwanza ya mzozo.
Idadi ya majeruhi imezidi watu 70,000, huku kukiwa na matatizo makubwa ya kupata huduma za matibabu kutokana na kuporomoka kwa mfumo wa afya na kusimamishwa kwa kazi kwa 70-80% ya taasisi za afya, na kuenea kwa magonjwa kama vile kipindupindu, surua na kuhara. Vile vile, elimu imeporomoka; kuna karibu watoto milioni 20 nchini Sudan leo ambao hawaendi shule.
Maeneo mengi yameshuhudia mauaji ya kutisha, kunyongwa kwa ubaridi, utekaji nyara na mateso, ikiwa ni pamoja na watoto. Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na machinjio ya Wad Al-Noura, Al-Hilaliya, Jalqani, Al-Sureiha, Tamboul, kambi ya Zamzam, vijiji vya Darfur Kaskazini, Al-Geneina, Ardumta na vijiji vya jimbo la Nile Nyeupe katikati mwa nchi, ambayo ilisababisha vifo vya maelfu ya raia na kuwahamisha mamia ya maelfu. Mbali na hayo, kuna uhalifu wa unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji wa kimbari dhidi ya wanawake, wasichana na hata watoto.
Mapigano haya yamesababisha watu zaidi ya milioni 14 kuyahama makazi yao, kulingana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa la Umoja wa Mataifa; ambapo zaidi ya milioni 11 wameyakimbia makazi yao ndani ya Sudan, na zaidi ya milioni 3 wamekimbilia nchi jirani kama vile Misri, Ethiopia, Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Chad, na hata Jordan.
Watoto wanawakilisha 53% ya watu waliokimbia makazi yao ndani ya nchi, na kuifanya Sudan kuwa janga kubwa zaidi la uhamaji wa ndani duniani, huku watu waliokimbia makazi yao wakiwa karibu theluthi moja ya wakazi wa Sudan wapatao milioni 50. Kambi za wakimbizi hazina huduma za msingi, kwani wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji safi na usafi, na huduma za afya. Pia, kambi hizi zinakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara, ambayo huongeza mateso ya wakimbizi.
Haya yote yamesababisha mzozo mkubwa wa chakula, hasa kwa vile pande zote mbili zinatumia njaa kama silaha ya vita kwa kuzuia chakula kuingia katika maeneo wanayoyadhibiti, ambapo takriban watu milioni 25 - karibu nusu ya wakazi - wanahitaji misaada ya chakula, hasa katika kambi za wakimbizi. Mamia ya maelfu ya watoto wanakabiliwa na utapiamlo mkali, na idadi kubwa yao wako hatarini kufa. Ripoti zinaonyesha kuwa takriban watoto milioni 3.7 nchini Sudan wanakabiliwa na utapiamlo, na matarajio ya kuongezeka kwa idadi hii ikiwa hali itaendelea hivi, na uwezekano wa vifo vya takriban watoto 220,000 wanaokabiliwa na utapiamlo mkali.
Hiyo ni kusema, Sudan, ambayo ilizingatiwa kuwa kikapu cha chakula cha ulimwengu kwa sababu ya wingi wa ardhi ya kilimo, maji na mifugo, watu wake wamekuwa wakisumbuliwa na njaa, umaskini, magonjwa na uhamaji, na inakabiliwa na janga kubwa zaidi la kibinadamu katika nyanja zote kutokana na vita vilivyolaaniwa kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka, ili kuendelea kutimiza matakwa ya bibi yao Amerika nchini Sudan na utajiri wake, ambao unalipiwa gharama kubwa na watu wa Sudan waliokumbwa na janga hili pekee.
Mapigano haya yataendelea nchini Sudan na nchi nyingine za Kiislamu mradi tu tamaa za kikoloni zinaendelea kuwepo, na watawala vibaraka wamekaa juu ya vifua vyao. Kwa hivyo, fanyeni kazi, enyi watu, kuwavua madaraka na kupata dola ya pili ya Khilafa iliyoongoka kwa mwongozo wa unabii ili Sudan na nchi zote za Kiislamu ziweze kukombolewa kutoka kwa minyororo ya ukoloni katika aina zake zote na mbinu zake. Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hayabadili neema aliyowafanyia watu mpaka wabadili yaliyomo katika nafsi zao﴾.
Kama Ibn Majah alivyosimulia kwa isnadi yake kwa Abdullah bin Omar, Mwenyezi Mungu awaridhie, akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alituelekea na akasema: "Enyi kundi la wahajiri: mambo matano ambayo mkiyakumbatia, na ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu msiyakute; Uasherati hautadhiri katika watu wowote mpaka wauweke wazi isipokuwa utaenea miongoni mwao tauni na magonjwa ambayo hayakuwahi kuwepo katika waliotangulia miongoni mwao, na hawapunguzi kipimo na mizani isipokuwa watachukuliwa kwa miaka na ukali wa gharama na dhuluma ya mtawala juu yao, na hawazuii zaka ya mali zao isipokuwa wanazuiwa mvua kutoka mbinguni, na lau si wanyama wasingenyeshewa mvua, na hawavunji ahadi ya Mwenyezi Mungu na ahadi ya Mtume wake isipokuwa Mwenyezi Mungu huwapa maadui kutoka kwao na kuchukua baadhi ya yaliyo mikononi mwao, na madamu viongozi wao hawata hukumu kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuchagua kutoka katika aliyoteremsha Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu atafanya vita vyao kuwa baina yao". Na hii, wallahi, ndiyo hali yetu katika nchi za Kiislamu tangu kuzama kwa jua la Khilafa na mchungaji na kiongozi anayehukumu kwa sheria na dini ya Mwenyezi Mungu.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya ofisi ya habari kuu ya Hizb ut-Tahrir
Muslima Al-Shami (Um Suhaib)