August 19, 2025 2097 views

Jibu la Swali: Matukio ya Armenia na Azabajani

Jibu la Swali

Matukio ya Armenia na Azabajani

Swali:

Uwepo wa Urusi katika eneo la kusini mwa Caucasus ulitikisika (baada ya Armenia na Azabajani kutiia tangazo la pamoja na Marekani kuhusu suluhu ya amani na makubaliano katika nyanja za biashara na usalama baada ya mzozo wa zaidi ya miaka 35 kati ya nchi hizo mbili jirani.. Al Jazeera 2025/8/15) Azabajani na Armenia zilikuwa zimetoa taarifa ya pamoja mnamo 2025/8/11, kufuatia makubaliano yaliyosainiwa kati yao huko Washington mnamo 2025/8/8, zikiomba pande zingine kutatua kundi la Minsk lililoanzishwa mnamo 1992 kutatua shida kati ya nchi hizo mbili. Na ilisisitiza kufungua mawasiliano kati yao kwa usafiri wa ndani, nchi mbili na kimataifa... Hili lilifanywaje wakati ambapo mahusiano kati yao yalikuwa yamechafuka na yenye vita, haswa katika nyakati za hivi karibuni? Na malengo yaliyokusudiwa ni yapi? Na Mungu akubariki kwa kheri.

Jibu: Ili jibu liwe wazi, tunapitia mambo yafuatayo:

1- Ukurasa wa Armenpress kwa Kiarabu ulichapisha mnamo 2025/8/9 maandishi ya makubaliano yaliyosainiwa na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev mbele ya Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House katika mji mkuu wa Marekani, Washington. Ilisisitiza ("kusainiwa kwa herufi za mwanzo za maandishi yaliyokubaliwa ya makubaliano ya kuanzisha amani na uhusiano wa kimataifa kati ya nchi mbili, Azabajani na Armenia, na kuendelea na juhudi zaidi kuelekea kutiwa saini rasmi, kusisitiza juu ya kudumisha na kukuza amani kati yao, na kuchora njia ya mustakabali usioamuliwa na mizozo ya zamani kulingana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na tangazo la "Alma-Ata la 1991". Hilo ni tangazo linalohusiana na makubaliano ya kuweka mipaka kati ya nchi hizo mbili baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti na kutengana kwa Azabajani na Armenia kutoka humo, na kutambuana kwa pande zote mbili, kuheshimiana uhuru na kutotumia nguvu kutatua mizozo. "Pia pande hizo mbili zilisistiza umuhimu wa kufungua mawasiliano kati ya nchi hizo mbili kwa usafiri wa ndani, nchi mbili na kimataifa kwa msingi wa kuheshimu uhuru wa nchi, uadilifu wa ardhi yake na mamlaka yake ya kisheria ili kukuza amani, utulivu na ustawi. Juhudi hizi zitajumuisha mawasiliano bila kizuizi kati ya sehemu kuu ya Azabajani na eneo la Nakhichevan (Nakhjawan) linalojitawala kupitia ardhi ya Armenia.") Hivyo makubaliano hayo yalilenga kufungua mawasiliano, usafiri na barabara kati ya nchi hizo mbili kwa sababu ya umuhimu wa suala hili. Kwa kuwa eneo la Nakhchivan, ambalo ni mali ya Azabajani, halijaunganishwa nayo na limekatwa na Armenia, na ili kuwasiliana, Waazeri lazima wapitie Iran. Makubaliano hayo yanaomba kufunguliwa kwa barabara kati ya Azabajani na mkoa wake wa Nakhchivan. Pia inaomba kufunguliwa kwa barabara kati ya Azabajani na Uturuki, kwani Armenia iko kati yao, na hakuna mawasiliano ya nchi kavu yanayowezekana isipokuwa kupitia Armenia... Na kwa njia hii, Amerika inaweza kuimarisha ushawishi wake nchini Azabajani na kueneza ushawishi wake nchini Armenia na kudhoofisha au kuondoa ushawishi wa Urusi huko.

2- Maandishi ya makubaliano pia yalisema, kama ilivyoripotiwa na ukurasa wa Armenpress kwa Kiarabu mnamo 2025/8/9, kwamba ("Armenia itafanya kazi na Amerika na washirika wa tatu walioafikiwa kwa pamoja kubaini mfumo wa utekelezaji wa mpango wa mawasiliano kupitia kile kinachoitwa "Njia ya Trump ya Amani na Ustawi wa Kimataifa" (TRIP) katika ardhi ya Armenia"). Amerika ilikuwa tayari imetoa ofa ya kuanzisha ukanda huu na kuukodisha kupitia kampuni ya kibiashara ya Marekani. Tovuti ya Middle East Eye iliripoti mnamo 2025/7/14 kwamba ("Amerika ilitoa kuchukua ukanda uliopangwa kati ya Armenia na Azabajani ili kuendeleza mazungumzo yaliyokwama kati yao, na kwamba Balozi wa Marekani nchini Uturuki Thomas Barrack alifichua ofa hii wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari siku ya Ijumaa (2024/7/11)", na tovuti hiyo ilinukuu kauli za Barrack kuhusu ukanda huo, ambao una urefu wa kilomita 32, ambapo alisema: "Wanabishana kuhusu kilomita 32 za barabara, lakini si suala dogo, limekuwa likiendelea kwa muongo mzima, kisha Marekani inakuja na kusema sawa, tutauchukua. Tupe kilomita 32 za barabara chini ya mkataba wa kukodisha kwa miaka 100 na mnaweza kuigawanya nyinyi wote"). Hii itaongeza ushawishi wa Marekani katika nchi hizo mbili. Hii inathibitishwa na kile Shirika la Habari la Reuters liliripoti mnamo 2025/8/8 kwamba ("Armenia ilikubali mpango wa Trump wa kukodisha ukanda wa mawasiliano na Jamhuri ya Azabajani kwa miaka 100, ambayo inamaanisha kwamba Marekani inatafuta kulazimisha neno lake juu ya mzozo unaoendelea kati ya Azabajani na Armenia. Ambapo ya kwanza, kwa msaada wa Uturuki, inatafuta kufungua njia ya mkoa wake wa Nakhchivan, ambayo imetengwa kijiografia kutoka kwayo ... Armenia inaona makubaliano hayo kama fursa ya kupata ulinzi wa Marekani dhidi ya shambulio lolote linalowezekana kutoka kwa jirani yake Azabajani, huku Urusi ikishindwa kuisaidia katika vita vya hivi karibuni") ambapo Armenia ilishindwa na jamhuri yao ilianguka katika eneo la Karabakh, ambalo walilitangaza miaka 35 iliyopita kwa msaada wa Urusi hapo awali.

3- Tovuti ya Middle East Eye ilisema kwamba ("Azabajani inadai kwamba ukanda huo usiwe chini ya udhibiti kamili wa Armenia". Ilisema kwamba "Uturuki imeweka shinikizo fiche kwa Azabajani kusaini makubaliano ya amani na kwamba ndiyo iliyoanzisha wazo la kuanzisha kampuni binafsi kwa idhini ya nchi hizo mbili kusimamia ukanda huo"). Erdogan alimpokea Rais wa Azerbaijan Aliyev mnamo 2025/6/19, na siku iliyofuata alimpokea Waziri Mkuu wa Armenia Pashinyan, ambaye ziara yake ilichukuliwa kuwa ya kihistoria kwa Uturuki. Ofisi ya Rais wa Uturuki ilisema kwamba ("Erdogan alisisitiza "umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo ya amani yanayoendelea kati ya Azabajani na Armenia ... na kujadili hatua zinazowezekana ambazo zinaweza kuchukuliwa katika mfumo wa mchakato wa kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Uturuki na Armenia"... Al Jazeera 2025/6/21) Hivyo tunaona Erdogan amefanya maandalizi ya kusaini makubaliano hayo kwa niaba ya Amerika, kwani anazunguka katika mzunguko wa Amerika na kuipa huduma za kueneza ushawishi wake katika eneo hilo badala ya kumsaidia kubaki madarakani, na kwamba Uturuki inanufaika na harakati za kibiashara kupitia barabara kutoka Armenia hadi Azabajani.

4- Makubaliano hayo yalisema kwamba wao ("walielezea shukrani zao za dhati kwa Rais wa Marekani Trump kwa kuandaa mkutano wao na mchango mkubwa katika mchakato wa kurejesha uhusiano wa nchi mbili kati ya nchi hizo mbili"). Rais wa Marekani Trump alitaka kuonyesha jukumu la nchi yake na jukumu lake binafsi haswa kwa namna iliyo wazi, kwani anapenda kujitokeza na kuonekana na kurekodi kila mafanikio kwa jina lake, akidai kuwa ana uwezo wa kufikia amani na ustawi, hivyo barabara ambayo itajengwa kati ya Azabajani na mkoa wake wa Nakhchivan kupitia Armenia ilipewa jina lake (Barabara ya Trump). Kwa kufanya makubaliano haya kati ya nchi hizi mbili, Trump pia anatumai kupata Tuzo ya Nobel ya Amani, kwani aliteuliwa kwa ajili yake na Kamanda wa Jeshi la Pakistani Munir Asim, pamoja na Waziri Mkuu wa Kitengo cha Kiyahudi Netanyahu. Ikumbukwe kwamba amani na ustawi ambao Trump anadai kufanya kazi kuyafikia inamaanisha kufikia maslahi ya Marekani na kueneza ushawishi wake na utawala wake juu ya maeneo mbalimbali duniani na kurejesha ukuu wake, kwani alizindua kauli mbiu ya "Amerika Kwanza" na kauli mbiu ya "Ifanye Amerika kuwa Kubwa Tena (MAGA)".

5- Imesemwa katika makubaliano kwamba ("watu waliosaini makubaliano waliomba nchi zinazoshiriki katika Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulayana miundo inayohusiana na Minsk kukubali uamuzi huo"). Hiyo ni, Trump analazimisha nchi nyingine katika kundi la Minsk kukubali uamuzi huu wa Marekani bila kushiriki ndani yake na hata bila kushauriana nao, na bila kuwapa thamani au umakini wowote. Hasa Urusi na Ufaransa, ambazo zinashiriki na Marekani katika uongozi wa kundi la Minsk, ambalo liliundwa kutatua tatizo la Azeri-Armenia mwaka 1992 kwa uamuzi wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya!Marekani ilisaini makubaliano haya tofauti na Urusi, na ilifanya muda wake kuwa kabla ya mkutano wa rais wake Trump na mwenzake wa Urusi Putin ili kusiwe na pingamizi kutoka Urusi, ambayo lazima iwepo katika mada hiyo kwani ina ushawishi katika eneo hilo, haswa nchini Armenia baada ya kupoteza ushawishi wake nchini Azabajani, na kwa kuwa ni miongoni mwa viongozi wa kundi la Minsk. Aliomba kutoka kwake, kama alivyoomba kutoka kwa wengine katika kundi, kutambua makubaliano haya na kuyaunga mkono... Na badala ya Urusi kuingilia kati na kupinga, haikufanya hivyo, jambo ambalo linaonyesha udhaifu wa msimamo wake na udhaifu wa ushawishi wake, ambao uko karibu kutoweka nchini Armenia.

6- Inaonekana kwamba Urusi haiko katika nafasi inayoiwezesha kuingilia kati na kupinga kwa nguvu na kisha kuishawishi Armenia kuizuia kuendelea kuimarisha uhusiano wake na Marekani. Na ilipendelea kwenda sambamba na hali hiyo, kana kwamba inaridhika na kile kinachoendelea, huku ikituma onyo kwa Armenia ili isimpoteze kabisa. Alisema kupitia msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova: ("Mkutano wa jamhuri hizo mbili zilizoko kusini mwa Caucasus kwa msaada wa upande wa Marekani unastahili tathmini chanya. Tunatumai kwamba hatua hii itasonga mbele ajenda ya amani...") Lakini alisisitiza "haja ya kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja bila msaada wa nje" na alionya kwamba "ushiriki wa wahusika kutoka nje ya eneo hilo lazima uchangie kuimarisha ajenda ya amani na si kusababisha matatizo ya ziada"... Al Jazeera 2025/8/9). Hiyo ni, anaonya dhidi ya kuenea kwa ushawishi wa Marekani huko. Na alikuwa ameionya Armenia katika tarehe ya awali dhidi ya kushirikiana na Magharibi, hivyo msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema mnamo 2025/7/24 kwamba ("wakati Armenia ina haki ya kuchagua mwelekeo wake wa kisiasa, Moscow inatumai kuepuka kurudia mabadiliko ya kijiografia ambayo yalishuhudiwa na Ukraine" na alisisitiza kwamba "Urusi bado inachukulia Armenia kuwa mshirika na inataka kuendelea kushirikiana pamoja"... Al Jazeera 2025/7/25) Na hilo ni tishio kwa Armenia kwamba itakumbana na hatima ya Ukraine wakati Urusi ilipoteza ushawishi wake ndani yake baada ya kuanguka kwa mteja wake Yanukovych mnamo 2014 baada ya Amerika na Ulaya kuwashawishi Waukraine na kuwasha moto mapinduzi dhidi yake. Waziri Mkuu wa Armenia Pashinyan alitangaza mwaka jana katika mahojiano na kituo cha France 24 mnamo 2023/2/23 ("kusitisha ushiriki wa kivitendo wa Armenia katika Shirika la Mkataba wa Usalama wa Pamoja linaloongozwa na Urusi ... kwa sababu halijafikia malengo yake kuhusiana na Armenia") kwani Urusi haikuilinda Armenia wakati iliposhambuliwa na Azabajani katika miaka ya 2020 na 2023 na kuitoa kutoka katika ardhi iliyokuwa inaikalia nchini Azabajani.Tulikuwa tumetajakatika jibu tulilolitoa mnamo 2023/10/4 kwamba ("Urusi pengine imetambua kwamba vita hivi vinalenga dhidi yake na vimepangwa na Marekani kupitia Uturuki ya Erdogan na Azabajani, ambayo imekuwa msimamizi wake, na vitaiviwisha bila faida na kutawanya nguvu zake, na sasa inazingatia vita vyake nchini Ukraine, ambayo ni vita vya hatima na haitaki kuipoteza, na inajua kwamba ikiipoteza itapoteza kila kitu na ikiishinda itaweza kurejesha ushawishi wake katika maeneo ambayo ilipoteza. Wakati huo huo, haitaki kugongana na Uturuki na inaihitaji katika hali hizi na mzingiro uliowekwa juu yake, na ni lango lake kwa ulimwengu wa Magharibi, na pia inataka kudumisha uhusiano wake na Azabajani, kwani ina uwekezaji huko, hasa katika rasilimali za nishati zenye thamani ya dola bilioni 6, na kiwango cha biashara kati yao ni zaidi ya dola bilioni 4. Na Armenia ni mzigo juu yake katika kila kitu... Na haiepukiki kwamba itairejesha kwa ushawishi wake kamili kama ilivyokuwa ikiwa itashinda vita nchini Ukraine").

7- Marekani ilipuuza Ulaya, hasa Ufaransa, ambayo inaongoza kundi la Minsk pamoja nayo, ili Trump aiangushe Ulaya, hasa Ufaransa, kama ilivyoangusha Urusi kutoka kwa mlinganyo na kujitenga katika suala hilo, bali Azabajani na Armenia zilituma ujumbe wa pamoja wa kuvunja kundi la Minsk, hivyo ilikuja katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Azabajani mnamo 2025/8/11 kwamba ("Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo mbili walituma ujumbe wa pamoja kwa Rais wa sasa wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya kumaliza kundi la Minsk", "Na baada ya ombi hili, rasimu ya azimio la kumaliza mchakato wa Minsk na miundo inayohusiana kati ya nchi zinazoshiriki katika shirika ilisambazwa" na "Azabajani na Armenia ziliomba kuunga mkono hatua zinazohitajika kuchukua uamuzi huu"... Shirika la Habari la Serikali la Azabajani 2025/8/11). Kwa hivyo Marekani inaangusha ushawishi wowote wa Ulaya katika suala hili ili kujitenga nayo na kuweza kueneza ushawishi wake ndani yake. Na nchi hizo mbili zimeanza kutekeleza makubaliano hayo haraka, ikiwa ni pamoja na ("kuondoa madai yote na mizozo ya pande zote mbili katika ngazi ya kimataifa kama ilivyoelezwa katika makubaliano"... Chanzo hicho hicho) Na Ufaransa ililazimika kutangaza kukubalika kwake kwa kuvunjwa kwa kundi la Minsk na haikuwa na jukumu au ushawishi wowote tangu 2020 baada ya Azabajani kutangaza vita dhidi ya Armenia na kisha kurejesha ardhi yake ambayo kundi la Minsk halikuisaidia kuirejesha kama kundi hilo lilivyodai kwamba linafanya kazi katika hilo kwa njia za amani. Na Ufaransa imekuwa ikimshukuru Marekani ili isionekane kwamba imepoteza na inatafuta jukumu la kucheza huko, hivyo ilidai kwamba inaunga mkono makubaliano hayo, ambayo ilikuwa ikiunga mkono Waarmenia kwa njia ya wazi dhidi ya Azabajani...

8- Vile vile, Trump alimpotezea Uturuki, ambayo ilikuwa ikingoja Rais wake Erdogan alipwe thawabu kwa huduma zake kwake kwa kumwalika Washington kuhudhuria kutiwa saini kwa makubaliano hayo, yeye ambaye alichukua jukumu muhimu katika kuunga mkono Azabajani na kuiwezesha kushinda Armenia na kukomboa ardhi zake zilizokaliwa kutoka kwake kwa mipango ya Marekani... Lakini hata hili Trump alimnyima, kwani hakuona haja ndani yake ya kukamilisha mkataba huu, vinginevyo angalimwita Washington, au kumwomba azungumze kwa njia ya simu na Rais wa Azerbaijan Aliyev, kama alivyoomba kutoka kwake azungumze na Rais wa Syria Ahmed Al-Shara kwa njia ya simu wakati wa mkutano wake naye huko Riyadh mnamo 2025/5/13 ili atekeleze maombi ya Marekani. Lakini katika makubaliano ya Armenia na Azabajani, alimpotezea! Hivyo ndivyo makafiri wakoloni wanavyovuna matunda na wengine wanaozunguka katika mzunguko wao au mawakala wanalima na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili yao badala ya ujira wa kubaki kwao madarakani, na hata hii si mara zote... Je, hawafikiri?!

9- Trump ana hamu ya kuonyesha ukuu wa Marekani na ukuu wake binafsi, na kwamba yeye ndiye mtu pekee duniani ambaye anaweza kuleta amani na kukamilisha kazi ngumu, na kuzindua vita vya kiuchumi dhidi ya maadui na marafiki, na kuwasha moto vita vya umwagaji damu moja kwa moja au kupitia kitengo cha Kiyahudi, kama alivyofanya hivi karibuni nchini Iran.. Anakiunga mkono kitengo cha Kiyahudi kwa njia ya wazi kuwaua watu wa Gaza, kuwanyima chakula na kuwahamisha bila haya wala hofu ili kufikia mradi wake wa kuigeuza kuwa mapumziko na bila mtu yeyote kuweza kuingilia kati kukomesha mauaji ndani yake au kuingiza kipande cha mkate kwa njia salama! Na amesahau kwamba Mungu alikuwa amewaangamiza kabla yake kutoka kwa vizazi ambao walikuwa na nguvu zaidi "kuliko yeye na nchi yake Marekani na kuliko kituo chake cha Kiyahudi" kwa nguvu na walikuwa na makusanyo na mauaji zaidi, na amesahau au amepuuza kwamba umma wa Kiislamu, haijalishi wamepatwa na ukandamizaji, dhuluma na dhuluma kutoka kwa watawala wao, marafiki wa makafiri, watainuka na kuasi dhidi yao, watawaangusha na kukabidhi mamlaka yao kwa yule anayestahili kutoka kwao ili awatawale kwa kile ambacho Mungu amekiteremsha, ili aanzishe tena Ukhalifa wa Rashid baada ya utawala huu wa kulazimisha ambao tunaishi ndani yake, uthibitisho wa bishara ya Mtume wa Mungu ﷺ katika Hadith yake tukufu iliyotolewa na Ahmad kutoka kwa Hudhaifa, alisema Mtume wa Mungu ﷺ «... Kisha kunakuwa na ufalme wa kulazimisha, kisha inakuwa vile Mungu anataka iwe, kisha anainyanyua anapotaka kuinua, kisha kunakuwa na ukhalifa juu ya mfumo wa unabii. Kisha akanyamaza» Na inabeba ujumbe wake kwa ulimwengu na kuenea ndani yake kama ilivyokuja katika Hadith tukufu iliyotolewa na Ahmad kutoka kwa Tamim al-Dari, alisema namsikia Mtume wa Mungu ﷺ akisema: «Hakika jambo hili litafika kule usiku na mchana vilipofika, na Mungu hataacha nyumba ya udongo wala ya manyoya isipokuwa Mungu ataingiza dini hii ndani yake, kwa heshima ya mheshimiwa au kwa udhalili wa mnyonge; heshima ambayo Mungu anaiheshimu Uislamu, na udhalili ambao Mungu anaudhalilisha ukafiri» Na hakika hilo litakuwa kwa idhini ya Mungu ﴿HAKIKA MUNGU NI MTENDAJI WA AMRI YAKE, MUNGU AMEKWISHAJAALIA KWA KILA KITU KIWANGO﴾.

Katika siku ya ishirini na mbili ya Safar Al-Khair 1447 Hijria

2025/8/16 Miladia

More from Maswali na Majibu