Mkutano wa Watawala Kibaraka Ni Dalili ya Usaliti Mpya
Habari:
Iran inazitaka nchi zilizopo katika nchi za Waislamu kuunda kituo cha pamoja cha operesheni kukabiliana na chombo cha Kiyahudi, na inasema lazima tuchukue maamuzi madhubuti ya kukomesha mauaji ya Wapalestina.
Maoni:
Uislamu unawalazimisha Waislamu kuwa na dola moja na mtawala mmoja ulimwenguni kote. Kwa hivyo, kwa uwazi kamili, tunasema: kwamba kuwepo kwa nchi nyingi katika nchi yetu ya Kiislamu ni jambo lililoharamishwa, hata kama nchi hizi zinaongozwa na Uislamu. Vipi ikiwa wanatawala kwa ukafiri wa wazi?! Ni usaliti kwa Mungu, Mtume wake, rehema na amani zimshukie, na kwa Waislamu ambao wanatamani umoja baada ya unyonge huu, utengano, na uvamizi wa mataifa makubwa juu yao.
Tunatambua na tunajua kwa yakini kwamba watawala wa nchi yetu ya Kiislamu hawakufika madarakani kupitia umma, lakini waliteuliwa na Magharibi kafiri mkoloni juu ya shingo zetu, na inafanya kazi nao kwa bidii ili kuweka nchi yetu chini ya udhibiti wao, kunyakua rasilimali zake, na kuhakikisha kutofanya kazi kwake katika operesheni yoyote ya mabadiliko.
Basi, vipi wito wa kuunda kituo cha pamoja cha operesheni kutoka kwa nchi hizi na watawala wake wasaliti, kukabiliana na chombo cha Kiyahudi ili kusimamisha mauaji yake kwa watu wetu huko Palestina na nchi zingine za Waislamu?! Ni kama mtu anavyoomba mbwa mwitu kuwa mlinzi wa kundi!
Vipi msaliti na kibaraka anaweza kuombwa kuwa huru na kufanya kile ambacho Bwana wa walimwengu anataka, wakati anachukulia Magharibi kafiri mkoloni, na Amerika akiwa kiongozi wao, kama bwana anayetiiwa?!
Kwa kifupi na kwa uwazi tunasema: Kuwepo tu kwa nchi hizi nyingi katika nchi yetu ya Kiislamu ni janga ambalo umma umeona hatari yake siku hizi waziwazi, na umetambua kwamba lazima uwe na dola moja yenye nguvu na tukufu inayotawaliwa na sheria za Uislamu katika siasa, uchumi, jamii, fedha, kilimo, viwanda, elimu, malezi, tiba, afya, mazingira, sayansi na masuala yote ya maisha.
Kwa hivyo, mkutano wowote unaofanyika kwa watawala wetu wasaliti siku hizi, haswa, ni kitendo ambacho kinatangaza usaliti na njama mpya dhidi ya umma kutoka Amerika, Magharibi, na mtoto wao mpendwa, chombo cha Kiyahudi.
Suluhisho halitakuwa katika mikutano ambayo matokeo yake yanajulikana mapema, lakini suluhisho bora, la kweli na linalowezekana litakuwa tu ikiwa umma utachukua uamuzi wake leo kabla ya kesho kwa kumpa ahadi khalifa mmoja ambaye atawatawala kwa Uislamu safi, na kuwaondoa watu wetu, sio Palestina tu, bali katika nchi zote za Waislamu, huzuni, dhiki, mauaji, uhamisho, na unyonge.
Ndiyo, nchi yetu itarudi kuwa nchi moja, na dola moja tukufu kwa Uislamu kama Mungu Mwenyezi na Mtume wake, rehema na amani zimshukie, walivyoamuru ﴿Na utukufu ni wa Mwenyezi Mungu, na wa Mtume wake, na wa Waumini, lakini wanafiki hawajui﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya ofisi ya habari kuu ya Hizb ut-Tahrir
Dkt. Muhammad Jaber
Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut-Tahrir katika jimbo la Lebanon