Warohingya ni sehemu ya Umma bora
Warohingya ni sehemu ya Umma bora

Habari:

0:00 0:00
Speed:
November 17, 2025

Warohingya ni sehemu ya Umma bora

Warohingya ni sehemu ya Umma bora

Habari:

Mamlaka za Malaysia zilitangaza operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji, ikihusisha majeshi ya wanamaji, walinzi wa pwani, polisi, na ulinzi wa raia, na baada ya takriban wiki moja tangu kuanza kwa operesheni hiyo, idadi ya walionusurika ilisimama kwa watu 14, na takriban watu 30 walipatikana wakiwa wamefariki majini, na hatima ya waliosalia katika mashua iliyoanguka haijulikani, au hatima ya meli mama ambayo inaaminika ilikuwa imebeba abiria takriban 230.

Serikali ya Malaysia ililaumu magenge ya uhalifu yaliyopangwa na wasafirishaji haramu wa binadamu kwa janga hilo, ambao Waziri wa Mambo ya Ndani wa Malaysia, Saifuddin Nasution, aliwatuhumu kwa kuwatumia vibaya wanyonge, maskini na walioathirika ili kujipatia faida za kifedha kwa gharama ya maisha ya watu waliokata tamaa, kwa kuandaa safari haramu za baharini ambazo hazina hatua za chini za usalama.

Maoni:

Zaidi ya miaka kumi na tatu na mashambulizi ya Wabuddha wenye chuki dhidi ya Waislamu hayajaacha, kwani utawala wa Myanmar unaendelea kuongeza kiwango cha mateso na dhuluma dhidi ya Waislamu wa Rohingya, na umeweka sera kali na vizuizi vya kutisha dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwazuia uhuru wa kusafiri kati ya vijiji vyao, na kuwanyima haki za msingi kama vile kazi, chakula, elimu na huduma ya afya. Kwa sababu hizi na hali ngumu, Warohingya waliamua kuhamia baharini kwenye boti chakavu na zilizojaa watu katika safari hatari wakitumaini kupata makazi na maisha mapya katika nchi zenye Waislamu wengi kama vile Malaysia, Indonesia na Bangladesh.

Boti zinazoitwa boti za mauti, ambazo licha ya hatari yake, zinawakilisha kimbilio pekee kwa Waislamu wa Rohingya katika kukabiliana na ukiukwaji wa kibinadamu na operesheni za utakaso wa kikabila. Na ni aibu kubwa kuona majeshi ya Malaysia yakifanya kazi ya kuopoa maiti baada ya bahari kuzimeza na mawimbi kuzitupa badala ya kuwatetea wakiwa hai na kuondoa dhuluma kutoka kwao na kuwalinda dhidi ya jeshi la Burma!! Mko wapi na kauli ya Mwenyezi Mungu: ﴿NA WAKIOMBA MSAADA KWENYE DINI, BASI JUU YENU NI KUWASAIDIA﴾?! Kuwaacha ndugu zenu huku wanachomwa moto na kuangamizwa mbele ya macho yenu ni aibu ya dunia na adhabu ya akhera, mtamwambia nini Mola wenu atakapowauliza kuhusu wanawake Waislamu ambao heshima zao zinakiukwa huko Myanmar? Hamuamki kuwasaidia ndugu zenu wanaodhulumiwa?!

Ewe Mola, tumefikisha, Ewe Mola, shuhudia, Ewe Mola, shuhudia

Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

Rana Mustafa

More from Sauti na Video