Hali, Damu na Rasilimali za Waislamu Zimehalalishwa Mbele ya Maadui Zao, Suluhisho Liko Wapi?
Habari:
Jeshi la taasisi haramu ya Kiyahudi limetangaza kuvuka kwa mamia ya Wadrusi kuingia ardhi ya Syria na kupenya uzio wa mpaka katika eneo la Majdal Shams, katika mabadiliko yasiyo ya kawaida katika eneo hilo ambalo linajumuisha vijiji vya Wadrusi pande zote mbili za mpaka. (Al Jazeera Net)
Maoni:
Idadi ya Wadrusi nchini Syria leo inakadiriwa kuwa watu 700,000, wanaoishi katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Suwayda na Golan, na wanachukuliwa kuwa miongoni mwa makabila madogo yanayoishi Syria. Idadi yao katika Palestina inayokaliwa inakadiriwa kuwa watu 150,000, na kutokana na matukio ya hivi karibuni, wameungana na kuvunja mipaka ya Sykes-Picot kuunga mkono kila mmoja. Wakati umma wa mabilioni ya watu umefungwa na mipaka hii mibaya licha ya kilio na ombi la msaada kutoka kwa watu wa Gaza waliojeruhiwa, ambao wamegeuka kuwa makaburi yaliyotawanyika kila mahali!
Matatizo na majanga yamefanya watu waulize, umma wa mabilioni uko wapi?! Je, nguvu ya kimataifa dhalimu imekuwa na nguvu zaidi kuliko nguvu ya itikadi ya Kiislamu? Na nini sababu ya ulemavu huu? Na suluhisho ni nini?
Ulemavu wa kushangaza wa umma leo kukabiliana na maadui wa Uislamu na kusimamisha mauaji na aina mbalimbali za ukatili sio kwa sababu ya udhaifu au kasoro katika itikadi ya Kiislamu, na sio kwa sababu ya ukosefu wa dini katika mioyo ya Waislamu au uoga na unyonge, lakini ni kwa sababu umma huu mtukufu hauna dhana halisi na wazi ya jinsi ya kutoka katika hali hii chungu, kwani unajiona umefungwa na hauwezi kusonga mbele ya nguvu za kimwili za maadui zake!
Umma unahitaji watu wa dola kama vile Makhalifa Warashidi katika dola inayosimamia masuala ya watu na kuwajibika kwao kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, ili kuweka mipango na ufumbuzi wa kivitendo wa moja kwa moja kwa matatizo na majanga, na kujibu hila za washirika wenye chuki, kuwatisha maadui wa Mungu na kurejesha hadhi iliyopotea tena, na bila ya hayo hali yetu haitabadilika na mambo yetu hayatabadilika.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Rana Mustafa