Kutoweka kwa Wamisri kwa Nguvu Baada ya Kuwataka Usalama Kukataa Kuzingirwa kwa Gaza
(Imetafsiriwa)
Habari:
Vijana wawili walitoweka baada ya video yao kuenea wakiivamia idara ya polisi ya usalama wa taifa katika kituo cha polisi cha Al-Maasara huko Helwan, kusini mwa Cairo, ambapo waliwaweka maafisa wa usalama katika seli. Nia ya hatua hii ilikuwa ni kulalamikia uzembe wa maafisa katika kuwasaidia watu wa Gaza. (Middle East Eye)
Maoni:
Katika video iliyochapishwa kwenye Telegram, vijana wawili, Mohsen Mustafa (27) na binamu yake Ahmed Sharif Ahmed Abdel Wahab (23), wanaonekana wakiivamia kituo cha polisi na kuwazuilia maafisa wa usalama katika seli. Watu hao wawili walikuwa wakiwaambia maafisa kwamba ikiwa wataombwa kuwakamata waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa ajili ya watu wa Gaza, watawakamata, wakisema: "Wao [watawala] wanawatumia kwa sababu hamkatai amri. Hamkatai amri kamwe! Hamtumii akili zenu." Waliendelea na maandamano yao wakisema: "Ndugu na dada zetu huko Gaza, na tunataka kufungua kivuko. Tunapaswa kufanya nini?" (Jukwaa la X)
Ushujaa huu, katika kukabiliana na mfumo, uso kwa uso ni ushujaa wa kweli! Kusema Mtume ﷺ: «Msaidie ndugu yako, awe dhalimu au madhulumu» Wakasema: Ewe Mtume wa Mungu, huyu tunamsaidia akiwa madhulumu, lakini tutamsaidiaje akiwa dhalimu? Akasema: «Mshike juu ya mikono yake».
Wamewatetea kaka na dada zao wanaodhulumiwa usiku na mchana. Walifanya wawezavyo kuwazuia maafisa wa utawala kushiriki katika ukandamizaji. Waliwahoji na kuwasikiliza, bila kuogopa matokeo yoyote ya matendo yao. Waliamka wakitambua kuwa mfumo wanaokabiliana nao unajulikana kwa kutesa na kuua yeyote anayetoka nje ya mstari. Lakini hilo halikuwazuia kufanya kila wawezalo kwa ajili ya ndugu zao. Tunamuomba Mungu akubali matendo yao, na msimamo huu uwe chanzo cha nuru siku ushuhuda utakaposimama.
Enyi Maafisa waaminifu katika Kinana: Tunajua kwamba kuna maafisa waaminifu miongoni mwenu, mliojiunga na jeshi au vikosi vya usalama kutekeleza wajibu wenu kwa Mungu. Tunajua hamtaki kuwa wadhalimu! Tafakari maneno ya Mohsen na Ahmed! Mnatumiwa kutumikia ajenda fulani. Nyinyi ni chombo tu kinachotumiwa na makafiri na mfumo wa wasaliti kutekeleza ajenda ya Magharibi, tumieni akili zenu, fikirieni na jiulizeni, itakapofika siku ambayo mashahidi wote watasimama kutoa ushahidi mbele ya Mwenyezi Mungu, msimamo wenu utakuwa upi? Mtawajibuje Muumba wenu atakapowauliza mlichowafanyia ndugu zenu walioketi upande wa pili wa mipaka bandia, ambao wanakufa kwa njaa?! Wakati ambapo hamwezi tu kuleta misaada, lakini pia mnaweza kukomboa Gaza na Palestina yote! Simameni imara dhidi ya mifumo hii, msichukue amri kutoka kwao, bali kutoka kwa yule atakayetekeleza hukumu za Mwenyezi Mungu, Khalifa.
Enyi Maafisa waaminifu: Semeni imetosha... fanyeni aina tukufu zaidi ya jihad na simameni imara dhidi ya mifumo! Mtume ﷺ alisema: «Jihadi bora ni neno la haki mbele ya Sultan dhalimu».
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya ofisi ya habari kuu ya Hizb ut-Tahrir
Khadija Hafeez