Ni lazima Erdoğan aelekeze hotuba yake kwa Umma Mtiifu na sio kwa walinzi wa Sykes-Picot
kwa ajili ya umoja na udugu wa Kiislamu!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Katika hotuba yake mbele ya Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu huko Istanbul, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan alitoa wito wa umoja zaidi na udugu kati ya nchi za Kiislamu. Erdoğan pia alisema: "Hatutaruhusu kuanzishwa kwa mfumo mpya wa Sykes-Picot katika eneo letu, ambao mipaka yake imechorwa kwa damu." Alisisitiza tena kwamba suluhisho liko katika "diplomasia na mazungumzo."
Maoni:
Ni umoja na udugu gani ambao Erdoğan anatoa wito? Na anatarajiaje kuimarisha umoja huu?
Msisitizo wa Erdoğan juu ya "suluhisho kupitia diplomasia na mazungumzo" ni usemi tu wa hamu yake ya kudumisha "mfumo wa Sykes-Picot" uliopo.
Vikwazo vya umoja na udugu katika Uislamu kwa hakika ni mipaka ya Sykes-Picot iliyochorwa kwa damu, na mataifa ya kitaifa yaliyoanzishwa ndani ya mipaka hii, na tawala vibaraka za Magharibi ambazo zinalinda mataifa haya. Haiwezekani kujenga umoja na udugu wa Kiislamu kupitia kuzungumzia utaifa, au mipaka ya taifa la kitaifa, au kulinda mipaka ya Uturuki, Iran, Palestina, Syria, na zinginezo, na sio kupitia kukandamiza umoja wa Waislamu katika imani chini ya utambulisho wa kitaifa. Palestina, na Gaza haswa, ni ushahidi wazi wa hilo. Kwa mipaka yake iliyochorwa chini ya Sykes-Picot, vikwazo vya Lausanne, katiba yake iliyonakiliwa kutoka Magharibi, sera zake za ndani na nje zinazoamriwa na makubaliano ya kimataifa, na kuwa nchi ya kwanza ya Kiislamu kutambua mnyama wa Kizayuni kama serikali halali ili kuwafurahisha mabwana zake wa Magharibi, je, Jamhuri ya Uturuki haiwakilishi ushahidi wazi zaidi wa usaliti wa udugu?
Erdoğan amechangia nini katika kuimarisha udugu wa Kiislamu tangu alipochukua wadhifa wa Waziri Mkuu nchini Uturuki mwaka 2003 na kisha Urais mwaka 2014?
Tuache usaliti wake huko Misri na Syria kwa sasa... Tangu "Dakika moja!" maarufu na "Jerusalem ni mstari wetu mwekundu," alisaliti mashahidi wa meli ya Mavi Marmara, na akaongeza mara dufu kiwango cha biashara ya Uturuki na entiteti ya Kiyahudi mara nyingi zaidi. Wakati alikuwa akitamka maneno mengi yanayoumiza moyo kuhusu Gaza, alikuwa akitimiza mahitaji yote ya "Nazi," kama anavyoiita entiteti ya kigaidi ya Kiyahudi, na kuipatia petroli, chuma, buti za kijeshi, vifaa vyeupe, na chakula... Na wakati alikuwa akipitisha matatizo ya Waislamu kwa watengenezaji wa Sykes-Picot, ambao wanaivunja Umma vipande vipande...
Kwa kweli, Erdoğan, ambaye anafanya kazi kama afisa mkuu mtendaji wa taasisi hii ya Sykes-Picot - au tuseme "kampuni ya huduma kwa Uzayuni" - hakufanya chochote kwa ajili ya wahudumu wa afya wa Gaza ambao walichomwa wakiwa hai, madaktari wake ambao wanateswa katika seli za Kizayuni, mama zake ambao wanafanyiwa upasuaji wa Kaisaria bila ganzi, watoto wake ambao viungo vyao vinakatwa bila ganzi, na watoto wake wenye njaa ambao wanachomwa wakiwa hai. Hii, licha ya kuwa na jeshi la tisa lenye nguvu zaidi ulimwenguni na jeshi la nne lenye nguvu zaidi katika NATO... Na licha ya kuwa na shemeji ambaye anazalisha ndege zisizo na rubani za hivi karibuni ulimwenguni, na ndege za kivita za hali ya juu... lakini anarudia kama kasuku kanuni za watetezi wa Sykes-Picot - akisisitiza kwamba suluhisho "liko katika diplomasia na mazungumzo" na "suluhisho la mataifa mawili"!
Kwa kifupi: Dhana ya Erdoğan ya udugu sio udugu wa Kiislamu! Wito wake wa umoja wa Kiislamu sio katika umoja ambao Mtume Muhammad ﷺ aliuonyesha. Watu ambao Erdoğan anazungumza nao kwa wito wake wa umoja ni watu duni wanaotafuta kukandamiza neno la kweli kwa Waislamu, na ambao wanasimama kama vizuizi mbele ya heshima ya Umma. Ikiwa entiteti ya Kiyahudi ambayo inafanya mauaji ya kimbari na ambayo inatambua kuwa kumwaga damu ya Waislamu huko Palestina na damu ya watoto wa Gaza na mtu mwingine yeyote ndio lengo lake pekee la kuwepo, bado ipo na inaongezeka ukatili kwa ujasiri unaoongezeka, basi sababu ni wazi: Ni kwa sababu ya Erdoğan, ambaye, kama vile watawala wa Kiarabu, anatafuta mamlaka na heshima katika mifumo ya kibepari sio katika Uislamu, na ambaye anaegemea upande wa marafiki zake makafiri badala ya kuwa katika safu za Umma.
Ikiwa Erdoğan anataka umoja wa Kiislamu, kuna mamilioni ya Waislamu ambao wameungana kwa ajili ya Gaza, wanasubiri amri moja itoke kinywani mwake. Ikiwa Erdoğan anataka udugu wa Kiislamu, kuna mamilioni ya Waislamu ambao wanaumia kwa ajili ya ndugu zao, na ambao wanatamani kuwa askari katika jeshi, wanaanza kulingana na amri yake.
Laiti Erdoğan angekuwa mwaminifu, angezungumza na Waislamu watiifu na sio walinzi wa Sykes-Picot. Na kama angekuwa hivyo, angependekeza umoja chini ya kivuli cha Qur'ani na Sunna na sio diplomasia ya kibepari kama suluhisho!
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Zahra Malik