Kila nafsi hulipwa kwa matendo yake!
Habari:
Vita kati ya Iran na Taifa la Kiyahudi
Maoni:
Ni nadra kutokea vita kati ya nchi mbili zilizo mbali na zisizo na mipaka baina yao, na kwa teknolojia ya kisasa vita vimezuka kati ya Iran na Taifa la Kiyahudi, kupitia makombora na ndege, na vita hivi vimesababisha uharibifu hasa nchini Iran baada ya Magharibi kuliunga mkono Taifa la Kiyahudi na Marekani kuingia vitani upande wake kwa ndege na kulipua mitambo ya nyuklia ya Iran. Hapa ni lazima tusimame na kukumbuka uhaini au uachaji wa Iran kwa wapiganaji wa jihadi huko Gaza.
Iran ambayo ilianzisha mfumo wake baada ya mapinduzi ya Khomeini juu ya magofu ya utawala wa Shah na imekita mapigano dhidi ya Taifa la Kiyahudi na kukabiliana nalo na kufanya miongoni mwa itikadi zake kuwa "Mauti kwa Israeli" na kufanya kazi ya kuliondoa, na ilitumia mgogoro kati ya Waislamu na Wayahudi kwa hivyo ikaanzisha na kuunga mkono upinzani dhidi ya Taifa la Kiyahudi, na makubaliano ya hivi karibuni au ahadi ambazo zilifikiliwa kati ya Iran na wafuasi wake kutoka kwa wapinzani iwe harakati ya Jihad au harakati ya Hamas au chama cha Iran na wengine na wakafikia ahadi kati yao yenye kichwa "Umoja wa Viwanja," na Hamas ilipoingia katika mapambano na Taifa la Kiyahudi mnamo tarehe saba Oktoba 2023 na kulidhalilisha na kuteka mateka makumi na kuua mamia ya vibaraka wake, ilikuwa inatakiwa kwa Iran na wafuasi wake kutekeleza ahadi ya umoja wa viwanja iliyopo kati yao, kwa maana kwamba ikiwa mmoja wao atapigana vita na Taifa la Kiyahudi basi wote watasimama upande wake, lakini waliitelekeza Gaza, na lau wangeliiunga mkono ingeweza kuondoa Taifa la Kiyahudi, kwa hivyo lau ingezindua makombora ambayo yanailipua leo, na ikaamuru chama chake na wafuasi wake huko Yemen na Iraq kulipua Taifa la Kiyahudi na kulivamia kutoka upande wa Lebanon kaskazini mwa Palestina wangekutana na wapiganaji wa jihadi huko Tel Aviv na Taifa hilo lingemalizwa, lakini Iran ilikinyamazisha chama chake huko Lebanon na kuizuia kuingilia kati, na ilibuni wazo la kuisaidia Gaza, yote hayo ili kumridhisha Amerika ili isikasirike, kwa hivyo ilizuia kusaidia na kuunga mkono watu wa Gaza na kuiacha na kuwatelekeza watu wake; matokeo yalikuwa nini?! Taifa la Kiyahudi lilimdhuru chama cha Iran na kumwangamiza, kisha likawaua makumi ya viongozi wa Iran na likamalizia kwa kuipiga Iran yenyewe na kuidhili na kuua makumi ya viongozi wake na kuharibu makumi ya taasisi zake ikiwa ni pamoja na maghala ya makombora na vituo vya utengenezaji wake na mitambo ya nyuklia, basi huu ulikuwa ndio malipo ya kile ilichokifanya yenyewe, na zamani ilisemwa "Kila nafsi hulipwa kwa matendo yake!"
Iran ilijitahidi kuendana na Magharibi na kuwapendeza ili wairidhike, matokeo yakawa imepoteza, kwanza, Mungu na Mtume wake na waumini, haswa ilipokabiliana na Waislamu kwa ukali huko Iraq na Sham na kuua mamia ya maelfu na kuwafukuza mamilioni ya Waislamu na kuzuia ushindi wa mapinduzi na kumuunga mkono dikteta wa Sham, kisha ikaanguka katika maovu ya matendo yake, na ushindi haukuweza kuja mikononi mwake na haikufanikiwa kupata ahadi ya Mungu, na matokeo yalikuwa kwamba ilionja ubaya wa amri yake kwa mauaji na uharibifu na kupoteza juhudi za miongo kadhaa, na jibu dhaifu kwa kulipuliwa kwa Amerika ni kuhifadhi heshima kidogo na kuwahadaa wajinga miongoni mwa wafuasi wake kwamba imefanya yale ambayo ilipaswa kufanya!
Katika suala hili hatuko katika maonyesho ya furaha bali ya kukumbusha kwamba yule anayeendana na maadui na kuwapendeza atampoteza Mungu na Mtume wake na waumini na kupoteza nguvu zake, na kwa hivyo amepoteza dunia na akhera, na yule aliye pamoja na Mungu, Mungu atamtukuza na kumshinda katika dunia na akhera.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Sheikh Dk. Muhammad Ibrahim
Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Lebanon