Aibu kubwa kwa watawala wa Waislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Katika mabadiliko ya hivi karibuni katika mkondo wa mauaji ya halaiki huko Palestina, nchi nyingi zinaelezea kuunga mkono Palestina, zikiwaacha nyuma taasisi ya Kiyahudi na watawala wake. Hivi karibuni, serikali ya Slovenia ilimtangaza Waziri Mkuu wa Kiyahudi Benjamin Netanyahu kuwa mtu asiyekubalika nchini humo, ikitaja vita vya mauaji ya halaiki alivyozindua huko Gaza. Slovenia, mwanachama wa Umoja wa Ulaya, ilitambua jimbo la Palestina mwaka 2024, na iliweka marufuku ya usambazaji wa silaha kwa taasisi ya Kiyahudi mnamo Agosti. Mnamo Novemba mwaka jana, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ilitoa hati ya kumkamata Netanyahu kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. (TRT)
Maoni:
Hakuna nchi yoyote ya Kiarabu iliyothubutu kufanya kitendo hiki cha mfano. Uturuki, Misri, Jordan, UAE, Bahrain na Morocco zina balozi za wazi za Wayahudi wavamizi katika nchi zao licha ya uharibifu mkubwa waliosababisha katika maisha na mali. Nchi zingine kama vile Saudi Arabia, Syria, Kuwait, Oman na Qatar zinadumisha mwonekano wa umbali, lakini matendo yao yanaonyesha kinyume chake. Nchi kama Bolivia na Nikaragua huko Amerika Kusini (ambazo zilielezea taasisi ya Kiyahudi kama ya kifashisti na ya mauaji ya halaiki) zimekata uhusiano wao na Wayahudi. Nchi zingine kama vile Colombia na Chile zimewaita mabalozi wao.
Kinyume chake, wakati makombora yanalenga taasisi ya Kiyahudi, nchi za Kiarabu ndizo za kwanza kukimbilia kuilinda. Inaonekana kwamba Jordan ilihisi kulazimika kusaidia mara mbili! Mnamo Oktoba 1, 2024 na Juni 2025, ambapo ilizuia makombora yaliyokuwa yanalenga, na sehemu zake zilianguka kote nchini kwa sababu hiyo (Amman, Al-Balqa, Zarqa, Madaba, Karak), na kusababisha uharibifu wa mali na kumjeruhi watu wengine.
Wakati huo huo, wakati Wayahudi wavamizi wanashambulia nchi za Kiarabu kwa ujasiri, hakuna msaada kutoka kwa nchi zingine za Kiislamu au hata majibu kutoka kwa aliye shambuliwa! Syria, Lebanon, Qatar na zingine zimelengwa bila kuadhibiwa.
Watawala wetu madikteta wanaunga mkono mauaji na njaa ya watu wote, na wanazuia msaada wowote kuwafikia kwa jina la kulinda sheria ya kimataifa isiyo na mashiko. Ni wanafiki na wadhalilishaji gani! Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: ﴿WANAYO MIOYO AMBAYO HAWAFAHAMU KWAYO, WANAYO MACHO AMBAYO HAWIONI KWAYO, NA WANAYO MASIKIO AMBAYO HAWASIKII KWAYO. HAO NI KAMA WA NYAMA WALIOFUGWA, BALI WAMEPOTEA ZAIDI﴾.
Nyuso mbaya za watawala wanafiki, vibaraka wa nchi za kikoloni za Magharibi, zimefichuliwa ili ulimwengu mzima uzione. Hatuna chaguo lingine isipokuwa kuanzisha Ukhalifa ambao utaunganisha sababu yetu na kutuma majeshi kukomboa Palestina iliyobarikiwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: "Hakika Imamu ni ngao, anapiganwa nyuma yake na kujikinga naye." Sahih Muslim
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Salim Muhammad