Tiba ya Matatizo Yanayoletwa na Mfumo wa Kibepari Ni Kutoka Nje Yake Tu
Habari:
Mwanachama wa muungano wa Al-Fatah, Mahmoud Al-Hayani, kwa kituo cha televisheni cha Rudaw: Mgogoro wa ukwasi unatishia mishahara ya wafanyakazi wa Iraq.
Maoni:
Mgogoro wa ukwasi wa fedha umeambatana na udhibiti wa mfumo wa kibepari ulimwenguni na kulazimisha thamani ya fedha kimataifa kwa msingi wa dola baada ya fedha kuwa dhahabu na fedha na kile kilicho chukua nafasi yao kama thamani yao halisi.
Upatikanaji wa fedha katika masoko huyaamsha na kuendesha gurudumu la maisha katika uhalisia, na hili ndilo ambalo jamii zetu zinakosa kwa sababu ya matibabu ambayo mifumo ya kibepari inafanya, ikiwa ni sahihi kusema hivyo, kwa sababu asili ya matibabu ni kutatua migogoro na sio kuizidisha zaidi na zaidi, na ikiwa Al-Hayani alidokeza katika mahojiano haya kwamba ukwasi hapa utaathiriwa na matukio ya kijeshi kati ya Iran na taasisi ya Kiyahudi kama tukio la nje na pia kile kinachotokea kutokana na mvutano kati ya kile kinachoitwa Mkoa wa Kurdistan na Baghdad kuhusu uuzaji wa mafuta na serikali ya mkoa kupata mapato yake katika bajeti ya shirikisho.
Kile ambacho Al-Hayani ametoa kama sababu sio sababu ya kweli ya migogoro, lakini ni matokeo ya tatizo moja, nalo ni kukubali shinikizo la Kimarekani, ambalo Al-Hayani alilifanya kama sababu inayoambatana na kile alichotoa kama sababu za mgogoro wa ukwasi unaowezekana katika siku zijazo.
Utiifu wa serikali ya Iraq kwa uvamizi wa Marekani na kukata rufaa kwa mfumo wa kibepari ndio sababu kuu, na pekee, ya shida zote zinazotokea kati yetu.
Na migogoro hii haitaisha hadi umma wa Kiislamu utakaporejesha mamlaka yake, kwa sababu mfumo wa kiuchumi, ambao ni sehemu muhimu ya mfumo jumuishi wa Kiislamu, umechukua hatua za kivitendo katika kutoa pesa kwa raia, pamoja na ugawaji wa mali na utoaji wa mahitaji ya msingi ya raia kutoka kwa chakula, bidhaa za mafuta na rasilimali zingine ambazo hutumikia hitaji la raia. Mtume, rehema na amani zimshukie, anasema: «Watu wanashirikiana katika vitu vitatu; Katika maji, malisho, na moto».
Mwenyezi Mungu amefanya mfumo huu wa Kiislamu kuwa msingi wa usalama na utulivu, kwani alisema, Mwenyezi Mungu Mtukufu: ﴿Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale walio kuwa kabla yao, na atawathibitishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Waniabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakao kufuru baada ya haya, basi hao ndio wapotofu﴾. Na akasema Subhaanahu: ﴿Ambao wameamini na nyoyo zao zikatulia kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia﴾.
Suluhisho la msingi la shida zinazokabili nchi ni kuondoa uvamizi wa Kimarekani na mfumo wa kibepari kutoka nchi yetu na kutekeleza sheria ya Mungu ya haki.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Wael Al-Sultan - Jimbo la Iraq