Chaguzi za Kidemokrasia Sio Chochote Ila Ni Vishawishi Vya Shetani
Chaguzi za Kidemokrasia Sio Chochote Ila Ni Vishawishi Vya Shetani

Habari:

0:00 0:00
Speed:
September 18, 2025

Chaguzi za Kidemokrasia Sio Chochote Ila Ni Vishawishi Vya Shetani

Chaguzi za Kidemokrasia Sio Chochote Ila Ni Vishawishi Vya Shetani

(Kimetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Septemba 13, 2025, kampeni ya uchaguzi wa rais ilizinduliwa rasmi Zanzibar, ambapo chama tawala, Chama Cha Mapinduzi, na chama cha upinzani, Alliance for Change and Transparency, walizindua kampeni zao. Chama Cha Mapinduzi kilisisitiza "utulivu", "amani" na "umoja", huku chama cha Alliance for Change and Transparency kiliweka kipaumbele uwajibikaji, usawa na fursa za kiuchumi.

Maoni:

Kipindi cha kampeni za uchaguzi nchini Tanzania kinaisha tarehe 28 Oktoba 2025, ambapo tarehe 27 Oktoba 2025 itakuwa siku ya kupiga kura kwa uchaguzi wa Zanzibar, huku siku ya Jumatano tarehe 29 Oktoba 2025 itakuwa siku ya kupiga kura kwa uchaguzi wa Tanzania, kulingana na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania. Hii ni uchaguzi wa tano wa vyama vingi tangu Tanzania ilipoamua kukumbatia demokrasia ya vyama vingi mwaka 1992. Uchaguzi wa mwaka huu ulionekana kufanana na chaguzi zilizopita, huku kukiwa na hali ya kutojali, kukabiliana na kususia, na kuwepo hisia za wasiwasi ambazo zilionekana kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki, kutokana na kutofanyika mageuzi ya uchaguzi.

Suala la demokrasia na kila kinachohusiana nayo, kama vile ushiriki na kuunga mkono kampeni za kidemokrasia na chaguzi zake, ni jambo lililo wazi katika Uislamu. Ambapo Uislamu unaharamisha kupiga kura kwa mfumo usio wa Kiislamu, na hairuhusiwi kuutekeleza au kuutoa wito. Kwa mtazamo mpana zaidi, haifai kutekeleza, kushiriki, kukumbatia au kutoa wito kwa mfumo wowote unaokhalifu Uislamu.

Sheria na hukumu katika Uislamu haziwezi kutolewa kutoka kwa mfumo wa kimanadamu, kama vile demokrasia, ambao ni mfumo wa kisiasa wa kibepari, bali lazima utoke kwa Mwenyezi Mungu pekee. Kwa hivyo, mfumo wowote wa kisiasa, kijamii au kiuchumi ambao haujajengwa juu ya sheria ya Kiislamu hauna nafasi katika Uislamu, na lazima ukataliwe. Kwa hakika, watu wa kawaida wanatambua, iwe Zanzibar, Tanzania, Afrika au ulimwenguni kote, kwamba demokrasia imewaangusha. Zaidi ya hayo, hakuna tofauti kati ya chama tawala na upinzani, vyama vyote vya siasa za kidemokrasia vinategemea misingi ileile ambayo itikadi ya kibepari ya kimagharibi ya kikoloni inategemea, ambayo inatokana na maslahi binafsi, unyonyaji na kutenganisha dini na maisha ya watu.

Nchi nyingi za Afrika zinaongozwa, isipokuwa nchi chache kama vile Tanzania, na kile ambacho hapo awali kiliitwa vyama vya upinzani, lakini hakuna kitu kilichopatikana ndani yake. Pamoja na hayo yote, Afrika inachukuliwa kuwa bara maskini zaidi licha ya kuwa na rasilimali nyingi za asili, ambazo zinachukuliwa bure na wakoloni wa Magharibi, kupitia ukoloni mamboleo, kupitia wanasiasa tunaowachagua mara kwa mara chini ya demokrasia!

Afrika na ulimwengu hauhitaji uchaguzi wa kilimwengu wa udanganyifu ambao hufanya kazi tu kwa ajenda ya kikoloni ya unyonyaji bila kuleta uamsho wowote wa kweli kwa watu.

Kanuni na mfumo mbadala wa kisiasa lazima utoke katika Uislamu. Chini ya Uislamu, ambao ni ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, uongozi wa kisiasa wa Kiislamu utaanzishwa barani Afrika, chini ya Khilafah ya kimataifa. Ndipo Afrika na ulimwengu utakapokombolewa kutoka kwa minyororo ya uovu na mfumo wa kisiasa wa kidemokrasia wa unyonyaji, na utashuhudia uongozi wa kweli na maendeleo ya haraka, kinyume na uharibifu, ucheleweshaji, umaskini uliokithiri na unyonyaji ambao uvamizi wa kikoloni ulileta mwishoni mwa karne ya kumi na tisa BK na hadi sasa.

Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir

Saeed Bitumwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Tanzania

More from null

Usitishaji Mapigano huko Gaza ni Pazia la Kuandaa Ukweli Mpya kwa Damu na Vifusi

Usitishaji Mapigano huko Gaza ni Pazia la Kuandaa Ukweli Mpya kwa Damu na Vifusi

Habari:

Uchunguzi wa Al Jazeera, unaotegemea uchambuzi wa picha za satelaiti, umefichua mifumo ya uharibifu wa kimfumo iliyofanywa na uvamizi huko Gaza kati ya Oktoba 10 na 30 iliyopita.

Shirika la "Sanad" la uhakiki wa habari la mtandao wa Al Jazeera limegundua operesheni za ulipuaji, ubomoaji wa kihandisi na mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na uvamizi ndani ya Ukanda huo tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano. (Al Jazeera Net)

Maoni:

Baada ya kutangazwa kwa usitishaji wa vita vilivyojaa mabomu dhidi ya Ukanda wa Gaza chini ya usimamizi wa Trump na kwa makubaliano na baadhi ya nchi za Kiarabu, ilikuwa wazi kuwa ilifikiwa kwa faida ya taasisi ya Kiyahudi. Hili limebainika kulingana na uchambuzi wa picha za satelaiti na ripoti za hivi karibuni za habari, kwamba jeshi la Kiyahudi lililipua maelfu ya majengo huko Gaza, haswa huko Shuja'iyya na Khan Yunis katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao, na vile vile Rafah, na maeneo yaliyo mashariki mwake ambayo yalishuhudia operesheni kubwa za uharibifu.

Uharibifu mkubwa huko Gaza sio wa bahati mbaya, lakini una malengo ya kimkakati ya muda mrefu, kama vile kuharibu mazingira yanayounga mkono upinzani. Kuondoa Gaza ya miundombinu yake, shule zake na makazi yake, inafanya kuwa ngumu kwa upinzani kujipanga upya au kujenga upya uwezo wake. Hii ni kizuizi cha muda mrefu kwa kuharibu uwezekano na kulazimisha ukweli mpya ambao unaifanya Gaza kuwa dhaifu na kuiacha ikiwa imepooza kiuchumi na haifai kwa makazi, ambayo huandaa njia ya kukubali suluhisho zozote za kisiasa au kiusalama, au hata kukubali wazo la uhamishaji, kwa sababu kuacha Gaza kama kifusi, inafanya kuwa ngumu kwa ujenzi kuwa mikononi mwa watu wake pekee. Badala yake, nchi na mashirika yataingilia kati kwa masharti ya kisiasa, na uvamizi unatambua kuwa yeyote anayejenga upya ndiye anayemiliki uamuzi. Hivyo basi uharibifu wa leo ni sawa na udhibiti wa kisiasa kesho!

Kwa kweli, kuelezea makubaliano ya kusitisha vita dhidi ya Gaza kama "yenye mabomu" haikuwa bure, kwa sababu ilikuwa ya sehemu, na malengo ya madai ya kijeshi hayakujumuishwa, ambayo inaruhusu Wayahudi kuendelea na uvamizi na uharibifu kwa kisingizio cha kiusalama. Vivyo hivyo, ilifikiwa na nchi kubwa zaidi inayounga mkono taasisi bila dhamana thabiti za kimataifa, ambayo inafanya kuwa dhaifu na inakabiliwa na ukiukwaji, haswa kwa kukosekana kwa uwajibikaji wa kimataifa, ambayo inafanya taasisi ya Kiyahudi kuwa juu ya uwajibikaji.

Tutaendelea kuwa taifa lenye unyenyekevu na linalokubali, tukitazama watu waliodhoofika, waliochoka, waliopotea na wenye njaa mpaka lini?! Na juu ya yote hayo, wanaruhusiwa wakati wowote?! Hebu sote tuwe Saladin al-Ayyubi, kwa sababu Gaza leo inakumbusha taifa kwamba Saladin hakuwa tu mtu shujaa, lakini alikuwa kiongozi katika dola iliyokuwa na mradi na jeshi na taifa moja nyuma yake. Kwa hivyo, wito wa kuwa Saladin haimaanishi ushujaa wa mtu binafsi, lakini kufanya kazi ya kuanzisha dola ambayo inafanya watoto wote wa taifa kuwa askari katika safu moja chini ya bendera moja.

Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Mna nini hamkupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto﴾.

Imeandikwa kwa Radio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir

Manal Um Ubaidah

Abdul Malik al-Houthi hachangii kutoka kwa mali yake au mali ya baba yake!

Abdul Malik al-Houthi hachangii kutoka kwa mali yake au mali ya baba yake!

Habari:

Kituo cha Yemen Sana'a kilirusha hewani Jumatano jioni, 2025/11/12, kipindi cha kibinadamu "Nchi Yangu", na katika sehemu ya "Tuko nanyi", kipindi kilionyesha kesi ya mwanamke ambaye alikuwa ameambukizwa ugonjwa adimu na alihitaji kusafiri kwenda India kwa gharama ya dola elfu 80, ambapo kiasi cha dola elfu 70 kilikusanywa kutoka kwa mashirika na wahisani, lakini mtangazaji wa kipindi alizungumzia sana sifa za mchangiaji wa mwisho wa dola elfu kumi, na ikawa wazi kuwa alikuwa Abdul Malik al-Houthi, na alisifu jukumu lake la mara kwa mara katika kusaidia kesi za kibinadamu ambazo zinaonekana kwenye kipindi.

Maoni:

Hakika, mtawala katika Uislamu ana jukumu kubwa, ambalo ni kutunza maslahi ya watu kwa kutumia kile kinachowanufaisha na kutoa kila kitu kinachowafariji. Kimsingi yeye ni mtumishi wao, na hawezi kufurahia maisha hadi atakapohakikisha hali zao. Jukumu hili sio ihsani au upendeleo, bali ni wajibu wa kisheria ambao Uislamu umemlazimisha, na anahesabiwa kuwa amepungukiwa ikiwa atalipuuza. Uislamu umewajibisha umma kumuwajibisha anapopungukiwa. Amani na baraka zimshukie: «Imam ni mchungaji na anaulizwa kuhusu kundi lake». Kwa hivyo, ni upuuzi kufurahia usikivu wa watawala au serikali kwa mahitaji fulani na kuita hiyo kazi ya kibinadamu, wakati kimsingi ni kazi ya kichungaji ya lazima.

Moja ya dhana hatari zaidi ambayo imekita mizizi na ubepari na utawala wake duniani ni kukataa kwa serikali kutunza watu na kuacha utunzaji wa watu kwa mashirika na vyama vya hisani vinavyoendeshwa na watu binafsi au vikundi, na watu huenda kwao mara nyingi kuwasaidia na kutimiza mahitaji yao. Wazo la vyama lilionekana kwanza huko Uropa wakati wa Vita vya Ulimwengu, ambapo familia nyingi zilipoteza wazazi wao na zikawa zinahitaji mlinzi, na serikali, kulingana na mfumo wa kidemokrasia wa kibepari, haitunzi masuala, bali ni mlinzi wa uhuru tu. Matajiri waliogopa mapinduzi ya maskini dhidi yao, kwa hivyo walianzisha vyama hivi.

Uislamu umefanya kuwepo kwa sultani kuwa wajibu wa kutunza masuala ya umma ili kuhifadhi haki zao za kisheria na kukidhi mahitaji yao sita ya msingi ambayo lazima yakidhiwe kwa watu binafsi na vikundi; chakula, mavazi na makazi lazima yatolewe na serikali kwa kila mtu mmoja mmoja, Waislamu na wasio Waislamu, na usalama, matibabu na elimu hutolewa na serikali bure kwa wote. Mtu mmoja alikuja kwa Khalifa wa Waislamu, Omar bin al-Khattab, Mungu amuwiye radhi, akiwa na mke wake na binti zake sita, akasema: (Ewe Omar, hawa ni binti zangu sita na mama yao, walishe, wavishe na uwe ngao kwao kutoka kwa wakati) Omar akasema: (Na vipi ikiwa sitafanya hivyo?!) Bedui akasema: (Nitakwenda) Omar akasema: (Na vipi ikiwa utakwenda?) Akasema: (Utaulizwa kuhusu hali yao Siku ya Kiyama, ukisimama mbele ya Mungu ama kuelekea Motoni au Paradiso), Omar akasema: (Umma huu hautapotea maadamu kuna watu kama hawa).

Enyi Waislamu: Hii sio ndoto, bali ni Uislamu ambao umefanya utunzaji kuwa wajibu kwa Khalifa wa Waislamu kwa kila mtu mmoja mmoja, Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimshukie, alisema: «Imam ni mchungaji na anaulizwa kuhusu kundi lake». Kwa hivyo, lazima turudishe hukumu hizi na kuzifanya ziwe za utekelezaji, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: ﴿Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyomo kwa watu mpaka wabadili yaliyomo katika nafsi zao﴾. Hivyo, kitakachobadilisha hali yetu kuwa haki na ustawi ni Uislamu.

Imeandikwa kwa ajili ya Redio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

Sadiq al-Sarari