Mtafaruku Kati ya Afghanistan na Pakistan
Habari:
Mapigano makali kati ya Pakistan na Afghanistan ambapo ndege za Pakistan zilitumika kukipiga maeneo kadhaa huko Kabul, yaliyojibiwa vikali na vikosi vya ardhini vya Afghanistan katika maeneo kadhaa ndani ya Pakistan, kwa ushiriki wa kundi la Taliban la Pakistan la Pashtun, na kusababisha hasara kubwa ya maisha na mali kwa pande zote mbili.
Maoni:
Hii si mara ya kwanza kwa damu ya Waislamu kumwagika kwenye mipaka iliyoundwa na Uingereza kafiri mkoloni na kusisitizwa na dhana za uzalendo za kijinga, ambazo zinadhibiti utamaduni wa wanasiasa nchini Pakistan na Afghanistan, kwani Uingereza mbaya iliacha nyuma mbegu ya fitna kati ya watu wa eneo hilo, kwa kugawanya maeneo ya makabila ya Pashtun kati ya Pakistan na Afghanistan, ambayo ilizalisha mgogoro wa kudumu kwa makabila haya na mfumo wa Pakistan ambao huchukua aina tofauti mara kwa mara.
Hakuna shaka kwamba nchi za kikoloni kama Amerika na India zinafurahia kuona vita vikishika moto na damu ikimwagika kati ya Waislamu nchini Afghanistan na Pakistan, bali zinaweza kupata mkono wa moja kwa moja ndani yake, haswa kwa kuongezeka kwa tamaa za Amerika katika eneo hilo na kutokukata tamaa na mradi wa ushawishi na udhibiti ndani yake.
Wajibu kwa Waislamu wa Pakistan na Afghanistan ni kufuta mipaka hii bandia kati ya nchi zao, na kuunganisha watu wa eneo hilo katika dola moja ya Kiislamu ambayo inawaunganisha kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake ﷺ, na kutoka mara moja katika hali inayofanana na hali ya Waarabu kabla ya Uislamu, ambapo walisambaratishwa na vita vya kikabila na mizozo ambayo maadui zao waliilisha, na hakuna kilichoizuia isipokuwa kukutana juu ya itikadi ya Uislamu, sheria yake, na dola yake. Mwenyezi Mungu Amesema: ﴿Na wakitaka kukughilibu, basi Mwenyezi Mungu anakutosha. Yeye ndiye aliyekutia nguvu kwa nusura yake na kwa Waumini. * Na akaunganisha nyoyo zao. Lau ungali toa vyote vilivyomo duniani usingaliweza kuunganisha nyoyo zao; lakini Mwenyezi Mungu amewaunganisha. Hakika Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima﴾.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu hilo liwe karibu.
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Sheikh Adnan Mazian
Mjumbe wa Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir